Mgomo wa wauza mafuta umeanza tena

Mgomo wa wauza mafuta umeanza tena

Viongozi wetu na wanasiasa ndio wafanyabiashara wakubwa wa mafuta.

Mmiliki wa ENGEN aliipa s/kali ya JK masaa 24 kwenye mgomo wa kwanza.
 
Public Private Partnership, so called 10%, njaa nyingi na tumbo zisizokua na shukrani....
Taifa langu litaangamia kwa kukosa maarifa.
Ulikwisha ibariki Tanzania, ikomboe sasa MUNGU....
 
Sera mbovu ya biashara ndiyo chanzo cha yote haya! Wafanyabiashara wa ndani tunaumizwa sana na maamuzi yanayotolewa kisiasa! Jaribu kuangalia zile mashine za TRA zinatuumiza sana tunaofanya biashara kwa kukopesha! Imagine una client unayemsupply mafuta let's say na anakulipa labda baada ya muda fulani. Wewe unampatia receipt ya TRA na mwisho wa mwezi unapeleka pesa ya TRA wakati wewe hujalipwa pesa yako, na unaweza kutokulipwa kabisa! Ni uonevu wa hali ya juu kwa wafanyabiashara wa ndani. Zile mashine zinatuumiza sana wajasiriamali.
 
Public Private Partnership, so called 10%, njaa nyingi na tumbo zisizokua na shukrani....
Taifa langu litaangamia kwa kukosa maarifa.
Ulikwisha ibariki Tanzania, ikomboe sasa MUNGU....

Kuna watu ni wasomi wazuri ila sijui wana laana gani, wapo serikalini na hawataki kutumia usomi wao kutatua matatizo yanayotukabili. Mijitu ina laana kubwa sana yani. Huwa nakereka sana inapofikia hatua ya mfanyabiashara kugoma kutoa huduma wakati anahitaji faida, yani mamlaka husika wanaona ni jambo la kawaida kabisa! Huu ni uozo wa ajabu sana saa nyingine nikimuona mshkaji anafanya serikalini huwa namshangaa kuona akiwa mtaani anaonekana mtu wa maana ila akiwa ofisini anakuwa hewa kabisa! Poor planning! Watu hawawajibiki kabisa, niliwahi kwenda ofisi moja ya serikali na nilikuwa nataka kuonana na bosi fulani anipe muongozo wa vibali ila nilikaa masaa matatu kisa kuna jamaa yake alienda kumsalimia. Yani nawasikia maongezi yao ndani na ni saa nne asubuhi, jamaa haoni kama ni muda wa yeye kuwajibika! Sasa unadhani mtu kama huyo atawaza saa ngapi kufuatilia kero za wateja wake! Laana tunayo! Kuchwa kucha kuwasifia wakenya wakati tunaweza kubadilika!
 
Viongozi wetu na wanasiasa ndio wafanyabiashara wakubwa wa mafuta.

Mmiliki wa ENGEN aliipa s/kali ya JK masaa 24 kwenye mgomo wa kwanza.

Miafrika especially mitanzania ndivyo tulivyo! Jitu linataka kuwa tajiri kwa kuiba mali ya umma. Yani Tanzania hakuna anayewaza kuwa tajiri bila ya kuwa mwanasiasa! Nchi hii tumeiharibu sana! Hata Mungu naamini anatuchukia kwa kukosa maarifa ya kuzitumia rasilimali zetu kimikakati endelevu!
 
Hata mm nisingeuza hayo mafuta,kwani mtu mwenye stock yake ya lita 100,000 ameinunua mwezi uliopita kwa bei flani leo aiuze tu kwa bei yoyote kisa Serikali na bei elekezi. Hivi serikali hii inajua ni mafuta kiasi gani yameingia nchini, na kwa siku yanatumika kiasi gani, ili mwisho wa mwezi wawe na rejeo la kushuka au kupanda kwa bei?
We acha hizo, unasema hivyo kwa vile ni mwanahisa kwenye hayo makampuni ya mafuta kama ID yako? Mbona bei zikipanda stock inakuwepo na wanauza na bei zikishuka hakuna stock, fikiri kabla ya kuropoka, hao jamaa zako ni wezi, wanyonyaji na majambazi na wape taarifa kuwa wananchi wamechoka na ubeberu wao, wananchi nao wana haki zao na uvumilivu una kikomo chake utafika wakati nao watajichukulia sheria ya kuchoma vituo vyenye mtindo huo wa kifisadi
 
Back
Top Bottom