Prince Naahjum_
Senior Member
- Jun 13, 2016
- 139
- 125
Alikuwa mwanamke mzuri, yes mzuri haswa hakustahili kuwa gerezani tena akitumikia kifungo cha miaka 15 jela na huku akiwa ameshatumikia miaka 11.
Akiwa na huzuni na msongo wa mawazo akapitisha adhma moyoni mwake ya kuwa mwaka huu usipite lazima atoroke gerezani kwa namna yoyote ile. Ni heri afe kuliko kuendelea kutumikia kifungo kwa miaka mingine tena.
Huko jela huyu mwanamke alijenga urafiki na mfungwa aliyehusika na uzikaji wa wafungwa wanaofariki gerezani, huyu hujulikana kwa jina la "care taker" au mgonga nyundo kazi yake kubwa ni kuzika wafungwa nje ya gereza.
Pale mfungwa anapofariki care taker alitakiwa kugonga kengere ya kifo ambayo ilisikika na wafungwa wote. Care taker angechukua maiti ya mfungwa na kuiweka katika jeneza "casket" angegongelea msumari mfuniko wa jeneza na kwenda ofisini kwake kuandika cheti cha kifo "death certificate".
Baada ya hapo huweka casket katika gari ya kubebea "wagonjwa" na kupeleka makaburini kuzika.
Kwa kuifaham hiyo ratiba pale panapotokea kifo gerezani, Mwanamke aliandaa mpango wa kutoroka gerezani, angesubiri siku kengere ya kifo igongwe, angetoka katika chumba chake cha gereza na kuelekea chumba cha wafu.
Angeingia katika jeneza lenye maiti na care taker angekuja kugonga nyundo. Na kulichukua jeneza katika gari la wagonjwa kwenda kuzika. Baada ya muda kidogo care taker angerudi makaburini kufukua na yeye angetoka akiwa huru.
Care taker alishirikishwa huo mpango, lakini alisita sana, lakini baada ya mwanamke kusisitiza sana na kwa sababu ya urafiki wao care taker au mgonga nyundo alikubali. Kilichobaki ilikuwa ni kusubiri tu mfungwa afe.
Baada ya wiki sita za kusubiri kifo cha mfungwa, usiku akiwa amelala alisikia kengere ya kifo ikipigwa, taratibu aliinuka kitandani huku akijua saa ya ukombozi imefika.
Alitoka nje ya chumba chake taratibu kuelekea chumba cha wafu, huku akinyata taratibu mara kadhaa alikaribia kushtukiwa na walinzi lakin aliwahi kujificha mpaka alipofikia chumba wanakohifadhi majeneza.
Kwa msaada wa tochi ndogo aliyokua nayo aliliona jeneza lililo wazi likiwa na maiti ndani na akajua ndimo alimotakiwa kuingia.
Alipanda taratibu na kujihifadhi vizuri na ile maiti iliyokuwemo ndani, akanyosha miguu na akarudisha mfuniko na kujifunika. Akisubiri mgonga nyundo aje agonge msumari na kwenda kulishusha katika kaburi.
Baada ya muda mfupi alisikia hatua za mtu zikija upande lilijo jeneza, akasikia nyundo ikigongwa kulifunga vizuri jeneza.
Pamoja na kuwa na hofu kuu lakini alijipa moyo kuwa kila hatua ni muhimu kwake kukaribia uhuru wake mwingine. Jeneza lilibebwa katika gari la wagonjwa na safari ya kuelekea mkaburini ikaanza.
Baada ya kufika yule mwanamke, alihisi jeneza likishushwa chini taratibu na baada ya muda mfupi alihisi kuwa ni mchanga ulikuwa ukitupwa juu ya jeneza. Akajipa matumaini kuwa ni jambo la muda mfupi tu kuelekea uhuru wake. Alitabasamu! Na kujisemea hatimae naenda kuwa huru tena, kwa maana uhuru wangu mekaribia!
Akaamua kuwasha tochi kujua ni mfungwa yupi aliyefariki. MUNGU wangu, kuangalia vizuri kumbe maiti aliyokuwa nayo mule ndani ni ya yule mfufuaji wake care taker ndiye alikuwa amefariki. Mwanamke alijizika akiwa hai kwa namna hiyo. Alilia sana kwa uchungu na kujutiaa maamuzi yake, na kusema bora ningebaki tu gerezani...! Hatimaye aliaga dunia kwa njia hiyoo....!
TUNAJIFUNZA NINI....!?
Wanadamu tulio wengi miongoni mwetu huwa tuna matarajio makubwa sana katika maisha yetu, kiasi ya kwamba tupo tayari kutafuta njia yoyote ile ya mkato ilimradi tu tuyafikie hayo malengo.
Nakusihi rafiki yangu....! NOTHING COMES AT EASY!! Na kama vitakuja kirahisi kwa njia ya mkato madhara yake hayatakuacha nyuma kamwe, na utayajutia sana maishani mwako.
Kama unataka kufanikiwa fanya kazi kwa bidii huku ukimuomba MUNGU wetu muweza, na kwa hakika yeye atakuonesha njia sahihi ya kuyafikia mafanikio yako.
BY:
PRINCE NAAHJUM ALSINA