Mh. Rais, fedha zitakazo okolewa kupitia watumishi hewa zitatumika kufanyia nini? Ushauri wangu huu

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
803
551
Habari zenu wakuu!

Mtakumbuka kuwa Rais Magufuli alipoingia madarakani alisitisha kufanyika kwa sherehe za kuwapongeza wabunge na kuzindua bunge jipya baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 mjini Dodoma. Fedha zilizopangwa kufanyia sherehe hizo aliamuru zikanunue vitanda vya wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili.

Vile vile, alisitisha kufanyika kwa sherehe za Uhuru yaani tarehe 9 Disemba 2015 na kuamuru fedha zilizopangwa kufanyia sherehe hzyo zikatumike kufanya upanuzi wa barabara ya Morocco jijijini Dar es Salaa.

Lakini pia, alisitisha kufanyika kwa sherehe za Muungano yaani tarehe 26 Aprili 2016 na kuamuru fedha zilizopangwa kufanyia sherehe hizo zikatumike kufanya upanuzi wa barabara ya Pasiansi - Ilemela - Airport ya jijini Mwanza.

Hivi karibuni ameendesha zoezi la kuwabaini watumishi hewa katika utumishi wa umma na akawaagiza wakuu wa mikoa aliowateuwa mwezi Machi wakamsaidie kufanikisha zoezi hilo. Tunaamini kuwa lengo la kufanya zoezi hili lilikuwa ni kuokoa fedha zilizokuwa zikipotea kupitia watumishi hewa ili kuipunguzia mzigo serikali.

Sasa basi, tumekuwa tukisubiri maelekezo ya Mh. Rais kuhusu fedha zitakazo okolewa kupitia watumishi hewa zitafanya shughuli gani kama alivyo amuru kwenye sherehe za Wabunge, Uhuru na Muungano? Je, atatumia fedha hizo kuajiri watumishi wapya ili kuziba pengo la watumishi hewa? Je, atatumia fedha hizo kuboresha mishahara ya watumishi halali waliopo ili kuwaongezea ari na morali katika utendaji kazi? Je, atatumia fedha hizo kufanyia nini?

Tukiwa tunaendelea kusubiri tamko lake kuhusu matumizi ya fedha hizo, naomba nitoe ushauri wangu juu ya matumizi ya fedha hizi ili kutoa muongozo kama ilivyokuwa kwenye uokoaji wa fedha za sherehe za Wabunge, Uhuru na Muungano.

Kwa kuwa kauli mbiu katika serikali yake ni "Hapa kazi tu", namshauri Mh. Rais Magufuli atumie fedha hizo kuboresha utendaji kazi kwa watumishi wa umma ili kuvuka malengo ya chini, kati na juu kwa muda mfupi. Kivipi? Asiongeze mishahara kwa watumishi ila awaongezee muda wa kufanya kazi kwa kuwalipa malipo ya ziada baada ya kuvuka muda wa kawaida (overtime). Kwa mfano: kama ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 2 itajengwa kwa masaa 8 kwa siku, basi watumishi wanao jiweza kufanya overtime ya masaa 4 watajenga barabara Km 1 zaidi, hivyo watakuwa wanatumia masaa 12 kujenga Km 3 kwa siku ikiwa ni ongezeko la Km 1 kwa masaa 4.

Tukiwa bado tunaendelea kusubiri tamko la Mh. Rais Magufuli kuhusu matumizi ya fedha hizo, Je, wewe unashauri nini kuhusu matumizi ya fedha zitakazo okolewa kuptia watumishi hewa?

Mshua.
 
Back
Top Bottom