Mh.Membe aiteka Kanda ya Ziwa.

Bwana Kiwuyo

Member
Joined
Oct 6, 2013
Posts
8
Reaction score
3
Ni nadra sana kwa wanasiasa nchini kukubalika kwa kiasi kikubwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na ushindani mkubwa wa kisiasa nchini hususani ndani ya Chama Cha Mapinduzi.Ila Mh.Bernard Kamillius Membe kwake imekuwa tofauti.

Jana akiwa ameongozana na kundi la marafiki zake,wafuasi wake na wanachama wa Ccm alizuru jiji la Mwanza saa moja usiku na kulakiwa na maelfu ya wasanii wa filamu,muziki na wananchi wa kila rika waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha kwa upendo mkubwa jijini Mwanza.

Halikuwa jambo dogo,kila aliyekuwepo hakuamini kilichotokea.Mh.Membe ana wafuasi ambao hata yeye hakuweza kuelewa wametokea wapi.Kila mmoja alitaka kuongea naye,kumshika mkono au kupiga naye picha.Chama cha waendesha bodaboda mkoa wa Mwanza walijitolea pikipiki zao bure kuongoza msafara wa kumlaki Mh.Membe.

Wananchi walikuwa wakiimba;"Membe jembeee,Membe oteshwa,Membe usitusahau wakazi wa Mwanza tunakuunga mkono".

Ilikuwa ni kama Mandela amezuru jiji la Mwanza.Historia imeandikwa rasmi,na huu ni mwanzo tu.Kilio cha wasanii kimesikika kutokana na kiu yao kubwa ya kuwa karibu na Mh.Membe na kusaidiwa matatizo yao yanayosibu tasnia ya filamu.


Wasanii walioongoza msafara wa kumpokea Mh.Membe wote wana ushawishi mkubwa nchini kama vile Mjomba Mpoto,Steven Mengele Nyerere,Adam Melele"Swebe Santana Nunda",Blandina Chagula"Johari",Wastara Juma,Cathy Rupia na Kulwa Kikumba almaarufu kama Dude.

Mh.Membe alikuwa kaalikwa kuzindua filamu iitwayo I Love Mwanza ikiyoandikwa na Adam Melele almaarufu kama Swebe Santana Nunda.Mh.Membe kaahidi neema kwa wasanii nchini.Kakubali kuwa baba wa hiari wa wasanii wote wa filamu nchini.

Mh.Membe pia katika msafara waje aliungana na Mh.Lazaro Nyalando,Mnec Christopher Mwita Gachuma,Paul Christian Makonda na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Waziri Rajab.

Jana Mh.Membe baada ya kuizindua filamu hii ya I Love Mwanza rasmi leo atakuwa Ccm Kirumba akikamilisha ratiba ya tamasha kubwa kuhusu sanaa kwa wakazi wa jiji la Mwanza.Wote mnakaribishwa!

Imetolewa na:
Friends Of Hon.Membe
 

Attachments

  • 1403419664758.jpg
    32 KB · Views: 701
Kumbe aliteka wasanii wa filamu , naye ni kuigiza tu kama kaka yake!!!!!!!!!!
 
hahahahahahaha umati uko wapi, akili hizi ndogo za mama salma zitawaharibu
 
Yaani walikuwa wanamlaki kama nani? Hebu fafanua. Kama ni urais, hatumuhitaji "dhaifu" mwingine aingie pale Magogoni.

Tiba
 

What is so special here! Wasukuma wa Mwanza walipata bei nzuri ya pamba, wananchi wa Kanda ya ziwa walipata meli mpya ziwa Victoria hasa wale wa mkoa wa Kagera!? Huu ni uzinduzi wa movie wa kwanza Mwanza au popote tanzania? So what is so special? Hii ni dhihaka, unamlinganisha Membe na Marehemu Nelson Mandela, the Great Man of Africa, the peace maker and freedom fighter wa kupigiwa mfano.
 
Sijaona umati hapo zaidi naona mijitu miwili tu tena mifisadi sasa sijui ndo umati hio.
 
Membe ana fit ktk wizara aliyo nayo, hakika hilo halina ubishi lkn ktk Ukuu wa nchi yetu bado hajaiva vya kutosha.
 
Sasa huo umati wenyewe uko wapi? By the way hii kazi ya kuzindua na kuwa karibu na wasanii si ilipaswa iwe ya Waziri wa vijana, sanaa, utamaduni na michezo sasa huyu membe na Nyalandu hizo ndio kazi zao....?
 

Kwa hyo nayeye kaamua kua msanii kama kaka yake.
 

Punguza manjonjo sema amelakiwa na wasanii toka dar aliowalipia ticket za ndege kuja kumpokea huku mwanza.
 
Membe bana anajaribu kuvaa uhusika asiokuwa nao,

eti anajijengea image ya kuWa mgombea Urais
hii nchi tunachezewa sana akili zetu
 
maembe kalakiwa na wananchi au wasanii wa dar unataka kutuaminisha nn?
hao friend of han membe wana nia gani? kama urais hapati mwacheni atumie hela zake vibaya
hatutaki wasanii pale magogoni huyu aliepo anatosha
 
Hii habari ungepeleka kwa Shigongo akaandike kwenye magazeti yake, yaani na wewe unajiita mfikirishi mkubwa, unaleta habari kama hii mtu akutane na wasanii uanze kutueleza amekutana na maelf ya wananchi!!!! Hafu si amepigwa marufuku asifanye siasa hadi mwaka kesho februari!

 
This is too low for membe. Kuwalipia tiketi za ndege wachumia tumbo Ally Salum Hapi na Paul makonda na kujifanya wakazi wa mwanza ili kupata attention ya kanda ya ziwa ni kufilisika kisiasa.
 
Hatutaki wacheza ngoma...nchi viongozi ni safari na matamasha
 
unaongelea kanda ya ziwa ipi? Hii niliyopo mimi au? Labda ziwa magharibi!
 
unaongelea kanda ya ziwa ipi? Hii niliyopo mimi au? Labda ziwa magharibi! Dhaifu mwingine hana nafasi Tz.
 

Kaka memmbe pole kwa kuzungukwa na marafiki vilaza kama huyu aliyepost hii nyuzi, huwezi hata siku moja ukapima wingi wa mashabiki wako huku umezungukwa na wasanii. Wafundishe wapambe kutokuwa waongo kwako kwa asilimia 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…