SoC03 Mh. Nuru kuweka mwangaza gizani

Stories of Change - 2023 Competition

Pitzachpyiyo

New Member
Jun 10, 2023
1
1
Mh. Nuru kuweka mwangaza gizani

Katika Kijiji kimoja cha Tutafika , nchi ya Gizani, kulikuwa na kiongozi wa kipekee aliyeitwa NURU GIZANI, Jina lake lilimaanisha "kufunuliwa au kuondolewa Kwa maskini" ambapo Gizani ni umaskini na shida zote ", na Nuru ni ujasiri na kujituma kwake. Alivutia na wengi ambapo alipata nafasi ya kuwa kiongozi wa nchi (Rais) katika nchi yake, alitambuliwa Kwa bidii yake Katika kuwatumikia wananchi wake.

Hadithi hii inaelezea safari yake ya uongozi, ukarimu wake na jinsi alivyowatetea wanachi wake, Kwa moyo wake wote na kuwa mfano wa vizazi vyenye ndoto za uongozi. NURU GIZANI alikuwa na ndoto ya kuleta mabadiliko chanya Katika nchi yake, alikua na karama ya kuona nahitaji ya watu wake na kutafutia suluhisho. Alikuwa kiongozi anayejituma na mwenye huruma ambayo aliweka maslahi ya wananchi wake mbele yake mwenyewe akiamini wao ndio chanzo cha maendeleo ya nchi ya GIZANI, alichukia wao walivyokua wakikandamizwa. Nia yake ilikuwa kuwawezesha watu wake na kuwapa fursa sawa za kufanikiwa na kuwasisitiza wajitume na kuheshimu pesa.

Kuanzia siku ya kwanza alipochaguliwa, NURU GIZANI alianza kutekeleza sera na miradi ambayo ililenga kuboresha maisha ya watu ambapo Barabara za viwango vya juu, hospitali, masoko; Aliongeza rasilimali Katika sekta za elimu na afya akiamini kuwa elimu na afya Bora na kufanya kazi Kwa bidii ni nguzo mhimu za maendeleo ya kitaifa. Alihakikisha upatikanaji na huduma hizo Kwa wananchi wore. MH. NURU GIZANI alipokuwa uongozini hakutamani ufisadi was viongozi wengine ulipofanyika hivo aliweka Sheria ataeiba hata shilingi, mali zake zote zitachukuliwa na serikali na pia bungeni ni vitu vya mhimu tu vitaruhisiwa kujadiliwa na wabunge white walipewa utaratibu wa kukaa katika majimbo Yao na kufika makao makuu ya nchi pale vikao vya bunge vinapoanza yote Hii kulahishisha usikilizwaji wa kelo za wananchi.

Na viongozi wa serikali safari zao za nje ya nchi zilitolewa taarifa na Kwa mpangilio maalumu Ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha na wizara za viongozi kwenda kukagua miradi aliweka utaratibu wa kuwa na watu wachache na usafiri wa magari machache Ili kuepusha matumizi makubwa ya fedha. Na hata siku za kusherekea baadhi ya vitu vidogo vinavyogharimu pesa nyingi aliondoa alikua ni rafiki mwema wa MAZINGIRA Kwa maana aliweka siku maalumu Kwa ajiri ya kupanda miti na kusafisha mitaa, kwa vijiji na kata na Kwa nchi, Katika vyanzo vya maji na Kila pahara kiumbe kinapoishi, pia hakuishia Hapo alilinda vyanzo vya maji kwa KUWEKA marufuku kulima karibu na vyanzo vya maji.

Pia alihakikisha idara zote zinatenda haki na kufanya majukumu Yao, mwananchi alipohurika hata Kwa bahati mbaya na wizara yoyote hata ya usafirishaji alihakikisha wananchi, aliomba maoni kwanza "kuvunja makazi Ili barabara ijengwe." Kupitia wizara yake ya majengo na maendeleo na mawaziri wake wote wakishirikiana na kurekebisha makosa ya mipango miji, Kwa kuvunja baadhi ya makazi karibu na barabara na wahisika kulipwa fidia stahiki na baada ya Muda ikafanya nchi ya GIZANI kuwa miongoni mwa nchi zenye ramani nzuri na kuvutia watalii kuja kuangalia ukiachilia mbali kutokana na rasilimali waliokuanazo za utajiri za asili Kaa milima, misitu ya maua ya kuvutia na misitu, maporomoko ya maji na chemichemi za maji moto, ambapo hii ilifanya azidi kusisitiza utunzaji wa MAZINGIRA.

Pia Katika kukuza ajira, alileta pamoja wabunifu wote nchini Ili kuanzisha viwanda na kukuza ubunifu wao na pia aliondoa wawekezaji wanyonyaji na njia zote zilizofanyika kuiba rasilimali za nchi ya GIZANI; Na aliziba mianya yote ya rushwa na kutengeneza gereza la mafisadi na watumiaji wa rushwa na watumiaji wabaya wa madaraka, wafanya buashara wakubwa alihakikisha wnalipakodi kadri wanavyotakiwa Ili kukuza uchumi waa nchi ya Gizani. MH, NURU GIZANI, alisikiliza sauti za wananchi wake, alianzisha programu za kijamii ambapo alikutana na Kila mwananchi wa kilakona ya nchi ya Gizani pia alifanya ziara Katika nchi yote Ili kusikiliza shida zao na kuzitatua au kuweka mipango thabiti, na alifanya ziara mara Kwa mara Ili kuona uwajibikaji Katika programu za maendeleo na kuwa wajibisha viongozi wapuuzi.

Alitambua umhimu wa kuwa karibu na watu wake na kujenga uhusiano thabiti kati yake na wananchi wake, wakati wa changamoto MH. NURU GIZANI alionyesha ujasiri juu ya kuweka Imani ya kujitegemea na kuacha kutegemea makaburu. Hata hivyo alivunja mikataba yote iliyosainiwa nyuma ambayo iliongeza unyonyaji wa rasilimali zao na kuwaongezea madeni nchi za nje hivo kufanya wimbi la umaskini kuendelea kuwapeleka huku na kule bila kujua mwisho wake lini, na pia baadhi ya misaada kandamizi ya kifedha aliikataa na kusema nchi yake ni tajiri sana na alijitolea na kuwapa maisha yake wananchi Kwa kua tayari hata kufa Kwa ajili ya maendeleo Yao, na Hapo alijenga misimamo hata Kwa viongozi wa serikali ndogo na hata kwa wapinzani wakawa hivo wakimuamini na hata watoto wadogo walimpenda maana tumaini lake lake kubwa lilikua kutoka Kwa Mungu wake wa Mbinguni alimwamini daima.

Alijitolea kuhakikisha usalama wa raia wake huku akisisitiza wamutumaini Mungu daima na alitetea haki zao, Kwa uwezo wake na nguvu zote kutokana maombi ya wananchi wake na baraka za Mungu aliishi miaka mingi mpaka kifo cha Hali kumfikia akiwa na miaka 99 na wanachi walipompa jina la (MH. JUA), kutokana na kua aliweza kuwaangazia kutoka Katika Giza ambalo liliwakumba Katika nchi Yao ikiwemo umaskini, ujinga na maradhi pamoja uongozi mbaya ambao haukufikilia kuhusu wao daima Bali ulifikiria maslahi Yao binafsina familia zao, ambapo ulisababisha waishi maisha ya shida Kwa Mda mrefu.

NuAlizikwa Kwa heshima kubwa huku wakiwa na majonzi ya furaha Kwa alipowafikisha na wakitamani arudi, lakini walisema amekufa yeye ila matendo yake hayajafa pamoja na ujasiri na tuliyojifunza toka kwake.
 
Back
Top Bottom