Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba

Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba

Inasikitisha na kushangaza..tumekua na mihemko ya kisisa na ushabiki usiokua na tija..hamna mtu anakaa chini tena anasoma vitu kwa undani , hamna mtu anakaa tena anatafakari mambo kwa undani, ni kukurupuka tu.. Na wale watu wenye uwezo mdogo kwenye mambo ndo wapo mbele..unadhani tutafika kweli..!
Mkuu hatufiki kwa mwendo huu ikiwa hata wasomi wameamua kuweka elimu zao kapuni. Wale watu wenye uchungu na nchi yetu wameishia wapi jamani. Inauma sana unapoona mtu yupo radhi kutetea maslahi binafsi na kuacha maslahi ya nchi tena wako tayari hata kuitwa majina mabaya ili mradi tu wanajiwekea sifa kwa wahusika ili baadae waweze kukumbukwa kwenye ufalme. Wengine wazee maskini ya mungu ukijiuiza hivi huyu hata akipewa 20yrs ya kutawala atakua na hali gaini , yaani ili mradi tu wafie kwenye uongozi. Kwa mtu mwenye kufikiri hawezi kutamani kuwa mtawala wa tz kwa hali ilivyo sasa kwani kuna purukushani nyingi . Ni ngumu sana kuondoa mitazamo ya kidini iliyojengeka miongoni mwa wananchi, rushwa , umasikini uiokithiri na zaidi watu wamezoea mipasho ukiwaambia kufanya kazi watajiuliza je wewe ni dini gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom