Mh. Adam Malima!

abousalimu

Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
62
Reaction score
19
Anasema bei ya nafaka za ndani ikiwa juu serikali huagiza nafaka kutoka nje! Mwenye weledi na mambo ya kiuchumi atudadafulie hili. Mwisho, wale waliomwibia huyu muheshimiwa walikamatwa?
 
alipokuwa anaongea alikuwa na mitepe yake au la?jibu litategemea na jibu lako maana mipet ya majini ina kawaida ya kumminya mtu akili yake..
 
Walimalizana kiaina,si alikuwa demu wake. Ila ishu ya kumiliki ile silaa naona mzee Mwema kamchunia,mambo ya kulindana
 
Anasema bei ya nafaka za ndani ikiwa juu serikali huagiza nafaka kutoka nje! Mwenye weledi na mambo ya kiuchumi atudadafulie hili. Mwisho, wale waliomwibia huyu muheshimiwa walikamatwa?

nimemsikia akitoa sababu kwa nini serikali inafanya intervention ambayo ni kawaida kwa serikali yeyote duniani - huwa sio kila mara market forces zikaachwa zijiendeshe ukichukulia kuwa sio kila mara soko litakuwa la ushindani kikamilifu.

bei kuwa juu ni ishara ya mahitaji kuwa zaidi ya ugavi. na inapokuwa hivyo watu ambao wanaumizwa zaidi ni watu wa mijini ambao wana nguvu (PRESSURE GROUP) HASA ya kisiasa kuliko vijijini ambako wana akiba yao ya chakula. Na katika uzalishaji tayari serikali imesaidia kwa mpango wa ruzuku. Malima ameenda zaidi na kuelezea suala la mfumuko wa bei (inflation) linayosumbua nchi zetu nyingi changa kwani nyumba zinatumia kipato chao kikubwa zaidi kwa chakula kuliko wenzetu wa nchi tajiri.
Kitu kikubwa ni timing - sidhani kwamba serikali itaagiza chakula toka nje wakati hapa nchini kipo cha kutosheleza.
 
Naye ni Waziri huyo! Hivi kigezo cha kuteuliwa waziiri kama Adam Malima, Philipo Mulugo ilikuwa ni nini hasa? Nadhani Angela Kairuki huenda uzuri ulikuwa ni kigezo
 
Tujaribu kuwatendea haki baadhi ya Mawaziri, specifically A.Malima na Kairuki; binafsi nimejaribu kufatilia jinsi Ndugu Malima anavyo jibu maswali mbali mbali bungeni na jinsi anavyp pangilia majibu yake - tukubaliane jamaa huyu ana akili sana na anajua ku-analyse mambo kwa kina, mambo mengine wana JF wanayo msema hayo ni mambo ya ujana tu yatapita, cha muhimu ni weledi wake katika maswala mbali mbali ya kiuchumi nk - hapo Mh. Malima hana mfanowe.

Sasa tuje kwa Mh.Kairuki naye vile vile yuko smart upstairs, kusema kwamba sura yake ndio kilikuwa kigezo cha kuteuliwa katika wadhifa wa uwaziri hapa naona tunavuka mipaka katika utunzi wa tamthilia za kusadikika!! Hii ndio tabia iliyojengeka kwa wanaume wengi ya kujaribu ku-teardown kisaikolojia uwezo wa kina mama kwa visingizio mbali mbali, binafsi tabia hii huwa inanikela sana; kila raia ameshuhudia Kairuki anavyo jibu maswali kwa ufasaha hata yale ya kushtukiza, sasa hapo SURA yake inachangia nini katika uwezo wake kiakili!! Niseme wazi kwamba utehuzi wa Kairuki katika wadhifa wake, aliye tekeleza utehuzi huo akubahatisha - mama huyo ni mkali kiakili haziko mbali na za Prof. A.K Tiba.
 

Hivi ingredient muhimu ya uongozi ni kujua kuongea?
 
Kwanza cheo cha Naibu waziri ni ubadhilifu wa hela za serekali. Ndio mana Kenya wameamua kuwa kama marekani. Sasa hivi wana cabinet secretaries kama 18 tu kwa ajili ya wizara 18 walizo nazo. Hapa kwetu baada ya JK kuwa raisi alichagua mawaziri 60 ili kuwapa ulaji watu wake wote wa mtandao. Na kwa kweli walikula aisee, mpakasasa hivi deni la taifa ni zaidi ya trillion 22. Hata wewe unayemtetea utalipa. Kazi ya naibu waziri hasa siioni zaidi ya kwenda kusoma majibu mbele ya wabunge, ambayo mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika anaweza kusoma. Majibu ya maswali yanaandaaliwa na wataalamu wa wizara husika na anapelekewa waziri kwenda kuwasomea wabunge tu.
 
Naye ni Waziri huyo! Hivi kigezo cha kuteuliwa waziiri kama Adam Malima, Philipo Mulugo ilikuwa ni nini hasa? Nadhani Angela Kairuki huenda uzuri ulikuwa ni kigezo

Kikoreee Nahavache,
Wee utakuwa hujamsikia Mh Pinda juzi kuwa uteuzi wa hawa Mawaziri na Waheshimiwa huwa wanapitia mchujo / mfumo mgumu sanaaaa...hadi kufikia lengo !

Venting huwa ngumu sanaaa...Yaaani hao ndio SUPER A+ .
 
Anasema bei ya nafaka za ndani ikiwa juu serikali huagiza nafaka kutoka nje! Mwenye weledi na mambo ya kiuchumi atudadafulie hili. Mwisho, wale waliomwibia huyu muheshimiwa walikamatwa?
mzee wa kumiliki silaha zaidi ya moja na kutembea nazo! Pinda anasema rais hutumia taarifa nyingi ili mtu kuteuliwa kuwa waziri, je hazikuangaliwa?
 
Kikoreee Nahavache,
Wee utakuwa hujamsikia Mh Pinda juzi kuwa uteuzi wa hawa Mawaziri na Waheshimiwa huwa wanapitia mchujo / mfumo mgumu sanaaaa...hadi kufikia lengo !

Venting huwa ngumu sanaaa...Yaaani hao ndio SUPER A+ .

Mchujo umepitishwa na mtu mmoja, JK na Pinda anaongea kwa sababu huwezi kuwa against bosi wako. Huwa kukosoa mawaziri kwa Pinda ni kujikosoa yeye. Yeye ndiye kiongozi wa serekalini bungeni kwa hiyo kuwatetea mawaziri ni kujitetea yeye. Na anajua wengi hakuna wanachofanya, ila mfumo wa serekali ya Tanzania haumpi mamlaka ya kuwatimua, mwenye hayo mamlaka ni raisi tu. Japo Kenya ndio tu wameanza mfumo wa vetting, nina uhakika mfumo huo utawapa moto sana watawala kuchagua wachapakazi na wawajibikaji. Nakumbuka Kenya majaji wengi tu walioteuliwa walipigwa chini kwenye vetting process kwa sababu huko nyuma walishafanya uzembe. Raisi Uhuru juzi ilibidi afanye umakini wa hali ya juu katika uteuzi wake wa mawaziri 17, in fact ni wawili tu ambao walikuwa na mushkel, Najib Balala na Charty Ngilu ila ilibidi awachukue tu kwa sababu ya kumsaidi kuupata uraisi. Taasisi ya intelligence ilitoa report ya kila aliyeteuliwa, TAKUKURU yao ilitoa report, watu binafsi waliruhusiwa kutoa taarifa za kila mtu kama kuna ushahidi, walichambuliwa vya kutosha ndio wakapitishwa. In fact, wiki iliyopita ndio walianza kwenda ofisini, na wengine mpaka leo hawajaenda ofisini. Wakiileta hii Tanzania, uwajibikaji utaongezeka. Lakini mchakato wa kutunga katiba mpya ulivyobakwa, sioni katiba ikitoka na suluhisho la kulindana kama ilivyo sasa. Wewe kiongozi mkuu wa serekali, amiri jeshi mkuu anatangaza kwenye mkutano wa chama; mliokosa tutawapa nafasi…., which means meritocracy sio jambo la muhimu katika kupena nafasi. Na kweli walipewa nafasi za ukuu wa mikoa, ukuu wa wilaya nk
 
Du mambo ya bastola

  1. Kompyuta (laptop) tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh. 5.6 milioni.
  2. Vinasa sauti (tape recorder) viwili vya digitali vyenye thamani ya Sh. milioni moja.
  3. Simu tatu za mkononi (Nokia C6 ya thamani ya Sh. 500,000, Nokia E200 ya Sh. 250,000 na Blackberry yenye thamani ya Sh. 5.5 milioni).
  4. Pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh. 2.5 milioni.
  5. Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na Sh. 6.5milioni.
  6. Fedha taslimu za Tanzania Sh. 1.5 milioni.
  7. Kadi mbili za benki (ATM).
  8. Mabegi matatu yaliyojaa nguo.
  9. Baraghashia mbili zenye thamani ya Sh. 50,000.
  10. Nyaraka “mbalimbali” za serikali na za binafsi.
  11. Pasipoti mbili za kusafiria.
Miongoni mwa vitu ambavyo havikuibiwa ni pamoja na bastola na bunduki aina ya shotgun.
Kwa maoni yangu, kubeba vitu vyote hivi, ni ulimbukeni kama wa hadithi ya zuzu aliyeshinda bahati nasibu akaamua kununua kila kitu mtaani kwake, hadi kituo cha basi.
Katika hali ya kawaida, mwanasiasa anasafiri na laptop tatu za nini? Vinasa sauti: Je, yeye amekuwa mwandishi wa habari au mpelelezi anayetafuta ushahidi wa sauti? Nini hasa?
Simu tatu: Bahati mbaya huu ni utamaduni nchini Tanzania, lakini pia sijawahi kusikia Blackberry ya gharama zote hizi karibu zaidi ya dola 3,400 za Marekani. Hiki ni kiroja…Ina nini hiyo simu?
Pete mbili: Hizo sawa lakini bado alipoongea na waandishi alikuwa amevaa mapete mengine. Sasa yote ya nini?
Dola za Marekani zote hizo kwa safari ya vijijini ni za nini? Au alizipata hukohuko?
Kiasi cha fedha za Tanzania, nadhani hicho ni sawa, maanake alihitaji kulipia gharama kadhaa. Pia, kadi mbili za benki ni sawa na hata mabegi matatu ya nguo si ajabu kama alikuwa na safari ndefu. Hata baraghashia mbili si tatizo.
Nyaraka za serikali: Hii ni fedheha kubwa, kwa kuwa kama naibu waziri alipaswa kujua jinsi ya kutunza nyaraka za serikali mara aingiapo hotelini au popote pale. Huwezi kuziweka nyaraka nyeti hovyohovyo tu.
Pasipoti mbili zote za nini? Alihitaji kwenda nazo Morogoro…? Silaha: Magazeti yameandika kuwa ni bastola na shotgun. Kwa kubeba silaha zote hizi anaogopa nini au analinda nini…?
Mavitu, makompyuta, mahela, masilaha, mavinasa sauti, mapete, madude mengi tu. Swali: Je, kuna utu-uzima hapo? Hii ni sifa nzuri ya kiongozi kweli…?
Pana tatizo hapa.



 
Mkuu NAVAHACHE, kila Mtanzania anajua kwamba majibu ya Bungeni yanatayaliswa mapema zaidi, kama wewe hicho ndicho unakiona ni kigezo cha kuwaponda baadhi ya Mawaziri na manaibu, basi nafikili kuna tatizo fulani katika kuwasoma watu/Viongozi! Hivi kwa nini ujiulizi inakuwaje baadhi ya mawaziri licha ya kupewa majibu on a silver plate lakini kuna baadhi yao hawana uwezo wa kuyachambua kwa kina na wakshtukizwa maswali wanaonekana kubabahika - hiyo inakupa picha GANI?

Kuna msemo usemao ni afadhali ukae kimya ili kuficha mapungufu yako kiakili (ie watu wasijue kama una akili au huna) kuliko kujitia kusema/kujibu alafu ndio unadhihilika kwamba kumbe kweli akili huna, in other words kujua kuongea na ku-analyse mambo ni componet/ingredient muhimu sana katika recipe au mixed grill ya UONGOZI don't U forget that! Reading between the lines za posts zako kuhusu uzi huu nashindwa kuelewa tatizo lako ni nini hasa? Je na kuhusu Malima na Kairuki au ukubwa kwa Cabinet ya JK, by Cabinet namaanisha Mawaziri na sio cabinet ya kufungia mafaili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…