Mh. Pinda aachie ngazi - wito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Pinda aachie ngazi - wito

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mizambwa, Feb 14, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Pinda aachie ngazi
  Pinda ameonesha udhaifu kama kiongozi na kama mshauri wa Rais.


  Hivi ni kweli tulisubiri hali ifike ilipofika hapa ndio tujue kuwa madaktari kweli walikuwa wamemaanisha na walikuwa tayari kwenda mbele kwa wiki nyingine? Hivi ni kweli watawala walisiburi kuona zile picha za wagonjwa na madripu yao, wazee wakibebwa mzobamzoba na kina mama wakilia mikono yao wakiwa wameachilia kwa kukata tamaa ndio wajue kuwa hali ni mbaya?

  Baada ya kuwawajibisha nusu ya viongozi wa Wizara ya Afya na baada ya hatimaye madaktari wetu kuonesha uzalendo na utu mkubwa wa kurudi wakiwa mikono mitupu hakuna kitu kingine kilichosalia isipokuwa kwa Waziri Mkuu mwenyewe kujiuzulu kwani kwa kufanya hivyo atalazimisha baraza zima la mawaziri kuvunjika.

  Kama Rais Kikwete anaona ni vigumu yeye mwenyewe kubadilisha mawaziri au kuvunja baraza – maana lote linatumika kwa ridhaa yake – na hasa baada ya kuona kuwa siri za baraza hilo zinaonekana kumwaga wazi kinyume na viapo vya mawaziri, basi Waziri Mkuu amsaidie Rais na kuonyesha kuwajibika; kwani kwa kiasi kikubwa mgogoro huu umechochewa na maamuzi ya yeye kuwapiga mkwara madaktari badala ya kukubali kwenda kuonana nao ile Jumatatu ya wiki karibu mbili zilizopita.

  Haiwezekani Waziri Mkuu amshauri Rais kitu kimoja, kikafanyika halafu akarudi na kumshauri kinyume na kitu kile kile na akabakia Waziri Mkuu. Hii ni kanuni ambayo baba wa Taifa aliiweka wazi kwenye suala la Tanganyika pale aliyekuwa Waziri Mkuu John Malecela alipotakiwa kuwajibishwa.

  Pinda alishauri kuwafukuza kazi madaktari waliogoma kutii agizo lake huku akiwaacha viongozi wa wizara na sasa amegeuka na kuwawajibisha wakuu wa wizara huku madaktari wakiachiliwa.

  Baada ya yote yaliyotokea, hakuna jinsi nyingine isipokuwa kwa Waziri Mkuu kujiuzulu kwa heshima, ili naye aende na kufurahia mafao yake ya “kustaafu” kama anavyofurahia yule Waziri Mkuu mwingine aliyejiuzulu naye katika kashfa na sasa anakula na kutanua “ustaafu” wake.


  SOURCE: GAZETI MWANANCHI  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...