Mgongo kuuma wakati wa "HEDHI" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgongo kuuma wakati wa "HEDHI"

Discussion in 'JF Doctor' started by Mlawi, Nov 1, 2011.

 1. M

  Mlawi Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu, heshima zenu.

  Nina tatizo la kuuma mgongo kabla na baada ya kupata HEDHI. nina mwaka wa 2 na hili tatizo na sijawahi kwenda hospitali kwa kujua kwamba ni kawaida. Sasa naona ninakoelekea ni kubaya zaidi.

  Nina mtoto wa miaka 13.
  Mlawi.
   
 2. Kelema

  Kelema Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana dada. Kuna sababu mbalimbali za kuumwa mgongo kabla na baadaya hedhi. Ukiongea na Daktari bingwa wa matatizo ya wanawake, anaweza kukusaidia. Ila kama unataka kujaribu msaada wa kwanza "first aid', nunua unga wa majani ya mlonge, unakunywa kijiko cha chai kutwa mara tatu. Unachemsha uji kidogo, ukiiva, unauweka kwenye kikombe, ndipo unaweka mlonge na sukari, uji ukiwa wa motoooo, una mix vizuri unakunywa uji. Kama hupendi uji, unaweza ku mix na maji moto au chai ya moto, unywe ikiwa bado moto.

  Vilevile angalia godoro unalolalia. Lisiwe linatumbukia au laini sana. Inafaa liwe gumu kiasi, na liwe kama la nchi 4 au 5 hivi.

  Vile vile, nunua hotwater bottle, ni ya plastic, unachemsha maji ya moto, unajaza, unaizungushia kwenye taulo nyepesi, unaweka sehemu inayouma.

  VILEVILE, jaribu kuwa na mazoea ya kunywa kitunguu saumu vipande vitau au vinne kutegemeana na ukubwa. Kama hupendi harufu yake, unamenya, unakatakata vidogo vidogo, unakunywa na maji asubuhi na jioni. Ni dawa nzuri sana!!

  Zoezi hilo lifanye kwa miezi mitatu mfululizo. Nina hakika utapata nafuu kama sio kupona kabisa. Ila usisahau kupimwa na Daktari, kwa sbb siku hizi kuna vifaa vya hali ya juu sana, kuweza kugundua matatizo.

  Natumaini utatupa majibu hapa jamvini.
   
 3. mshihiri

  mshihiri Senior Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tafuta magome ya mkunazi unachemsha pamoja na maji lita moja ukimaliza unakunywa nusu kikombe cha chai mara mbili kwa siku muda wa siku 21 mfululizo
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Mhh! kaaazi kwelikweli. Udaktari kweli kazi.
  Mkuu 3 months mbona parefu? Huyu dada huenda ikawa anapata maumivu kwa muda usiozidi siku 5, sasa hii 'First Aid' ya miezi mitatu si bora ingekuwa tiba kabisa.

  Lakini pia ushauri wako inaonekana upo zaidi upande wa tiba mbadala, sasa hao madaktari bingwa unaosema ni wapi?

  OK fine, nisiingilie sana taaluma za watu, ila nadhani huyu dada/mama anasumbuliwa na tatizo linaloitwa(Dysmenorrhoea). Ingawa hajasema kama ameishazaa(mara ngapi), ila hili ni tatizo la kawaida kwa akina dada hasa ambao hawajazaa na mara nyingi hupungua hadi kuisha kabisa kwa kadiri anavyozidi kuzaa. Mara nyingi linakuwa halina sababu nyingine zaidi ya contraction ya uterus kwa ajili ya kutoa nje ile damu. Na baada ya kuisha ile damu taratibu contractions zinaanza kupungua hadi kuisha kabisa.

  Kuna dawa za kupunguza maumivu kama vile diclofenac, tramador, hyoscine nk. huwasaidia wengi(ingawa pia wapo wachache ambao haziwasaidii).

  Lakini ili kuwa na uhakika ni vema ukaonana na daktari ufanyiwe vipimo ili kuwa na uhakika wa nini hasa tatizo lako.
   
Loading...