Mh. Halima Mdee niambie uhalali wa hii ada..

Endeleaaa

Endeleaaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
1,335
Likes
412
Points
180
Endeleaaa

Endeleaaa

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
1,335 412 180
Leo nimeshangazwa sana kudaiwa ada ya kupaki gari katika fukwe za kokobeach maeneo ya oysterbay. Mkusanya ada huyo ni mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya oysterbay guard. Baada ya kumhoji sana uhalali wa kulipa ada hiyo aliniacha akaondoka na hivyo nikapaki bila kulipa hadi nikaondoka.

Kilichonishangaza watu wote wanaokuja na magari yao kupunga upepo pale beach wakidaiwa hiyo ada wanalipa tu bila hata kuhoji ipasavyo uhalali wa ada hiyo. Ada yenyewe ni shs 1000 kwa saa.

Kulingana na mlinzi huyo hiyo ada ni makusanyo ya serikali ya mtaa oysterbay. nilimuomba namba ya BOSS wake niongee nae kabla sijalipoa hiyo ada lakini aligoma na kuamua kuondoka na kuniacha niendelee na starehe zangu hapo beach.

Mheshimiwa Mdee wewe kama Mbunge wetu eneo hilo tuambie kwanini tunatozwa kodi maeneo ya kujipumzisha kama hayo? Na hiyo kodi ni kulingana na kifungu gani cha sheria? Kwanini halijawekwa bango la serikali linalotoa tamko kuwa kokobichi linalipiwa ada za kuengesha magari? kwanini tudaiwe ada na askari? toka lini askari wakawa wakusanya kodi?

Nijuavyo mimi kokobichi ni eneo la wazi la watanzania kupumzika bure. tungekuwa na hela sana tungeenda commercial beaches mbona ziko nyingi tu.

Tafadhali Mheshimiwa Mdee liangalie hili isije kuwa ni aina nyingine ya ufisadi.

Asante
 
MAMA POROJO

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
4,979
Likes
46
Points
145
MAMA POROJO

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
4,979 46 145Kokobeach ipo jimbo la Kawe au iko jimbo la Kinondoni?
 
M

mohermes

Senior Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
111
Likes
4
Points
35
M

mohermes

Senior Member
Joined Oct 19, 2010
111 4 35
jimbo la kawe bro.
 
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2007
Messages
3,584
Likes
41
Points
0
H

Hofstede

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2007
3,584 41 0
Leo nimeshangazwa sana kudaiwa ada ya kupaki gari katika fukwe za kokobeach maeneo ya oysterbay. Mkusanya ada huyo ni mfanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya oysterbay guard. Baada ya kumhoji sana uhalali wa kulipa ada hiyo aliniacha akaondoka na hivyo nikapaki bila kulipa hadi nikaondoka.

Kilichonishangaza watu wote wanaokuja na magari yao kupunga upepo pale beach wakidaiwa hiyo ada wanalipa tu bila hata kuhoji ipasavyo uhalali wa ada hiyo. Ada yenyewe ni shs 1000 kwa saa.

Kulingana na mlinzi huyo hiyo ada ni makusanyo ya serikali ya mtaa oysterbay. nilimuomba namba ya BOSS wake niongee nae kabla sijalipoa hiyo ada lakini aligoma na kuamua kuondoka na kuniacha niendelee na starehe zangu hapo beach.

Mheshimiwa Mdee wewe kama Mbunge wetu eneo hilo tuambie kwanini tunatozwa kodi maeneo ya kujipumzisha kama hayo? Na hiyo kodi ni kulingana na kifungu gani cha sheria? Kwanini halijawekwa bango la serikali linalotoa tamko kuwa kokobichi linalipiwa ada za kuengesha magari? kwanini tudaiwe ada na askari? toka lini askari wakawa wakusanya kodi?

Nijuavyo mimi kokobichi ni eneo la wazi la watanzania kupumzika bure. tungekuwa na hela sana tungeenda commercial beaches mbona ziko nyingi tu.

Tafadhali Mheshimiwa Mdee liangalie hili isije kuwa ni aina nyingine ya ufisadi.

Asante
Mkuu hakuna haja ya kushangaa, mbona michezo hii ipo mingi tu Dar?, unajua ilianzaje?. Wizi wa vipuri vya magari ndiyo umechochea mtindo huu, ikafikia wakati sasa watu wakawa wakifika sehemu na magari yao kama wanataka kupaki basi wanaangalia nani yupo na kumuomba awaangalizie huku wanamwachia buku(1000) au jero(500). Na kuna baadhi ya sehemu kuna walinzi ila mtu kujihakikishia usalama wa chombo chako bado unampatia mlinzi chochote kitu ili aongeze ukaribu na chombo chako. Sasa tabia hii imeendelea mpaka ikafikia mahali mtu ukipaki sehemu kama kuna mlinzi na usimwachie kitu basi wanakuona wewe mkono wa korosho na wakishika namba ya gari yako basi ujue kuna siku utarudi kwenye gari ukute hakuna spare tyre au sight mirror au kioo kimevunjwa na hata kung'olewa kabisa. Katika maeneo ambao mlinzi ni lazima alinde na kikipotea kitu inakula kwake basi naona watakuwa wamebuni mbinu mbadala ya kuwakwanyua watu vijisenti kama kwa kisingizio ulichopewa wewe.

My take: City council wanaweza kuwa na potential ya kuongeza mapato kama tu watatenga sehemu za parking maalum ambazo unalipia na kupewa risiti kwa muda utakaokuwepo kwa kuajili walinzi na watu kuangalia usalama wa magari yote na kikiibiwa kitu City council inakulipa. Tatizo tulilo nalo bongo hakuna viongozi wenye mitazamo chanya yenye manufaa kwa Taifa zaidi ya yeye binafsi atanufaikaje matokeo yake wanapeana TPS na miradi mingine ya kukusanya hela bila kuwa na liability ya kuyalinda magari hayo.
 
Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2009
Messages
3,013
Likes
30
Points
135
Questt

Questt

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2009
3,013 30 135
My take: City council wanaweza kuwa na potential ya kuongeza mapato kama tu watatenga sehemu za parking maalum ambazo unalipia na kupewa risiti kwa muda utakaokuwepo kwa kuajili walinzi na watu kuangalia usalama wa magari yote na kikiibiwa kitu City council inakulipa. Tatizo tulilo nalo bongo hakuna viongozi wenye mitazamo chanya yenye manufaa kwa Taifa zaidi ya yeye binafsi atanufaikaje matokeo yake wanapeana TPS na miradi mingine ya kukusanya hela bila kuwa na liability ya kuyalinda magari hayo.
Ndg yangu Hii Bongo imejaa wasanii....hao city Council wakiileta hii watu wataanza kujiibia then ndo watakuwa wanaenda kupaki....mtu atachomoa power Window home then atataka kulipwa......hapa n kutengeneza ajira za kutosha atleast mojority wawe busy...........
 
Forum statistics

Threads 1,237,964
Members 475,809
Posts 29,308,135