Mh. Lukuvi acha siasa kwenye swala la hati za viwanja

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,558
2,854
Hoja yangu itajikita kwenye hili swala la watu wenye Offer wanaostahili kupata Title deed(Hati ya kumiliki kiwanja).
Naishi ilala,nina kiwanja changu nilichopimiwa na kupewa ofa mwaka 2009.toka kipindi hicho nilifuatilia hati mpaka nikachemsha baada ya kutapeliwa hela nyingi za rushwa na watendaji wa Wizarani/upimaji wilaya ya ilala.
NIlipata matumaini mwaka huu mwanzoni mh.Lukuvi.alivyotoa tangazo kuwa wenye ofa tukachukue HATI ndani ya miezi mitatu.nilienda kwa afisa ardhi ilala toka mwezi wa tatu sijapata hati ni usumbufu tu mara hatuna vifaa/faili hatulioni/mhusika kafiwa/subiri barua ya kukupa uende wizarani/ulipimiwa miaka mingi teknologia imebadilika/ulichelewa kulipia ofa yako/hakuna mtandao nenda wizarani!

kwa ufupi anachotamka waziri na tunachokikuta Ardhi ni vitu viwili tofauti wale watendaji wanaonyesha hawana habari na tamko la waziri/hawajari utendaji wao wa kazi haujabadilika.japo nikiri kuwa swala la rushwa limepungua kwasasa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma.

Naomba Mh.LUKUVI focus kuwanoa wafanyakazi wako waende sawa na maono yako/ya wizara.kwasasa unatuchosha tu.wale jamaa wanapigakazi kwa mazoea.

karibu kama kuna mhanga mwingine
 
Back
Top Bottom