Mh. Lukuvi - Baada ya kulipia kodi ya ardhi maeneo yetu yatambuliwe ki-sheria

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
33,106
40,363
Mh. Lukuvi, sisi wananchi tupo tayari kuyalipia maeneo yetu ambayo tunamiliki ki mila, ama tumeyanunua na tuna hati za mauziano zilizosainiwa na wenyeviti ama watendaji wa serikali za mitaa mbalimbali hapa nchini.

Ombi kwa Waziri Lukuvi, tunaomba pia utuwekee utaratibu ndani ya Wizara yako kwamba baada ya kulipa kodi maendeo yetu ambayo hayajapimwa na hayatambuliki ki-sheria, tunaomba utuwekee utaratibu ili mashamba haya yatambulike kwa muda mpaka hapo serikali itakapokuja kuyapima rasmi.

Umiliki huo wa muda wa kisheria utatusaidia sisi kufanya yafuatayo:-
1. Kuyaendeleza kupitia vibali maalum toka Wizara na Halmashauri husika.
2. Kuyakodisha kwa wawekezaji wa mikataba inayotambulika ki-sheria
3.Kukopa toka taasisi za fedha yakiwemo mabenki wa kutumia hati hizo za muda kama dhamana.
4. Kuuza kwa bei ya soko endapo muhitaji atapatikana hasa wawekezaji.


Tunahitaji mwongozo na taratibu kutoka wizara yako tadhadhali maana jambo hili ni jema.
 
Back
Top Bottom