Mh. Mwigulu Nchemba na Uvaaji Wake

neene

Member
Feb 1, 2007
48
61
Ndugu zangu,

Sina budi kumpongeza Mh. Mwigulu Nchemba kwa uvaaji wake wa magwanda. Natamani Watanzania wote tungebuni sare ya magwanda kama anayovaa Mh. Mwigulu Nchemba kwani inaashiria hali halisi ya nchi yetu na kwamba iwe ni kielelezo kuwa inabidi tufanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu hasa ya kuwakomboa watu wenye hali duni ambao wengi wao wanaishi vijijini.

Mimi huwa najiuliza, hivi ujasiri wa kuvaa suti na kufunga tai katika dimbwi la umaskini wa watu wetu tunaupata wapi?

Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea atashika jembe kumsaidia mkulima katika ziara zake vijijini?

Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea kushiriki katika kuchimba mashimo ya vyoo kwenye shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo?

Mambo mengi katika nchi hii yangeweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi kujiletea maendeleo yao. Lakini sitegemei hilo kutokea kama viongozi wetu wataendelea "kuvaa suti na tai" ndani la dimbwi la umaskini uliokithiri wa watu wetu.

Inabidi Waheshimiwa Wabunge walielewe hilo na warudi kwenye majimbo yao wavae magwanda na kufanya kazi na wananchi. Ni aibu kuona tangazo la Haki Elimu wanafunzi wa shule fulani wakisukumana kugombea kuingia chooni eti matundu ya choo hayatoshi! Tukiamua "kuvaa magwanda" na kufanya kazi na wananchi tunaweza kumaliza tatizo hilo ndani ya mwezi mmoja.

Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi. Kwa mfano, hali ya usafi kwenye masoko mengi mijini inatisha miaka nenda miaka rudi. Na tunaendelea "kudunda" tu!

Ni lazima Watanzania tubadilike. Ni lazima viongozi wetu wabadilike.
 
Mzalendo wa ukweli asie na majigambo binafsi hua namkubali sana ni vile tuu hanijui ninavyo mpenda!laati angejua ninavyomkubali angeshanipa hata kazi ya kuosha gari lake
 
Umeongea Mengi lakini sijaona Uhusiano wa uvaaji wa Magwanda ya Mh. Nchemba na kazi ulizozitaja.

Je,umewahi kumuona Mh Nchemba pamoja na uvaaji wake akishika jembe na kuchimba mashimo ya vyoo? Umewahi kumuona akisafisha sokoni?

Mbona kuna viongozi wengi walikua wakiyafanya hayo bila kuvaa magwanda? Unamkumbuka Mh. Deo Filikunjombe (Mungu ampumzishe mahali anapostahili) alipokuwa akipiga kazi na wananchi wake wa Jimbo lake bila hayo magwanda?

Mwisho nikuulize,unafikiri Uongozi ni uvaaji magwanda na kufanya kazi Mtaani?
 
Mkuu inawezekana ndie mwenyewe anajipigia promo
 
Ndugu zangu,

Sina budi kumpongeza Mh. Mwigulu Nchemba kwa uvaaji wake wa magwanda. Natamani Watanzania wote tungebuni sare ya magwanda kama anayovaa Mh. Mwigulu Nchemba kwani inaashiria hali halisi ya nchi yetu na kwamba iwe ni kielelezo kuwa inabidi tufanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu hasa ya kuwakomboa watu wenye hali duni ambao wengi wao wanaishi vijijini. Mimi huwa najiuliza, hivi ujasiri wa kuvaa suti na kufunga tai katika dimbwi la umaskini wa watu wetu tunaupata wapi? Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea atashika jembe kumsaidia mkulima katika ziara zake vijijini? Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea kushiriki katika kuchimba mashimo ya vyoo kwenye shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo?

Mambo mengi katika nchi hii yangeweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi kujiletea maendeleo yao. Lakini sitegemei hilo kutokea kama viongozi wetu wataendelea "kuvaa suti na tai" ndani la dimbwi la umaskini uliokithiri wa watu wetu. Inabidi Waheshimiwa Wabunge walielewe hilo na warudi kwenye majimbo yao wavae magwanda na kufanya kazi na wananchi. Ni aibu kuona tangazo la Haki Elimu wanafunzi wa shule fulani wakisukumana kugombea kuingia chooni eti matundu ya choo hayatoshi! Tukiamua "kuvaa magwanda" na kufanya kazi na wananchi tunaweza kumaliza tatizo hilo ndani ya mwezi mmoja.

Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi. Kwa mfano, hali ya usafi kwenye masoko mengi mijini inatisha miaka nenda miaka rudi. Na tunaendelea "kudunda" tu!

Ni lazima Watanzania tubadilike. Ni lazima viongozi wetu wabadilike.

Mzalendo wa ukweli asie na majigambo binafsi hua namkubali sana ni vile tuu hanijui ninavyo mpenda!laati angejua ninavyomkubali angeshanipa hata kazi ya kuosha gari lake

Wadhifa wako na ulicho post haviendani hata kidogo.
Ni kama Mbingu na ardhi
 
Bila shaka Wewe ni miongoni mwa waliotumwa kuchafua miundombinu across the country kwa kuandika eti "mwizgulu rais"

Nime Magnify andiko lako.
 
Kwa huu uzi buku 7 imeshaingia.
Kweli maisha ni kuchagua.
 
Gwanda ni vazi la kazi na aghalabu huwa la khaki sasa yeye alikuwa ana vaa la kijani pamoja na likofia la MAO, ukiwa mbali unaweza sema ni 'shamba la alizeti' Ila sasa amestaarabika kidogo...naona anajitengenezea 'kajina'...!
 
Gwanda ni vazi la 'wanaharakati' Mwigulu atakua anavutiwa na uvaaji wa Makamanda wa Chadema hivyo akaamua kuiga.Mi pia ninazo gwanda zangu za kaki hua navaa siku moja moja.
 
Ndugu zangu,

Sina budi kumpongeza Mh. Mwigulu Nchemba kwa uvaaji wake wa magwanda. Natamani Watanzania wote tungebuni sare ya magwanda kama anayovaa Mh. Mwigulu Nchemba kwani inaashiria hali halisi ya nchi yetu na kwamba iwe ni kielelezo kuwa inabidi tufanye kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu hasa ya kuwakomboa watu wenye hali duni ambao wengi wao wanaishi vijijini. Mimi huwa najiuliza, hivi ujasiri wa kuvaa suti na kufunga tai katika dimbwi la umaskini wa watu wetu tunaupata wapi? Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea atashika jembe kumsaidia mkulima katika ziara zake vijijini? Mh. Mbunge au Waziri au Kiongozi yeyote akivaa suti na tai utamtegemea kushiriki katika kuchimba mashimo ya vyoo kwenye shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo?

Mambo mengi katika nchi hii yangeweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi kujiletea maendeleo yao. Lakini sitegemei hilo kutokea kama viongozi wetu wataendelea "kuvaa suti na tai" ndani la dimbwi la umaskini uliokithiri wa watu wetu. Inabidi Waheshimiwa Wabunge walielewe hilo na warudi kwenye majimbo yao wavae magwanda na kufanya kazi na wananchi. Ni aibu kuona tangazo la Haki Elimu wanafunzi wa shule fulani wakisukumana kugombea kuingia chooni eti matundu ya choo hayatoshi! Tukiamua "kuvaa magwanda" na kufanya kazi na wananchi tunaweza kumaliza tatizo hilo ndani ya mwezi mmoja.

Yapo mambo mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwahamasisha wananchi. Kwa mfano, hali ya usafi kwenye masoko mengi mijini inatisha miaka nenda miaka rudi. Na tunaendelea "kudunda" tu!

Ni lazima Watanzania tubadilike. Ni lazima viongozi wetu wabadilike.
Promotion zingine hazina tija. Tunataka kazi atuhitaji magwanda, sifia brain ya mwigulu siyo nguo, magwanda hata washika ukuta wanavaa, au Yanga wanaovaa kandambili inamaana wanajua kucheza mpira kuliko Real madrid?
 
You are being deceived.. To me, he is just a creative politician who is positioning himself to "Phish Phools".. nothing more.
 
Mzalendo wa ukweli asie na majigambo binafsi hua namkubali sana ni vile tuu hanijui ninavyo mpenda!laati angejua ninavyomkubali angeshanipa hata kazi ya kuosha gari lake

ninachoshukuru mitusi kaacha kutukana labda kwa kuwa kapewa kitengo ndo maana
 
Back
Top Bottom