Mh. Bashe watesa familia zetu

Mh. Bashe watesa familia zetu

makamaka

Member
Joined
Dec 1, 2011
Posts
55
Reaction score
28
Mheshimiwa Bashe,

Mbona watesa familia za watanzania wenzako wanyonge? Ulipokuwa kiongozi wetu wa New Habari (2006) Limited ulilazimisha tupewe barua za kupunguzwa kazi bila idhini yetu na kutuahidi kutulipa fedha zetu za retrenchment na malimbikizo ya mishahara yetu kwa wiki mbili. Ilikuwa mwezi wa sita na sasa ni October inaenda November hakuna taarifa yeyote.

Kumbuka watanzania wenzako tena wanyonge tupo mtaani tunahaha kutafuta kazi na hakuna chochote cha kusapoti familia zetu. Tunajua una majukumu makubwa ya taifa hili lakini hili linakuhusu kwa asilimia zote.

Tunakuomba utushughulikie malipo yetu tuachane kwa amani kiongozi wetu. Tunakuomba uvae viatu vyetu na ulitizame suala hilo kwa mtazamo mkubwa ulionao. Nadhani unajua wazi namba moja wetu hapendi watu wake wadhulumiwe.

Tunakusihi sana rekebisha hili ili nafsi yako iwe safi na uendane na uwajibikaji wa serikali ya awamu hii.

Asante.
 
Mimi sijaelewa sijui kwa sababu leo sina hela(stress)
 
Huyu mweshimiwa kaweka pamba masikioni, kulipa hadi ajisikie na ameshaingia Serikalini hakuna cha kumfanya, hapo tuvizie siku akimuudhi Rais atalipa asipomuudhi ndo basi tena
 
IMG_20191107_061545.jpg
 
Back
Top Bottom