Jaji Joseph Sinde Warioba hana 'bifu' na mtu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,348
Reaction score
26,144
Pamoja na kusemwa,kukosolewa,kukejeliwa,kuombewa dua baya na kutajwatajwa kwa kiburi na kejeli ndani ya Bunge Maalum la Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba amebaki alivyo. Uzalendo wake kwa nchi;utii wake kwa chama tawala-CCM,weledi wake wa kiuongozi na kitaaluma umemuweka Jaji Warioba kuwa mtu wa kipekee.

Jaji Warioba anaijua nchi hii zaidi ya mamilioni ya wananchi wa Tanzania.Anaijua ilipotoka,ilipo na inakokwenda. Jaji Warioba anawajua viongozi wote wakuu wa nchi hii-kuanzia Mwalimu Nyerere hadi Rais Kikwete. Anaujua uimara na udhaifu wa kila mmoja. Kutokana na kuiva kwake kiuongozi,anabaki na mambo yake akilini na moyoni mwake.

Jaji Warioba hana 'bifu' na mtu. Angekuwa hivyo,mara kwa mara angejitokeza kupambana na wanaomsema.Hafanyi hivyo.Kila akiongea,hujielekeza kwenye Rasimu ya Tume yake na kuitetea. Uzalendo wa Jaji Warioba umejidhihiri leo katika Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Alijitokeza kwa heshima,utii na unyenyekevu mbele ya Rais Kikwete kupokea zawadi yake aliyotunukiwa. Hakujificha;hakusita.

Mungu akupe maisha marefu Jaji Warioba na uione nchi hii ikineemeka!
 
Kama uzalendo ndio unapimwa hivyo, hiyo kali. Bifu zipo kwetu huku uswahilini...wenzetu hao wanamakubaliano...
WeWe unadhani kamati ile ya maridhiano ina kazi gani...NIPE NIKUPE AU MIE NANUFAIKA VIPI!!!
Ila lazima uonyeshe utii kwa Rais....,tii mamlaka
 
Nikwl kbs mkuu kwan kikwete mbona ni mswahili? Anapuliza na king' ata kama panya bukwa? Warioba watanzia wengi wanamkubal sn tu
 
Mungu amtie nguvu,baraka,hekima na hata kuendelea kumpa kwa kumuongeza weledi jaji warioba.hakika utaendelea kuheshimika ktk nchi hii ya tanganyika.bakiwa kutukuzwa,kusifiwa,kuheshimiwa na hata kuenziwa kupitia msimamo wako juu ya kuipenda nchi hii ya tanganyika.uzalendo wako hakika una htajika kwa watanganyika wengi.hakika warioba ataenzia pamoja kiongozi
 
Hongera zake.Kwenye ukweli uwongo hujitenga,kuna siku watamtafuta lakini watakuwa wamechelewa.
 
Pamoja na kusemwa,kukosolewa,kukejeliwa,kuombewa dua baya na kutajwatajwa kwa kiburi na kejeli ndani ya Bunge Maalum la Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba amebaki alivyo. Uzalendo wake kwa nchi;utii wake kwa chama tawala-CCM,weledi wake wa kiuongozi na kitaaluma umemuweka Jaji Warioba kuwa mtu wa kipekee.

Jaji Warioba anaijua nchi hii zaidi ya mamilioni ya wananchi wa Tanzania.Anaijua ilipotoka,ilipo na inakokwenda. Jaji Warioba anawajua viongozi wote wakuu wa nchi hii-kuanzia Mwalimu Nyerere hadi Rais Kikwete. Anaujua uimara na udhaifu wa kila mmoja. Kutokana na kuiva kwake kiuongozi,anabaki na mambo yake akilini na moyoni mwake.

Jaji Warioba hana 'bifu' na mtu. Angekuwa hivyo,mara kwa mara angejitokeza kupambana na wanaomsema.Hafanyi hivyo.Kila akiongea,hujielekeza kwenye Rasimu ya Tume yake na kuitetea. Uzalendo wa Jaji Warioba umejidhihiri leo katika Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Alijitokeza kwa heshima,utii na unyenyekevu mbele ya Rais Kikwete kupokea zawadi yake aliyotunukiwa. Hakujificha;hakusita.

Mungu akupe maisha marefu Jaji Warioba na uione nchi hii ikineemeka!
Anastahili Tuzo! Kudos JK... Naamini hata Mzee Ngombale Mwiru alikuwa anastahili tuzo kwa busara na hekima zake...Lukuvi alikuwa anastahili tuzo ya laana katika ardhi hii ya Karume na JKN...RIP waasisi wetu ...
 
Kesho atakuwa live ITV NA RADIO 1 SAA 3USIKU Usikose ndani ya dk45 utaona mambo yake. LIVE LONG JUDGE J.S.WARIOBA and sir God increase his mercy for you. AMEN
 
Ahsante kwa taarifa, hasa ya radio one maana wengine TV ni msamiati!
 
Back
Top Bottom