waache tu waandamane ilhali wamekatazwa halafu cha moto na mabomu ya tumboni yatawashukia
hawa cdm hakika ni watovu sana wa nidhamu...
Uwoga uwoga ndio utaacha watu wafe njaa au wasiweze hata kupata lita moja ya maji wakati huyo kamanda wa Police yeye anachezea maji hiv kweli nini maana ya Binadamu wote ni sawa,jamani tokeni muende kwenye maandamano ya haki kama kufa mtakufa kwa haki na kawakamata watakamata wangapi.Stand up for yr right Peoples
Umeona itv saa 12,wakazi wa makongo wanauziwa maji sh 300 kwa ndoo.sasa kama hutaki tuandamane tupe maji safi na salama
Dini zote zinasema tii Mamlaka iliyopo, isitoshe Mamlaka iliyopo ni halali kwa maana tumeichagua kwa wingi wetu, hivyo tuna kila wajibu wa kuitii, kama tunataka mabadiliko tusubiri Uchaguzi ujao, tuangalie tulipoteleza na kujisahihisha tayari kwa kushinda Uchaguzi 2015, ila kwa sasa kuna Mamlaka tuliyoipa dhamana, na hatuna budi kuitii!
Sawa mkuu kwa kuwa wewe unapata maji sawa tuache sie walalahoi kama mtuitavyo tukakumbane na mabomu kwa kudai haki maake tukikaa kimya hatuwezi kupata haki,nani atatupigania kama si CHADEMA??Tutakufa kwa ajili ya haki zetu hata Mungu anatuona hatuandamani kwa kwenda kuua watu wache watupige mabomu tufe au nife kwani hata wewe na wao Police njia yenu ni moja i mean hiyo hiyo tofauti itakuwa mie nilipigwa na kitu chenye ncha kali kama kawaida ya Tanzania Police kila wakiuwa utasikia kapigwa na kitu chenye ncha kali au kaangukiwa na kitu kizito hata sifahamu nani anawapa mafunzo hawa Police na hizi mbinu za kijinga wanazitoa wapi ati kapigwa na kitu chenye ncha KALI

Tatizo ni kwamba kwa kila tukio linalohusisha Mtu kufa au kuumia ndivyo Watu wengi wanavyozidi kujiuliza Maswali kama kweli Wapinzani wapo kwa ajili ya kuwatetea au vinginenvyo, haya mambo hayataki jazba, kitu cha mwisho ambacho Wapinzani wanahitaji sasa hivi ni wananchi kupoteza Imani kwao, na hiyo Imani itazidi kutoweka kila pale Mtanzania anapopoteza Maisha, bila sababu! Tiini Mamlaka iliyopo, basi hata Mungu atawabariki huko mbeleni kwa maana imeandikwa!
Mliipa nyie ambao mnapata maji kila siku na sio sie ambao hatuna maji yaani kama sio Watanzania vile tunatumia maji ya chumvi ilhali kuna watu kama nyie mliowapa mamlaka hao usemao kwa kuwa ulifahamu kabisa kuwa huko ndio ushibako na hamko wengi mshibao kupitia kwa mamlaka hiyo kama sie.
Nani kakuambia haya usemayo kumbuka maandamano hayo hatuendi kuuwa mtu au watu tunaenda kiamani zaidi bila ya fujo iwe lakini mnaogopa maandamano kama mnajiamini?Mie naona mshauriana muache watu waandamane kwa kuwa ni haki ya kikatiba so hata police hawana haki ya kuzuia sema tu kwa Tanzania hutokea kwa kuwa hakuna kiongozi wote wanavunja sheria ati wanasema utawala bora sasa utawala bora uko wapi kama sheria zinavunjwa au mnataka watu waandamane kama wale wagonjwa wa akili wa juzi waliopanga ati kuandamana kwa ajili ya raia wa UK kuikashifu serikali nonsens tunaandamana kwa haki ili serikali iwajibike kwa watu kama wewe pia uliowaweka madarakani.
Amani, amani kwa kiingereza peace! Unaijua wewe! Mwili unahitaji maji kwa asilimia 70 kama siyo 90. Sasa unadhani bila maji utaishi, mh siungi mkono maandamano ila nahitaji maji basi hata kama ni 2015 november ila yaje kwa amani.
Kwani kuna siku hawa watawala na jeshi lao la Polisi walishakubali maandamano ya amani? kama watu wameshafuata taratibu zote ya nini kuja kuwaletea A,B,C,D si wangekataa tangu mwanzo na kutoa vigezo vyao!!vigezo vyenyewe ni wizi mtupu