Mh Rage ndani ya Tabora

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,707
Reaction score
1,729
Jana kupitia radio yake iitwayo Voice of Tabora mheshimiwa Ismail Aden Rage, mbunge wa Tabora mjini, alikuwa 'live' akiwahutubia wapiga kura wake mjini hapo. Nilimsikia akitoa pikipiki na pesa. Kilichonishangaza ni muda wa mkutano kuendelea mpaka saa moja kasorobo jioni na kumsikia mmoja kati ya wazungumzaji akilalamikia uhaba wa ulinzi (polisi) katika mkutano huo. Wana JF hebu tujadili mambo haya mawili:-
1. Nijuavyo mikutano yote mwisho saa kumi na mbili jioni, au ni ile ya uchaguzi pekee?
2. Kwa nini pawe na ulinzi hafifu wakati mikutano ya vyama mbadala ulinzi huwa mkubwa zaidi?
 
Rage -Simba imemshinda, kaiharibu kabisa na kuwa mdebwedo - Hapa amewasikitisha sana wapenzi wa Tim ya Simba wanamsimbazi.

Rage aliyegeuka mtisha wapigakura kampeni za ubunge Igunga kwa kuonesha Bastola yake majukwaani ovyo kinyume cha sheria.

Rage ambaye akiwa bungeni husahau kabisa majukumu yake na kugeuka kuwa msemaji wa kuitetea na kujibu hoja za serikali kwa mawenge.

Rage huyu sasa amerudi Tabora kutaka kuwashawishi wanatabora kwa mikutano ya mpaka usiku ..............!!!!!!! Ukiona hivyo Hauziki tena bali sasa analazimisha. Tusubiri kama atarudi 2015. Hayo ni mawingu na dalili ya Rage kuchokwa.


 
Rage hasa makazi yake ni wapi?Huyu kilaza Kabla ya kuwa mbunge alikuwa anashinda sana pale kwenye club ya saigon wanachama wengi wa simba wanajua makazi yake ni ilala.
 
Kwa Mh. Rage, wana-Tabora wameumia. Hapo muhimu kwake ni umaarufu na maslahi binafsi. Atafanya longolongo nyingi ilimradi tu apate
 
Kwa kifupi tu Tabora imelala sana kwani haitii akilini kwa wananchi wake kumchagua mtu wa kijiweni kama Rage, ingawa hata sisi tulimchagua mtu asiye na sifa Kikwete.

 


Ukweli ni kwamba jana mimi bahati nzuri nilikuwepo pale kwenye viwanja vya standi ya zamani mjini Tabora: Ukweli uko hivi watu walikuwa wachache sana ila cha zaidi ni Pale Mwampamba ambaye aliambatana na Rage alizomewa sana na vijana na kumuonyesha ishara ya vidole viwili pale tu alipoanza kumsema Mbowe na Zitto. na mkutano nusura uvurugike kwani baada ya hapo katibu wa mbunge naye alizomewa sana na vijana, Rage alihutubia watu wachache mno. Nomba kuwasilisha
 
mkuu rage siku zake zinahesabika kwahiyo muache afanye mkutano ata saa 2 usiku.
 

hana ishu tabora wanamlia kama haamini asubiri next election, pili huyu jamaa ni mfanyabiashara he is not a leader, tatu ukitaka kujua ni mjanja2 muulize hizo piki2 alizotoa zitawasaidia nn wanamboka, atawanunulia wese? mwisho lengo la kugawa pesa ni nn?
 
Uzuri wa ninacholipendea jimbo la Tabora mjini huwa hakuna mbunge anayetawala kwa awamu zaidi ya moja Tangu mfumo wa vyama vingi uanze ingawa mara zote magamba wameibuka kidedea so far.
 
Hakuna mtu wa kumngoa rage tabora. Nadhani wanasiasa wa conservative union wanahitaji kutathmini madhara ya siasa za uongo na kupakaza chuki kama kweli ni mtaji wa kisiasa au ticketi ya kuondokea kwenye ulingo wa siasa. Tusubiri majibu ya serikali baada ya vigogo wa hiki chama kutajwa na wafanya vurugu mtwara kuwa walikuwa wanawapa maelekezo. Kuna haja ya kutoa mafunzo maalum kwa watu wenye elimu za kati na muda mfupi ambao hawakusoma vizuri na wanatamaa ya kuongoza nchi hii watatuingiza vitani pasipo sababu.
 
Rage maharage sitaki hata kumsikia kaifanya simba imekuwa koko wasomali bwana mwingine anaua tembo tu
 
Hapo kwenye red unaweza kufunguka zaidi mkuu?
 
Arudi akagombee somalia, mwizi huyu aliwahi kufungwa kwa kuiba pesa ya FAT simba tukamchagua kuwawenyekiti, ccm nao wakampitisha mgombea tabora wakamchagua mbunge, aibu kubwa hizi!!!

MKUU JAMAA MAHAKAMA ILIMSAFISHA NA SIO MUARIFU KWANI ALISHINDA KESI NA KUONEKANA HAJAIBA

Alitumia ujanja wa mjini kuhakikisha rufaa yake anashinda kumbe alikuwa ana lake jambo, mwanzo nilikuwa najiuliza mbona huyu jamaa ameshapewa msamaha na Rais lakini anaendelea na rufaa, kumbe alichokuwa anataka ni mahakama imsafishe ili awe na sifa ya kushika nyadhifa mbalimbali.
 

Kweli huyu jamaa ni mjanja mjanja kama ulivyosema, unakumbuka kesi yake enzi zile alivyokuwa FAT, pamoja na kutolewa kwa msamaha wa rais lakini alikomaa mpaka rufaa yake ikashinda kumbe shida yake ilikuwa apate sifa ya kugombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…