Mh. JK tairi inazunguka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. JK tairi inazunguka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Jan 20, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  JK akiwa anaendesha gari kwa spidi ya ku achieve MDG 2015 na kupunguza umaskini mara anakuta vijana barabarani na kumtania " dereva tairi inazunguka" mara anasimamisha gari na anashuka na kuanza kukagua matairi kana kwamba hayatakiwi kuzunguka. Kisha anawakemea wale vijana na kuunda tume ya kuwachunguza na pia anamtuma Pinda kuongea na vyombo vya habari kwa gharama ya walipa kodi. Baada ya miezi kadhaa kupita safari inaanza tena na akiwa kwenye spidi ileile anakutana na watoto wanatoka shule mara hii wana mtania "dereva hujawasha taa" . Mara hii anasimamisha gari anashuka na kuangalia kama kweli hajawasha taa kana kwamba mchana gari huwa linawasha taa. Mara anawatuma wasaidizi wake wawakemee wale watoto na kisha anaunda tume akiwamo waziri wa elimu na waziri mkuu na mkuu wa mkoa kufuatilia ile kashfa ya kutaniwa na hawa dogo. Tume hii inapewa miezi mitatu tu iwe imetoa taarifa.

  Akiwa hajaanza safari mara Vyuo vikuu vinaanza mgomo na hapo anaitisha vikao kadhaa na hapa anamtuma mkuu wa polisi aawatulize wanafunzi na inashindikana then anaunda tume kufuatilia matatizo ya wanafunzi kana kwamba hayajui.Kisha anamtuma Pinda kuongea na jumhiya ya Chuo kikuu.

  Kabla pinda hajatulia wanaharakati na wasomi wanaandaa kesi ya kukataa kulipwa kwa DOWANS na hapa baadhi ya mawaziri wanaanza kuwaunga mkono. Jk anamwomba waziri wa utawala bora awakemee mawaziri na hapo anajiandaa kuanza tena safari ya kuifikisha Tanzania 2015.
  Kabla safari hii haijaanza ghafla anafariki jaji mstaafu na safari inahairishwa kwa siku mbili tu na hapo lazima JK ahudhurie mazishi na kuifariji familia.

  Jk anajiandaa tena na kabla safari haijaanza tena mabalozi wapya wanawasilisha hati za utambulisho na lazima akawapokee Ikulu.

  Hapa JK anamaliza shughuli zote na safari inaanza ila kabla hajafika hata KM moja anapewa taarifa kuna gazeti limeandika eti kikao cha Chama kinaenda kuwafunga midomo akina nani na hapo anahairisha safari. Na anaitisha kikao cha dharura na katibu wake mkuu kiongozi kisha anamwaagiza akanushe na atoe taarifa kwenye vyombo vya habari ndo aendelee na safari.

  Anapotaka kuanza safari tena anaitwa kushuhudia Mr. Mugabe akiapishwa na kipindi hiki anawahi siku mbili na kupitia kwanza South.

  Then anarudi Tz baada ya siku 5 kwani pia alipitia tena South kumpa pole waziri X aliyekuwa amelazwa huko.

  Akiwa njiani anarudi anapewa taarifa kwamba kule same kwa mama Anna kuna maporomoko na watu wamepoteza maisha na inabidi ili kuonyesha solidarity aende kuwafari na hapa helkopta inaandaliwa mara moja na kesho yake safari inaanza.

  Mwaka unaisha na tarehe 31 Deecember tunatangaziwa kwamba JK atatoa hotuba ya kumaliza mwaka na pamoja na mambo mengine ataeleza mafanikio ya uongozi wake katika kipindi cha mwaka huu uliopita na mikakati ya mwaka unaofuata. Muda wa kuangalia hotuba unafika na mara wimbo wa taifa unapomalizika umeme unakatika!!!.


  Wanjameni kweli hayo maendeleo tunayoambiwa haswa kufikia malengo ya millenia 2015 huyu mkuu atatufikisha kweli. Mbona safari ya kufika huko inakumbwa na interruptions ambazo ni za kujitakia? interruptions ambazo haziwezi kumkwamisha mtu serious kuendelea na safari ya kuwaletea watanzania maendeleo?.

  Mbona tunaacha ku focus kwenye target tunapambana na mabo madogo yasiyo na tija kwa maendeleo ya watanzania?
  Angalia mwaka umeisha na hukufika ulikokuwa unakwenda na inawezekana ukianza safari tena gari likawa haliwaki kutokana na mafuta ya kuchakachua.

  Viongozi wetu lets stick to the targets hebu ifike mahali tuwe serious na tusiwe kama hatuna malengo. Inabidi tujue wakati ni ukuta. Viongozi Kupoteza muda kupambana na magazeti na waandamanaji wakati kuna mambo ya msingi ya kupambana na umaskini ni kutokuwa serious na kukosa dira.

  Hivi kuonya gazeti au kuvunja maandamanoau kukejeli vyama vya siasa kuna msaidiaje mkulima ambaye amekosa mazao kutokana na ukame?

  HIVI TUNAJUA TUNAPOTEZA MUDA HUKU SIKU ZIKISONGA? TUJUE MAENDELEO HAYATUNGOJI .
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kikwete............a leader with neither mission nor vission!/..........yupoyupo tu....masheikh na maprofessor wa madrasa ndiyo wasemaji wake wakuu?...............tumeuziwa mbuzi kwenye gunia......
   
 3. Shomoro

  Shomoro Senior Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo
   
 4. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kajaza mashemeji, mahawala, maswahiba kwenye uongozi hana lolote tunahiji mabadiliko....
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,740
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Nani aliwaambia mumchague awatawale? Ni kwa vigezo vipi mlimchagua?
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Muulize tendwa na tume yake ndo walimtangaza kuwa raisi,.....hakuna mtanzania aliye mchagua hapa unapo uliza,...
   
 7. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu m2 aliiba kura,wt walidhamilia kufanya mabadriko
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Std 7 questions: 1. Jadili mtunzi alikuwa na dhamira gani? 2. Tunga kichwa cha habari. 3. Je mhusika mkuu ni mfano wa kuigwa ktk jamii? 4. Mhusika mkuu ana elimu gani? 5. Toa uhalisia wa mhusika mkuu na mazingira yanayomzunguka. 5. Mtunzi ametumia mfumo upi ktk kufikisha ujumbe. 6. Fupisha adithi yake katika maneno manane tu. (marks 100) note: (a)all questions carry no mark). (b)don't attempt the second question bcoz its answers are: msafiri/traveller or waziri wa mambo ya nje kivuli or handsome boy or fisadi or kilaza or none of the above.
   
 9. e

  eddy9811 Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 5
  thats funny. napenda maswali
   
 10. m

  matawi JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hatujamchagua sisi ni Usalama wa taifa wakisaidiana na Makamba
   
 11. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anazo Digrii nyingi za kuchakachua!
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  a leader? leader of what and who? he is a ruler and follower
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Yaani hapo umeandika robo ya theluthi ya mambo yote, nimekukubali yaani hata yule aliemtungia kitabu chenye pg 300 ni sawa, kumbe na sie tukiamua kuyalist hapa yatazidi kurasa na maneno ya kwenye encyclopedia kadhaa!!!
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Hivi anafaa kua hata monitor kweli?
   
Loading...