GE2025 Mgore aongoza kura za maoni Musoma Mjini

GE2025 Mgore aongoza kura za maoni Musoma Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
365
Reaction score
459
Mgore Miraji ameibuka mshindi kwenye kura za maoni baada ya kuwabwaga wapinzani wake watano aliokuwa akishindana nao katika mchakato wa kumpata mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu ujao katika Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara.

Endapo Mgore atapitishwa na kamati Kuu ya chama chake kupeperusha bendera na kisha kuwa mshindi katika uchaguzi huo, basi atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa mbunge wa jimbo hilo la Musoma Mjini.

Akitangaza matokeo ya kura za maoni kwa Wilaya ya Musoma Mjini, Katibu wa CCM wilayani humo, Burhan Ruta amesema Mgore amepata kura 2,255 huku mpinzani wake wa karibu Juma Mokili akipata kura 1,543.

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano ni pamoja na Dk Eliud Esseko (115), John Bwana (43), Philbert Sasita (34) na Mashaka Biswalo (44).

“Jumla ya kura zilizopigwa ni 3,796, zilizoharibika ni 62 na halali zilikuwa 3,734, kwa hiyo namtangaza Mgore kuwa ameongeza kwenye kura za maoni,” amesema.

Ruta amesema kutokana na kanuni za chama hicho, mgombea aliyeongoza katika kura za maoni hapaswi kufanya sherehe ya aina yoyote kabla ya vikao vya uteuzi kwa maelezo kuwa kuongoza sio kigezo cha kuteuliwa na chama.

1754331289409.png
 
Duh! Huyo Mkorea asingehama upinzani angechukua Jimbo, Sasa kakimbilia CCM wamemla kichwa.
 
Nani huyo?

Dr Elliud Esseko Tongora. Jamaa alikuwa na Upepo Sana pale Musoma mjini, sema karudi CCM Tena. Alikuwa CHADEMA akaenda ACT naona karudi CCM ila kapigwa Chini vibaya mno. Bila CHADEMA Hilo Jimbo ni la CCM kwa asilimia 100
 
Hiyo pisi inaenda kuwa chakula ya akina Ndungai tu huko bungeni.
 
Back
Top Bottom