Mgomo wa Wasafirishaji Mji wa Moshi: Siasa za CHADEMA vs CCM

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,917
1,660
Wana bodi asalaam aleykum
Tangu juzi Ijumaa Mji wa Msohi umekumbwa na kadhia ya Wasafirishaji kugoma kusafirisha abiria kati ya mji wa moshi na Arusha pamoja na sehemu zingine za mkoa wa Kilimanjaro.
Hali ni mbaya sana kwani abiria wanalazimika kupanda magari binafsi aina ya Noah. Na magari hayo kupambwa kwa maua kama vile wanaenda Msibani. kwani kuna vijana wamepangwa Njia ya panda Himo,Barabara ya Kibosho kwa ajili ya kupopoa mawe mabasi ambayo yanakaidi mgomo.
Pia nimejaribu kuongea na baadhi ya makundi ya vijana wapopoaji kuhusu theme ya mgomo wao. Cha kwanza kabisa waliniuliza itikadi yangu nikaawaambia mimi ni mwana CDM. Duh. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunijalia Mbio.
Nilichokugundua kuwa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Moshi na Mkoa wanachochea mgogoro huu ili kuchonganisha wananchi wa Moshi na Halmashuri ya Mji wa Moshi ambayo inaongozwa na Chadema. Kuna magari ambayo yanapeperusha bendera za CCM yanabeba abiria bila kikwazo chochote. aliyepo moshi aende barabara inayoenda TPC/Kahe atayaona vizuri tu.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kilimanjaro Godliving Moshi. ambaye kimsingi ni mpiga debe wa magari ya Marangu/Holili chini ya mwavuli wa Akiboa ndiye aliyepanga vijana maeneo yote hayo yenye vurugu. Pia warusha mawe hao ni wale vijana wa CCM waliopiga wagonjwa Hospital ya KCMC mwaka 2010
NAOMBA KUWASILISHA
 
Hili tatizo la magari kugoma kutoa huduma za usafiri zimekua kero kwa mji wa moshi na arusha takriban wikiki sasa.ilianza daladala za moshi na sasa coaster ziendazo moshi,asubuhi ya leo imenilazimu kulipa alfu ishirini kufika moshi.hakuna gari ya kwenda dar iliyoruhusiwa kuchukua abiria wa moshi kwahiyo kama safari yako ilikua ni yalazima basi ilikubidi ulipe nauli ya kwenda dar.sababu za mgomo ni kodi zisizo na tija zinazotozwa pindi wapitapo kila kitu.ukitoka arusha kwenda moshi kuna kodi mara nne yaani kwenye vituo vinne lazima ulipe 2500.kituo cha kwanza ni stand ya mabasi arusha,tengeru,bomangombe na kituo cha mabasi moshi.sasa wewe piga hesabu vituo vyote hivyo kutoza kodi ina tija gani kimaendeleo au ni roadtall inarudishwa kwa staili ingine?mgomo mwingine unaonukia ni wa magari ya dar arusha nao wanasema wapo njiani kuunga mkono wenzao kwani wao ndio wanalipishwa hela nyingi mpaka inakera.hii serekali inaelekea bila mgomo haiendi.migomo iliyopo ni ya madaktari na sasa inayofuatia ni walimu nahapo ndipo nchi itakapo kua haitawaliki rasmi.
 
lazima CCM ICHINJWE 2015 HATA WAKILETA VURUGU,MAMEMCHINJA MWENYEKITI ARUMERU SASA WANALETA BIFU ZA KIJINGA SI WAHAME HICHO CHAMA KWANI LAZIMA KUWA CCM? CHAMA CHA MAFISADI HICHO JAMANI HAMUONI KAMA MMELAANIWA?
 
Chanzo cha mgomo wa wasafirishaji ni CCM, ushahidi huu hapa:-
 
Acha kupotosha umma. Wasafirishaji walio wengi K'njaro ni CDM, ule ni mgomo wa wasafirishaji usio na uhusiano na chama cha kisiasa.
 
So kila kitu siasa. Hata udaku utakuwa siasa nao yaani Wema amchamba Wolper siasa, Diamond ni freemason sias. Du kali.
 
Kwanza nishukuru sana kwa thread hii
Binafsi leo nimestushwa sana na mgomo huu wa leo. Juzi tarehe 9/7 tulikumbwa na mgomo kama huu! Siku ya pili mgomo ukapungua na watu kuendelea na shughuli zao. Leo mambo yamerudia tena vibaya zaidi.
Kibaya sana MEYA WA MANISPAA anasimama na kusema kuwa halmashauri imekwisha hamua yule asiyetaka aweke gari lake nyumbani! Ndugu yangu Jaffar Michael Meya wa manispaa ya Moshi unatakiwa uchunge sana mdomo wako! Hii siyo kauli kwa wapiga kura wako! Ukipita kila sehemu hata asiyejua chochote utasikia akisema haya ndo maafa ya kuchagua CHADEMA! Tumeshuhudia mashirika mbalimbali wakiwaita wadau wao na kuwaelezea kusudio lao la kupandisha gharama mbalimbali. This is a soft approach for your people! Tulitegemea Halmashauri ya Moshi ingekaa na wadau kupitia kipengele kwa kipengele kuwashawishi ni kwa nini tozo lipande. CCM wamemchezesha mziki wanaoupenda wao nao wameingia kucheza bila kujijua. Poleni sana CDM!
Mwenyekiti wa CDM Taifa na Mzee Ndesamburo kaeni na kijana wenu mumwelimishe! Amechemka sana, mwambieni aache jazba na hasira. Mkimwacha atawacost 2015. Believe me 2015 mna kazi kubwa kuliko mnavyofikiri!
Jimbo la Moshi ni muhimu sana! Naskia wanaCCM wanamwaga mboga huku! Sio ajabu nanyi mkaja na sera za kumwaga ugali! Madiwani wa Moshi wengi ni CDM, jueni kuwa mgomo huu anayenyooshewa kidole ni CHADEMA!
Je Mtaweza kujinasua?
 
Kibanga Ampiga MKoloni

Barua hii labda mtu ambae ametoka mirembe ndie atakubaliana nayo kua CCM wame andika! Barua imetengenezwa na Chadema kwa propaganda za kichadema
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama halmashauri tu wanashndwa kuiongoza,wataweza kuongoza nchi kweli?i pity you chadema.
 
Mkuu wacha kuleta mambo ya siasa watu wanagoma ushuru umepanda kutoka 1000 mpaka 1500 haijapita muda wameongeza tena 2000 watu wamechoka wameamua wagome sasa wewe na siasa zako zinaingiaje hapa au umetumwa?
 
Sasa kama halmashauri tu wanashndwa kuiongoza,wataweza kuongoza nchi kweli?i pity you chadema.

Hicho ndo kitu mnachotaka kuwajengea wananchi wapate kuamini ila mkumbuke mTz wa leo siyo yule wa 2005 au wa 2010, mabadiliko ni lazima na siyo ombi!
 
Back
Top Bottom