Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Inaonesha ukarbu wa mh Mkapa na rais wa sasa mh Magufuli ni wa siku nyingi.
Lakini kwanin angalau Magufuli hauigi mazuri ya mh.Ali Hassani mwinyi ukayaweka kisasa,ukachukua ya mkapa ukayaweka kisasa,ukachukua ya Jk ukayaweka kileo zaidi mabaya au walipoteleza unapaboresha ili tu nchi iende mbele.
Kama hujui wapi pa kuanzia mimi leo nakuonesha.
HOTUBA.
Nitajikita zaidi kwa mh.WB mkapa.mtu huyu alikuwa mzuri kutoa hutoba na inawezekana aliiga baadhi ya vitu toka kwa Mtangulizi wake,naye akaboresha kidogo na tulikuwa tunamuelewa,vivyo hivyo kaja Jk na utaratibu wa kuongea na wazee wa Dar nakwingineko,na muda mwingine vijana lakini lengo ni kama Rais kuwa adimu maskioni na machoni kwa wananchi ili kutengeneza a well determined interaction with the people you lead.
Najua kama mkapa alikuwa na vimaneno vigumu akiwa amechukia,tulijua kuwa sasa Rais kuna jambo limemkera.
Na hata alipohutubia wakati wa furaha tulijua pia;kwa mfano alipenda sana kusalamia vijana kwa neno "mamboooo!"huku akilisindikiza na tabasamu la kiu-Rais,wakati wa huzuni vile vile alihutubia tukajua sasa taifa linahuzuni..nakumbuka matukio mawili aliyohutubia akiwa anatangaza kifo cha baba wa taifa 1999;na ajali mbaya ya MV BUKOBA nilikuwa mdogo lakini hadi leo nakumbuka kutokana namna matukio yale yalivyotangazwa nk.
Mh.Rais binafsi nashindwa kukujua wapi una furaha,wapi umenuna,na wapi una majonzi.muda wote una foka na ka kuonesha tabasamu la usoni(sio moyoni).
Mkuu ili wewe mwenyewe kuepuka kutoa kauli zinazokinzana,kuudhi au kuwatia hasira wanachi.tengeneza mazingira ya waaandishi wa habari,wananchi "wakumiss!"...
Usipende kutolea maelezo kwenye kila jambo wewe mwenyewe.
Mambo madogo madogo waachie wasaadizi wako watolee maelezo."waamini na waache wajiamini"
Lakini pia HOTUBA ZAKO ziwe na ajenda *ikiwezekana moja tu kwa hotuba.ikiwezekana ziwe prepared ili ukwepe kutamka vitu kwa hasira au kwa mihemko.Lakini zaidi ili kuhakikisha ulichotaka kuongea kieleweke kwa watu wote vizuri.
Panga muda wa kuongea na taifa lako,inaweza kuwa kila mwezi au baada ya meizi kadhaa ili kuleta
UADIMU wako,na kujenga hamu ya watu kuhitaji kukuskiliza.
Vinginevyo utazoeleka sana na utahisi magazeti yanakupotezeaa kumbe ni hio style yako ya kuongea mara kwa mara kwa kila jambo kunafanya unakuwa common sana kwa watu wako.
Kiufupi kama unaweza muige mkapa kwa kipengere hiki cha hotuba.......nakuonea huruma sana kuhangaika na Bashite kama rais hauitendei haki taasis hio...
Likija kukaa vibaya kwa mfano nani atalisemea mwishoni?
wewe ndio Rais, kuwa adimu kwenye baadhi ya mambo ili yasije yakawa fimbo ya kukuchapia 2020 nahata ukiwa umestaafu...mara mia kaa kimyaa ukiwa unajua nini kipo moyoni mwako.
[HASHTAG]#Mwene[/HASHTAG] chungu