Mh.Mnyika hii si sawa

Mh.Mnyika hii si sawa

mathabane

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
2,405
Reaction score
1,898
Mh.Kamanda J.Mnyika mbunge wa Ubungo, Nimesikiliza WAPO RADIO kipindi cha yaliyotokea ambapo msaidizi wa mbunge akitoa tamko kuhusiana na kuwepo maandamano ya kesho kinyume na tangazo la jana la kamanda wa polisi mkoa Kindoni kusitisha maandamano hayo.

Mimi nadhani itakuwa sio busara tena kuwashawishi wananchi kuendelea na maandamano ilhali tayari mamlaka zinazohusika kusimamia usalama wa waandamaji zimekunyima kibali cha kufanya hivyo.

Lazima tujifunze kuepuka majeruhi na vifo visivyo na lazima kwa walala hoi kwani maandamano haya hayataleta maji bali mbunge kaa chini na makamanda wenzako kwa kutumia influence yako.
Ninaimani ufumbuzi uko mikononi mwenu bila gharama ya damu ya watanzania.

Ninafahamu nguvu ya harakati katka kulinda heshima na utu wa mtu ila busara ikitawala kiasi cha damu ya kumwagika kitapungua.
 
Umeona itv saa 12,wakazi wa makongo wanauziwa maji sh 300 kwa ndoo.sasa kama hutaki tuandamane tupe maji safi na salama
 
waache tu waandamane ilhali wamekatazwa halafu cha moto na mabomu ya tumboni yatawashukia
hawa cdm hakika ni watovu sana wa nidhamu...
 
Uwoga uwoga ndio utaacha watu wafe njaa au wasiweze hata kupata lita moja ya maji wakati huyo kamanda wa Police yeye anachezea maji hiv kweli nini maana ya Binadamu wote ni sawa,jamani tokeni muende kwenye maandamano ya haki kama kufa mtakufa kwa haki na kawakamata watakamata wangapi.Stand up for yr right Peoples
 
Sawa mkuu kwa kuwa wewe unapata maji sawa tuache sie walalahoi kama mtuitavyo tukakumbane na mabomu kwa kudai haki maake tukikaa kimya hatuwezi kupata haki,nani atatupigania kama si CHADEMA??Tutakufa kwa ajili ya haki zetu hata Mungu anatuona hatuandamani kwa kwenda kuua watu wache watupige mabomu tufe au nife kwani hata wewe na wao Police njia yenu ni moja i mean hiyo hiyo tofauti itakuwa mie nilipigwa na kitu chenye ncha kali kama kawaida ya Tanzania Police kila wakiuwa utasikia kapigwa na kitu chenye ncha kali au kaangukiwa na kitu kizito hata sifahamu nani anawapa mafunzo hawa Police na hizi mbinu za kijinga wanazitoa wapi ati kapigwa na kitu chenye ncha KALI
 
Dini zote zinasema tii Mamlaka iliyopo, isitoshe Mamlaka iliyopo ni halali kwa maana tumeichagua kwa wingi wetu, hivyo tuna kila wajibu wa kuitii, kama tunataka mabadiliko tusubiri Uchaguzi ujao, tuangalie tulipoteleza na kujisahihisha tayari kwa kushinda Uchaguzi 2015, ila kwa sasa kuna Mamlaka tuliyoipa dhamana, na hatuna budi kuitii!

Maji hakuna unatuambia tuwe nanidhamu!!ondoa uoga wako eti maandamano hayata leta maji!!nch zilizo endelea hua wanathamini maandamano na polisi hua wanawapa ulinzi nasio kuwaua so maandamano yako pale pale kwani hatuhitaji kupewa ruhusa yakwenda kuda haki yetu ya msingi kwani bila maji hata gari hazitembei labda ngamia tu.wewe kesho kajifiche utuachie libeneke tulicheze na hawa watnto wetu mapoliceccm tulio wasomesha kwa pesa zetu tena kwa kujinyima nawao wamepigika sema tu wanaroho za kishetani na zakusahau mapema kesho mwenye kijiko kikombe bakuli diaba vidumu ndoo madram njoon nayo tukateke maji kwa waziri na wakitugusa liwake la nch nzima tuone kama mabomu yatatosha
 
Umeona itv saa 12,wakazi wa makongo wanauziwa maji sh 300 kwa ndoo.sasa kama hutaki tuandamane tupe maji safi na salama

Tatizo ni kwamba kwa kila tukio linalohusisha Mtu kufa au kuumia ndivyo Watu wengi wanavyozidi kujiuliza Maswali kama kweli Wapinzani wapo kwa ajili ya kuwatetea au vinginenvyo, haya mambo hayataki jazba, kitu cha mwisho ambacho Wapinzani wanahitaji sasa hivi ni wananchi kupoteza Imani kwao, na hiyo Imani itazidi kutoweka kila pale Mtanzania anapopoteza Maisha, bila sababu! Tiini Mamlaka iliyopo, basi hata Mungu atawabariki huko mbeleni kwa maana imeandikwa!
 
Dini zote zinasema tii Mamlaka iliyopo, isitoshe Mamlaka iliyopo ni halali kwa maana tumeichagua kwa wingi wetu, hivyo tuna kila wajibu wa kuitii, kama tunataka mabadiliko tusubiri Uchaguzi ujao, tuangalie tulipoteleza na kujisahihisha tayari kwa kushinda Uchaguzi 2015, ila kwa sasa kuna Mamlaka tuliyoipa dhamana, na hatuna budi kuitii!

Mliipa nyie ambao mnapata maji kila siku na sio sie ambao hatuna maji yaani kama sio Watanzania vile tunatumia maji ya chumvi ilhali kuna watu kama nyie mliowapa mamlaka hao usemao kwa kuwa ulifahamu kabisa kuwa huko ndio ushibako na hamko wengi mshibao kupitia kwa mamlaka hiyo kama sie.
Nani kakuambia haya usemayo kumbuka maandamano hayo hatuendi kuuwa mtu au watu tunaenda kiamani zaidi bila ya fujo iwe lakini mnaogopa maandamano kama mnajiamini?Mie naona mshauriana muache watu waandamane kwa kuwa ni haki ya kikatiba so hata police hawana haki ya kuzuia sema tu kwa Tanzania hutokea kwa kuwa hakuna kiongozi wote wanavunja sheria ati wanasema utawala bora sasa utawala bora uko wapi kama sheria zinavunjwa au mnataka watu waandamane kama wale wagonjwa wa akili wa juzi waliopanga ati kuandamana kwa ajili ya raia wa UK kuikashifu serikali nonsens tunaandamana kwa haki ili serikali iwajibike kwa watu kama wewe pia uliowaweka madarakani.
 
tatizo ni kuwa kutotii amri halali na mamlaka zilizopo ni tatizo sana mkuu,hawajakataliwa kufanya maandamano bali wametakiwa kuahirisha kwa madai ya kiusalama..sasa kama wanaanza kubishana na mamlaka tutapata breaking newz kesho na magazeti yatauza sana ya jumapili...tuko pamoja sana mkuu ila tusisapoti kila kitu tu kwa kuwa kimesemwa na cdm

Sawa mkuu kwa kuwa wewe unapata maji sawa tuache sie walalahoi kama mtuitavyo tukakumbane na mabomu kwa kudai haki maake tukikaa kimya hatuwezi kupata haki,nani atatupigania kama si CHADEMA??Tutakufa kwa ajili ya haki zetu hata Mungu anatuona hatuandamani kwa kwenda kuua watu wache watupige mabomu tufe au nife kwani hata wewe na wao Police njia yenu ni moja i mean hiyo hiyo tofauti itakuwa mie nilipigwa na kitu chenye ncha kali kama kawaida ya Tanzania Police kila wakiuwa utasikia kapigwa na kitu chenye ncha kali au kaangukiwa na kitu kizito hata sifahamu nani anawapa mafunzo hawa Police na hizi mbinu za kijinga wanazitoa wapi ati kapigwa na kitu chenye ncha KALI
 
Na tunaopoteza wapendwa wetu unadhan hatumjui mchawi wetu? Tunajua. Na ndio maana twaendelea. Kila mtu afanye analohiari. Asietaka kuandamana aache. Anaetaka aende. Uzuri hakuna mtu anafuatwa na gari kwenda andamana. Sio shuruti ni hiari. Mbona mnapenda kuisemea mioyo ya wenzenu? Wakifa juu yao.
 
Kwani kuna siku hawa watawala na jeshi lao la Polisi walishakubali maandamano ya amani? kama watu wameshafuata taratibu zote ya nini kuja kuwaletea A,B,C,D si wangekataa tangu mwanzo na kutoa vigezo vyao!!vigezo vyenyewe ni wizi mtupu
 
Sawa mkuu kwa kuwa wewe unapata maji sawa tuache sie walalahoi kama mtuitavyo tukakumbane na mabomu kwa kudai haki maake tukikaa kimya hatuwezi kupata haki,nani atatupigania kama si CHADEMA??Tutakufa kwa ajili ya haki zetu hata Mungu anatuona hatuandamani kwa kwenda kuua watu wache watupige mabomu tufe au nife kwani hata wewe na wao Police njia yenu ni moja i mean hiyo hiyo tofauti itakuwa mie nilipigwa na kitu chenye ncha kali kama kawaida ya Tanzania Police kila wakiuwa utasikia kapigwa na kitu chenye ncha kali au kaangukiwa na kitu kizito hata sifahamu nani anawapa mafunzo hawa Police na hizi mbinu za kijinga wanazitoa wapi ati kapigwa na kitu chenye ncha KALI

kaka usilie ukombozi umekaribia..hakika Mungu ameyaona mateso ya Watanzania na amenyoosha mkono wake kutukomboa hata wafanye nn hawawezi kuzuia..
 
Tatizo ni kwamba kwa kila tukio linalohusisha Mtu kufa au kuumia ndivyo Watu wengi wanavyozidi kujiuliza Maswali kama kweli Wapinzani wapo kwa ajili ya kuwatetea au vinginenvyo, haya mambo hayataki jazba, kitu cha mwisho ambacho Wapinzani wanahitaji sasa hivi ni wananchi kupoteza Imani kwao, na hiyo Imani itazidi kutoweka kila pale Mtanzania anapopoteza Maisha, bila sababu! Tiini Mamlaka iliyopo, basi hata Mungu atawabariki huko mbeleni kwa maana imeandikwa!

Hivi kati ya anayedai haki yake kwa amani na anayeua watu kwa makusudi nani anatii mamlaka. Ni upuuzi kupenda kutisha watu wakati wanaumia, wakati nyie na wakubwa zenu mnaishi maisha yasiyolingana na mtanzania wa kawaida, nyie ndio mnaopata dhambi na mlaaniwe. Jiulize aliyekuwa kipenzi cha watanzania inakuwaje siku hizi amekua adui yao? Mara polisi wanyanyase waendesha bodaboda yani ni tabu tupu,waambie hao unaowatetea kwa kigezo cha kutii mamlaka watende haki uone km watu wataandamana
 
Amani, amani kwa kiingereza peace! Unaijua wewe! Mwili unahitaji maji kwa asilimia 70 kama siyo 90. Sasa unadhani bila maji utaishi, mh siungi mkono maandamano ila nahitaji maji basi hata kama ni 2015 november ila yaje kwa amani.
 
Mliipa nyie ambao mnapata maji kila siku na sio sie ambao hatuna maji yaani kama sio Watanzania vile tunatumia maji ya chumvi ilhali kuna watu kama nyie mliowapa mamlaka hao usemao kwa kuwa ulifahamu kabisa kuwa huko ndio ushibako na hamko wengi mshibao kupitia kwa mamlaka hiyo kama sie.
Nani kakuambia haya usemayo kumbuka maandamano hayo hatuendi kuuwa mtu au watu tunaenda kiamani zaidi bila ya fujo iwe lakini mnaogopa maandamano kama mnajiamini?Mie naona mshauriana muache watu waandamane kwa kuwa ni haki ya kikatiba so hata police hawana haki ya kuzuia sema tu kwa Tanzania hutokea kwa kuwa hakuna kiongozi wote wanavunja sheria ati wanasema utawala bora sasa utawala bora uko wapi kama sheria zinavunjwa au mnataka watu waandamane kama wale wagonjwa wa akili wa juzi waliopanga ati kuandamana kwa ajili ya raia wa UK kuikashifu serikali nonsens tunaandamana kwa haki ili serikali iwajibike kwa watu kama wewe pia uliowaweka madarakani.

Naelewa machungu yako, lakini hayabadilishi ukweli kwamba Mamlaka iliyopo imechaguliwa na Watanzania kwa wingi wao, wenye maji na wasio na maji, wenye umeme na wasio na umeme, Maskini na Matajiri hivyo wote kwa ujumla wetu hatuna budi kuitii, ndio demokrasia yenyewe hiyo, na kama tunaona haitutendei haki tuna uwezo wa kuibadilisha 2015 na kuweka Mamlaka ambayo itafanya yale yanayotupendeza, ila kwa sasa hatuna jinsi!

Isitoshe hata Wapinzani nao siku moja watapewa Mamlaka ya kuongoza na Watz, ninaweza kukuhakishia sio 100% yetu tutawachagua, lkn kwa kuwa wengi watakuwa wamewachagua wengine tuliobaki tutakuwa hatuna budi pia kutii Mamlaka watakayokuwa nayo, sasa kama kila mtu akisema kwa kuwa hapendezwi na maamuzi ya Mamlaka iliyochaguliwa kihalali aandame hata kama Mamlaka imemkataza, pia wao watashindwa kuongoza, na watatumia njia zilezile ambazo Mamlaka ya sasa hivi inatumia, hakuna jipya Dunia hii tumeona Afrika Kusini, ANC wanatumia jeshi lile lile na mbinu zile zile kuuwa watu walewale waliokuwa wanawapigania miaka yote!

Demokrasia ni ngumu sana!
 
Amani, amani kwa kiingereza peace! Unaijua wewe! Mwili unahitaji maji kwa asilimia 70 kama siyo 90. Sasa unadhani bila maji utaishi, mh siungi mkono maandamano ila nahitaji maji basi hata kama ni 2015 november ila yaje kwa amani.

Ujumbe Mzuri sana na umetulia! Hata mimi nataka mabadilko lakini siko tayari kuiharibu Tanzania yangu, na ndio maana mimi naunga mabadilko lakini ya Amani tu na si vinginevyo, hivyo kama Serikali imekataza maandamano watu watii, lakini na uhakika ujumbe umefika, na 2015 tusiwachague!

Kwani kuna siku hawa watawala na jeshi lao la Polisi walishakubali maandamano ya amani? kama watu wameshafuata taratibu zote ya nini kuja kuwaletea A,B,C,D si wangekataa tangu mwanzo na kutoa vigezo vyao!!vigezo vyenyewe ni wizi mtupu

Haijalishi, Maandamano yamekatazwa na Serikali na hatuna budi kutii na Si vinginevyo, hasira zetu tuzipeleke kwenye Uchaguzi 2015!

Maandamano nihaki yetu hatuwezi kusubiri mpaka 2015 kwani nch sasa ishakua kichwa cha mwenda wazimu,wanao tuongoza hawajitambui wala hawajiamini
 
Back
Top Bottom