Mh. Dr. Slaa, Naomba ufafanuzi wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Dr. Slaa, Naomba ufafanuzi wako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amoeba, Nov 29, 2011.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Salam,
  Nafahamu kuwa una majukumu chungu mzima, lakini vilevile nafahamu kuwa JF ni kijiwe chako, hivyo hauishi kuchungulia humu na kuona wadau wana mpya gani, hasa baada ya Ujumbe wa CHADEMA kukutana na kuzungumza na Mh. Kikwete kuhusu mapendekezo ya SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2011. Nimesoma walaka huo uliojaa mapendekezo mwanana yaliyoshiba maslahi tele kwa taifa. Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa masikio ya Watanzania wengi yalikuwa wima kuskiliza Raisi na Jopo lake watajibu nini katika hoja hizo nzito zinazotuhusu moja kwa moja sisi kama Watanzania, mmoja mmoja, na hakika tulitegemea baada ya kikao kilichosheheni watu muhimu kabisa tunaowaamini katika taifa hili kuwa watakuja na maafikiano na majibu yaliyo fafanufu na yaliyoshiba maslahi ya taifa (ikizingatiwa kuwa kodi zetu zilitumika kugharimia kikao hicho), kinachosikitisha na kuchanganya ni kupata "taarifa" yenye ukurasa mmoja tu na vipengele viwili tu vya makubaliano, ambayo haina anwani, utambulisho, wala mhuri wowote, "tangazo" lililosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa upande mmoja, na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mwingine!!! Baada ya maelezo, naomba kuuliza maswali kadhaa ya msingi, ili uweze kututoa kizani kama kuna mambo ya muhim yaliyotupita;
  1. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, ambayo nimeambatanisha hapa ni nyaraka halali?
  2. Hayo makubaliano, kama yanavyosomeka katika TAARIFA KWA VYOMBO vya habari ndiyo mazao ya mjadala uliogharimu masaa mengi na fedha nyingi za walipa kodi, mjadala uliokutanisha vichwa vyenye kuwaza kwa mapana kuhusu ustawi wa Tanzania ya leo na kesho, Ndiyo majibu ya waraka wa CHADEMA wenye kurasa 17?
  3. CHADEMA iko tayari kuweka hadharani nyaraka na makubaliano halali za kikao kati ya Rais na wajumbe wa CHADEMA?
  4. Naamini kuwa CHADEMA kukutana na kujadili suala la katiba na Rais ni moja ya masuala ya msingi kabisa mwanamapinduzi yeyote anaweza kufanya kwa niaba ya wananchi wenzake, Je Ulishiriki mazungumzo hayo? na kama haukkuhudhuria na kushiriki ni kwa nini?
  Mkuu, tunataka kufahamu kwa uwazi na ufasaha, ni nini kilijadiliwa, na ni kwa mapana yapi. Tunataka kufahamu, ni nini kiliafikiwa, na ni kwa undani upi? Ni mambo mengi mno ambayo yamejificha/yamefichwa na wananchi tunataka, na tunahaki ya kufahamishwa bila vificho na kuletewa mikataba ya kilaghai isiyo kichwa wala miguu.

  Natanguliza shukrani zangu, na nakutakia kila la heri katika kujenga TANGANYIKA HURU ILIYOJAA HAKI NA USAWA!
  People's Power,
  Amoeba Mdudu.

  Makubaliano CHADEMA na SERIKALI.jpg
   
 2. B

  Bombambili Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  khah! :A S embarassed:
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tusubiri majibu
   
 4. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,228
  Trophy Points: 280
  It ıs too late!
  The man has sıgned that bıll wıthout Chadema's concern.
  nımeyaamını maneno ya Mkw$r$r$ alıpowahutubıa wazee pale PTA yakwamba sasa anapractıce udıctator na umwamba na ndıcho alıchowafanyıa Chadema leo hıı.
   
 5. B

  Bweru JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kwa mawazo hayo. Ni vema tukajua kila kitu waziwazi. Enzi za kila kitu kuwa siri zimepitwa na wakati.

  Aidha, tunaomba Dr. Slaa, ulivalie njuga suala la posho. Kifo cha ccm kinaanza kufika mwisho. Usilaze damu. Ridhikeni na mishahara mnayolipwa pamoja posho za kujikimu. Hizo posho za kukaa kwenye viti vinavyozunguka na hata kuwafanya msinzie ni wizi wa kodi zetu.
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Tunachotaka ni taarifa rasmi ya chama, ule waraka waliuweka wazi mpaka kwenye vyombo vya habari; iweje makubaliano tuyapate kwa hearsay? Ni kitu gani kimeafikiwa ambacho ni siri "yao"?
   
 7. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nasubiri taarifa.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hawezi kukujibu. Slaa huwa hajibu mambo yanayomhusu yeye na CDM, kazi yake ni kujibu mambo ya viongozi wa CCM tu.
   
 9. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  muswada wenyewe ndo umeshatiwa saini na kuwa sheria sasa, imeshatoka hiyo, mafisadi wanachekelea huko walipo.
   
 10. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ingependeza kama ungemaanisha wewe ndio unataka majibu ya Dr. Slaa sio wote.
  Kwanini usimu ulize profesa aliehudhuria? Hakuna kiongozi yoyote wa siasa ambaye hachungulii JF
   
Loading...