Mgomo wa wahisani: Serikali ya JK yajifariji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa wahisani: Serikali ya JK yajifariji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, May 22, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  WAKATI wahisani wakishikilia msimamo wao wa kukataa kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 220 ilichopunguza katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha unaoanza Julai, serikali imeanza kutoa kauli za kujifariji kuwa haibabaishwi na uamuzi huo.

  Uamuzi huo wa serikali unaolenga kuwaaminisha wananchi kuwa kiasi hicho cha fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi bilioni 297 si chochote si lolote, ulitangazwa mbele ya waandishi wa habari jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

  Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri Mkulo alikiri kupunguzwa kwa kiasi hicho cha msaada kutoka kwa wafadhili wa bajeti kuu.

  "Ni kweli wahisani wamepunguza msaada kutoka dola za Marekani milioni 754 hadi dola milioni 534 na nitawaeleza kwanini, lakini pamoja na hayo hakuna kitakachoharibika hapa.

  "Kama serikali tulilijua hili tangu Novemba mwaka jana tulipokutana na wafadhili wa bajeti yetu, tukazungumza na kuna mambo walitaka tuyafanye, lakini sisi tumechelewa kuyatekeleza… tukajipanga kuziba pengo hili kwa kupata mkopo wa sh milioni 250 kwa gharama nafuu kutoka benki ya Stanbic," alisema Mkulo.

  Aidha, alivitaja baadhi ya vikwazo vilivyolalamikiwa na wahisani hao kuwa ni urasimu katika uwekezaji, utaratibu wa kutambua na kuzihamasisha sekta binafsi na muongozo mbovu wa kifedha serikalini.

  Kuhusu urasimu, Mkulo alikiri kuwepo na hali hiyo ambapo mwekezaji humaliza zaidi ya mwezi mmoja kufuata taratibu za kukubaliwa kuwekeza nchini, jambo linalolalamikiwa na wafadhili.

  Suala jingine ambalo Tanzania imechelewesha utekelezaji wake ni kutokuwa na utaratibu wa serikali kushirikiana na sekta binafsi jambo lililoelezwa na waziri huyo kwamba tayari muswada wa sheria ya kutambua sekta binafsi (PPP), utafikishwa bungeni, kujadiliwa na kupitishwa.

  "Ni kweli tumekuwa goigoi katika kutekeleza yale tuliyokubaliana na wahisani wetu… unajua kila kitu kina masharti yake, na kuhusu kuzitambua sekta binafsi, katika Bunge lijalo la bajeti tutapitisha sheria ya Public Private Partnership," alisisitiza.

  Hata hivyo, aliwaeleza wananchi kwamba Tanzania imejiwekea akiba ya dola za Marekani bilioni 3.5 na kwamba ina uwezo wa kujiendesha kama nchi kwa miezi mitano bila matatizo.

  Alisema uwepo wa fedha hizo unaashiria uimara wa uchumi wa nchi na kufafanua kwamba hivi sasa Tanzania inaondoka kwenye orodha ya nchi maskini sana ulimwenguni.

  "Kwa hali tunayokwenda nayo, tumeanza kuaminika huko duniani… yaani tunaweza kukopesheka, na hii ni dalili kwamba tunaingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa wastani sio maskini sana…

  "Ndani ya miaka minne ijayo naamini hii itakuwa Tanzania ya tofauti sana," alisisitiza Mkulo na kuwataka Watanzania wasubiri hadi Juni 10 itakaposomwa bajeti ya mwaka 2010/11 aliyoielezea kuwa na matumaini, huku akishindwa kueleza kuhusu kupanda sana kwa viwango vya kodi kwenye bidhaa mbalimbali.

  Wahisani waliotangaza kusitisha msaada huo wa bajeti wiki iliyopita ni Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Canada, Denmark na Jumuiya ya Ulaya (EU).

  Wengine katika kundi hilo ni, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia (WB).

  Katika bajeti inayofikia mwisho mwezi ujao, wahisani hao walichangia sh trilioni 1.9 kupitia katika miradi ya maendeleo na mifuko ya kisekta.

  Katika bajeti hiyo ya mwaka jana, kiasi kingine cha shilingi milioni 968,028 zilitokana na mikopo ya ndani na sehemu ya mchango wa wahisani hao kupitia misaada ya kibajeti.

  Tamko hilo la wahisani kusitisha misaada hiyo lilitolewa na Peter Dorst wa ADB ambayo ndiyo mwenyekiti wa wahisani hao na katika taarifa yake, walieleza kuwa, uamuzi wa kupunguza fedha za kusaidia bajeti ya serikali, umetokana na mambo mengi, ikiwemo serikali kushindwa kufikia malengo kadhaa ya maendeleo.

  Uamuzi huo wa sasa unakuja ikiwa ni miaka miwili tangu wafanye hivyo mwaka juzi walipogoma kutoa fedha baada ya serikali kusuasua kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi, wakiwemo wale wa fedha za EPA.

  Source: Tanzania Daima

  Mtazamo: Serikali ikiwa inaendesha kwa mikopo ni hatari na inaweza kupelekea kuanguka kwa dola husika mfano wake ni Greece, UK na nchi nyenginezo. Ufadhili wa wazungu unafaida yake kwani unaweza ukaja baadae mkasamehewa mikopo mliyokopa. Au mkawa na makubaliano ya muda mrefu lakini kukopa kwa financial institution ni kuliingiza taifa katika janga la mzigo mkubwa wa madeni. Ukichukulia nchi yetu haina mfumo mzuri wa ukusanyaji kodi, mfumo mzuri wa ufatiliaji wa uwekezaji inabidi kama this is the only solution waweke mazingira mazuri ya ufatiliaji wa kodi nchini otherwise mzigo utaangukia kwa wafanyakazi kuishia kulipa kodi kubwa ili serikali ingeze pato lake.

  Ni njia nzuri kama wakiwa wamekosa njia ya kukopa but still wangelifikiria bado kwenda kukopa IMF, WB au EADB, AB ambapo terms can be favorable compare kwenda kwa banks ambao wako katika kumaximize profit tu. ni ushauri lakini!!!!
   
Loading...