Mh. Mwigulu Nchemba kwa aina yako ulichoongea ni siasa hakitoki moyoni

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,757
7,692
Mwigulu Nchemba. Huyu mheshimiwa hata ongea yake Si ile tuliyoizoea amekuwa mnyonge sana.

Hata kama unadai umezunguka mikoa yote kuagiza hili lakini bado hili haliondoi kuwa wewe ni Waziri ndiye unayepaswa kusikika katika hii vita
Iweje upo kimya siku zote unajibu kirahisi hivi kuna nini?
 
Paul Alex. Mkuu kauli ya mwigulu kuhusu ukimya wake alieleza kwa ufupi siwezi kuandika kama simulizi sijajaliwa utunzi.
 
We ulitaka apige kelele ili wakimbie au wapoteze ushahidi? Hili suala si la kisiasa au kupaza sauti, bali ni la kufuatilia kwa kunusa hadi mtu anabambwa na ushahidi.
Tunamuunga mkono Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar juu ya vita hivi, isipokuwa approach aliyotumia ndio wengi tunatofautiana maana wengine tunaona kama vile itasababisha watu kupoteza ushahidi wote na mwisho wa siku vita inaweza isifanikiwe. Katika kupambana na vita hii lazima uwe na mikakati na mbinu sahihi.
 
Hakuna kiongozi mkubwa aliyesapoti vita uchwara ya dar zaidi ya mkuu mwenyewe. Ndio maana hakutaka kusema lolote wakati dogo anajikaanga mwenyewe.
 
We ulitaka apige kelele ili wakimbie au wapoteze ushahidi? Hili suala si la kisiasa au kupaza sauti, bali ni la kufuatilia kwa kunusa hadi mtu anabambwa na ushahidi.
Ushahidi walisha upoteza mtuhumiwa unamtangaza kwa media na ajipeleke polis hapo kuna nn
 
Mwigulu afanye nini wakati Rais wa Dar es salaam ameshafanya kazi yake? Unataka yamkute ya Nape????

"Silence is the point of making a mark" inafaa sana Kwa nyakati hizi tena ukiweza kufunga mdomo Kwa kushonwa hospital ni bora zaidi hasa Kwa wateule Kama yeye!

Songela zigizigi Mwigulu
 
Wakati mwingine najiuliza sana. Wtz. Hivi hatuwazi kuwa nao wana akili kuliko sisi ambao tumejaa hapa JF kupinga tu kila kitu. Eti ametoa ushahidi. Unaona Siro naye kama kazi umemfundisha wewe. Ndo tunalojua wtz kudandia. Hatuanzagi wenyewe ila kudandia hasa issue inayogusa bundle zetu uuuuu mt ataongea weeeee kila lugha. Mpka unashangaa hivi hizo div wanagawa bure au kuna kosa katika uelimishaji wetu. Kila mtu anamajibu. Na katika majibu hakuna negative na positive ya kitu. Ila ingekuwa issue ya kufanya usafi kutumia nguvu kwa afya utaskia kodi tunalipa nk. Tunasahau nchi yetu maskini sana. Lkini pia hatujiulizi kwanini hatukosi bundle la kupiga majungu. JAMANI tatizo ni mtu au ni umuhimu wa Jambo. Kama madawa ya kulevya na mabaya then vita iwe juu ya madawa. Mbona maneno mengi ni kama watu hawataki vita hii. Wanakazania watu na nani kasema nini. Siasa siasa siasa. Afu tunakaa tunapiga kelele nchi hatuoni chochote. Its not about words ,its about words turned into actions .
 
Mwigulu ni mtu mwenye ndoto kubwa alichukua form za Udereva wa nchi, anajulikana nchi nzima 2025 hii hapa usoni hawezi kukurupuka kama Kondakta wa Dar
 
Kwanini hao mapapa walio kamatwa na mtangulizi wako hawakutangazwa kwenye media ili tuwajuwe kwamba niakinanani.Ni jambo la muhimu mnapowakama na ushahidi mtutangazie kwenye media ili tuwajuwe , tutakapo wa ona mitaani wananchi tujiulize wametokaje kwni kesi ya madawa haina dhamana.Sema ndugu waziri hayo malibu yako nirahisi sana.
Umetaka ushauri wa wabunge kwani nyie serikali huwa mnafuata ushauri wa wabunge!!!!!?Hilo bunge limekaa kuwazuga wananchi wasio jielewa,sema kila kitu mmeshamaliza maofisini kwenu.Mnakuja bugeni kuwahadaa wabunge wenu ili wapitishe mawazo yenu wenyewe mliyo yatunga maofisini kwenu.
 
We ulitaka apige kelele ili wakimbie au wapoteze ushahidi? Hili suala si la kisiasa au kupaza sauti, bali ni la kufuatilia kwa kunusa hadi mtu anabambwa na ushahidi.
Tunamuunga mkono Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar juu ya vita hivi, isipokuwa approach aliyotumia ndio wengi tunatofautiana maana wengine tunaona kama vile itasababisha watu kupoteza ushahidi wote na mwisho wa siku vita inaweza isifanikiwe. Katika kupambana na vita hii lazima uwe na mikakati na mbinu sahihi.
Labda inaweza kusaidia kuwatisha wauzaji halisi.
 
Back
Top Bottom