Nilipata hati bila ya usumbufu wowote kwenye klinik ya ardhi Dar! Mikoani bado ni changamoto

Idofu

Senior Member
Oct 24, 2022
110
187
Kwanza kabla ya yote naomba nikupongeze kwa Kazi kubwa unayopambana nayo!! Keep it Up!!

Pili naomba nikupe uzoefu kidogo niliokutana nao katika zoezi la urasimishaji wa ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam na mkoani!! Katika Ile klinic ya ardhi kwa Dar es Salaam hatimaye nilipata hati bila ya usumbufu wowote!!

Kwa Mkoani, bado nilikumbana na changamoto ya Umungu mtu wa baadhi ya watendaji wa idara ya ardhi kwa kukaa na fomu kwa muda mrefu bila ya kuzipeleka kwa Kamishna wa Ardhi ili hati ipatikane, na wanakuambia kabisa mpaka utoe fedha ili fomu zipelekwe!!

Nyaraka zote ziko sawa, na zimeshasainiwa na wakili, gharama zote zimeshalipiwa, hizo fomu kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi kwenda kwa Kamishna wa Ardhi ni miezi mitatu sasa hazijapelekwa, na hizo ofisi zote ziko ndani ya Km 5 tu!! Mpaka dispatch naye anataka alipwe ndio azipeleke hizo fomu!! Kwa mtindo huo malengo yenu ya kurasimisha ardhi yatafikiwa kweli?
 
Weka Wazi, Mkoa Gani..?

Ikiwezekana taja Hao maafisa watendaji wanaojifanya Miungu Watu ambao wanakutamkia Kbs kwamba hakifanyiki kitu bila chochote.

Tukitaka kuiponya nchi,yabidi kujitoa mhanga.. Taja Watu.
 
Weka Wazi, Mkoa Gani..?

Ikiwezekana taja Hao maafisa watendaji wanaojifanya Miungu Watu ambao wanakutamkia Kbs kwamba hakifanyiki kitu bila chochote.

Tukitaka kuiponya nchi,yabidi kujitoa mhanga.. Taja Watu.
Huu Mkoa ni wa Nyanda za Juu Kusini!!

Kwa wahusika wanaweza kufanya uhakiki kwa waliolipia hati kwenye mfumo wao, na kwa nini hati hawajapewa
 
Back
Top Bottom