Mgomo wa wafanyabiashara sumbawanga mjini

Julido

Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
83
Reaction score
21
Wakuu nimepita viunga vya mji wa sumbawanga mida hii mgomo unaendele na wafanyabiashara wote wamefunga sehem zao za biashara.

Kuanzia muuza vocha, mwenyewe kibanda cha mpesa/tigo pesa/groceries /mama ntilie hadi maduka makubwa hakuna huduma.

Kuna kundi linapita kila mtaa na kuwaamuru wale waliofungua sehem zao zao za biashara zifungwe ili kuunga mkono mgomo!!

Nadhan ipo haja kwa TRA kutoa elimu zaid kwa wafanyabiashara! !
 
Attachments

  • 1392206997025.jpg
    1392206997025.jpg
    42.1 KB · Views: 176
  • 1392207034612.jpg
    1392207034612.jpg
    41 KB · Views: 147
  • 1392207056548.jpg
    1392207056548.jpg
    64.2 KB · Views: 140
  • 1392207089718.jpg
    1392207089718.jpg
    61.3 KB · Views: 136
  • 1392207137188.jpg
    1392207137188.jpg
    77.4 KB · Views: 132
  • 1392207166956.jpg
    1392207166956.jpg
    53 KB · Views: 137
Tanga watu wametandikwa kwa kufungua maduka ila hali imerejea baada ya kuyafunga...hii ishu serikali inachukulia rahisi kwa sababu inadharau sana wananchi wake pamoja na kwamba inawakamua kila kona kuanzia kodi hadi huduma mbovu...ipo siku tu
 
Duh naona hapo 2 way inayotoka round about kwenda stendi ...majanga.
 
Wakuu nimepita viunga vya mji wa sumbawanga mida hii mgomo unaendele na wafanyabiashara wote wamefunga sehem zao za biashara.

Kuanzia muuza vocha, mwenyewe kibanda cha mpesa/tigo pesa/groceries /mama ntilie hadi maduka makubwa hakuna huduma.

Kuna kundi linapita kila mtaa na kuwaamuru wale waliofungua sehem zao zao za biashara zifungwe ili kuunga mkono mgomo!!

Nadhan ipo haja kwa TRA kutoa elimu zaid kwa wafanyabiashara! !

ndio maana nawapenda sana wachina,huwezi kudhubutu kufanya hiki kinachofanywa na wafabiashara hapa Tanzania sasa.
hata Idd amini dada kule uganda kunakipindi watu wake walikuwa wakimpenda sana.
Kama kuna mapungufu yafanyiwe kazi,lakini hii haiwezi kuwafanya wafanyabiashara kukataa kuisaidia serikali kukusanya kodi
Serikali isipo jenga barabara nzuri tunalalamika,inapotaka kukusanya kodi ili iweze kuboresha miundo msingi ya nchii hii tunagoma,nini tunataka? nchi za wenzetu zinaendelea tunawaonea wivu,sisi hatutaki kuliwa ili nchi isonge mbele,
tusione vinaelea huko majuu,watu wametaabika jamani kufikia malengo.
Lakini pia serikali iwe makini krk hili,maana isije ikawa kama zile speed governor sijui ziliishia wapi.mambo kama haya pia yanawakatisha watu tamaa na kuogopa kutekeleza maagizo ya serikali.
 
Hakuna serikali ambayo wananchi wake hawalipi kodi.Serikali isiyokusanya kodi ni serikali mfu.Muhimu ni kwa wadau wote,serikali na wafanyabiashara kukaa chini na kutatua tatizo.Kwa sasa hakuna sababu ya kuoneshana misuli kwani uchumi wa nchi unadidimia na kuwapa usumbufu wageni wanaofika kununua bidhaa nchini.
 
ndio maana nawapenda sana wachina,huwezi kudhubutu kufanya hiki kinachofanywa na wafabiashara hapa Tanzania sasa.
hata Idd amini dada kule uganda kunakipindi watu wake walikuwa wakimpenda sana.
Kama kuna mapungufu yafanyiwe kazi,lakini hii haiwezi kuwafanya wafanyabiashara kukataa kuisaidia serikali kukusanya kodi
Serikali isipo jenga barabara nzuri tunalalamika,inapotaka kukusanya kodi ili iweze kuboresha miundo msingi ya nchii hii tunagoma,nini tunataka? nchi za wenzetu zinaendelea tunawaonea wivu,sisi hatutaki kuliwa ili nchi isonge mbele,
tusione vinaelea huko majuu,watu wametaabika jamani kufikia malengo.
Lakini pia serikali iwe makini krk hili,maana isije ikawa kama zile speed governor sijui ziliishia wapi.mambo kama haya pia yanawakatisha watu tamaa na kuogopa kutekeleza maagizo ya serikali.
Mkuu kama unadhani lengo la serikali hapo ni kukusanya kodi wangezitoa hata bure hizo mashine.... ni ufisadi tu upo nyuma ya biashara ya hizo mashine ... na kama unafuatilia vizuri sio kwamba wafanya biashara wamegoma kutumia hizo mashine, bali wamegomea bei kubwa ya hizo mashine...ambazo kwa kenya tu inasemekana ni hata laki haifiki bei yake
 
Hivi na akili zenu timamu na mawazo yenu finyu mnazani wafanya biashara hawalipi kodi, miaka yote mpaka wanafungua unamaana walikuwa hawalipi tatizo ni mfumo wa hizo machine
 
Zitto Kabwe

EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.

Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.
Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........​

Any way,tuendelee kusubiri tujue watafikia wapi,kibarua cha Shahada Mkuu-uya aka mama tunakopesheka
 
Hivi na akili zenu timamu na mawazo yenu finyu mnazani wafanya biashara hawalipi kodi, miaka yote mpaka wanafungua unamaana walikuwa hawalipi tatizo ni mfumo wa hizo machine

mimi sikubaliani na swal la mfumo,labda uwe huwaelewi wafanya biashara wakitanzania na afrika kwa ujumla
SOMA hapa
Zitto Kabwe

EFD zilianza kutumiwa mwaka 2010 kwa jumla ya wafanyabiashara 16,000 waliosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Mwaka wa fedha 2009/2010, kabla ya EFD, makusanyo ya kodi ya VAT yalikuwa tshs 791 bilioni. Mwaka 2011/2012 makusanyo yaliongezeka kwa asilimia 40 mpaka tshs 1,086 bilioni. Mwaka 2012/2013 makusanyo yakaongezeka kwa asilimia 63 mpaka kufikia tshs 1,770 bilioni. Makusanyo haya ni kwa Wafanyabiashara 16,000.

Iwapo awamu ya pili ya EFD itatekelezwa bila vikwazo jumla ya Wafanyabiashara 200,000 watafikiwa ikiwemo ni pamoja na vituo vya mafuta (Petrol Stations), Mahoteli na Migahawa nk. Mamlaka ya Mapato inatarajia kukusanya zaidi ya tshs 3,500 bilioni kutoka VAT peke yake iwapo EFD zitatumika.
Wafanyabishara kote nchini wanalalamika. Mwanzoni hoja kubwa ilikuwa ni bei za mashine hizi. Hoja inayoeleweka kabisa. Kamati ya PAC iliwahi kushauri kuwa Wafanyabiashara wapewe bure kabisa mashine hizi (bila kusubiri kurejeshewa kupitia kodi. Kimsingi mashine hizi ni Bure isipokuwa Mfanyabiashara huikopesha TRA na TRA kumrudishia kupitia kodi ya Mapato katika mwaka wa kwanza wa matumizi).
Leo nimesoma kwenye vyombo vya habari wafanyabiashara wanataka mashine hizi zisitumike kabisa, mpango mzima ufutwe. Ni kweli Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa mashine hizi?
Wafanyabiashara wanasema kodi ya VAT ya 18% ni kubwa mno na inakatwa bila kuzingatia manunuzi yao ie gharama zao za uzalishaji. Siku zote VAT inakatwa kutoka kwenye mauzo ghafi au kutoka faida?
Hebu tujadili masuala haya na yale malalamiko ya msingi yafanyiwe kazi na yasiyo ya msingi yapuuzwe.
Tutaendelea kuwa Taifa tegemezi iwapo hatutaweza kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Nchi hii haina mjomba.........​

Lakini wadau,tusizungumze tu juu ya kodi na maendeleo ya Taifa letu,ila tufikirie pia ni kwa jinsi gani wanasiasa na watawala wanavyotafuna pesa zetu kienyejienyeji,huenda nayo ni sababu na hawasemi,si mmeona na mmesikia inasemekana wajumbe wa bunge la katiba watalamba 49 mil,serikali haijakanusha,
vilevile si mmesikia ile 160 mil ya kiinua UTI WA MGONGO??? Ingawa serikali imekanusha,ila lisemwalo.......
Matumizi mabaya ya serikali yanasikika,ubadhilifu unasikika,mchwa wanaokula pesa za Halmashauri mnawasikia,hii ina maana gani???hii inatia hasira walipa kodi,si wafanyabiashara tu,hata mim mfanyakazi ambaye nalipwa kiasi kidogo kabisa
 
Igunga ngoma bado nzito,mgomo unaendelea,watu hawataki ccm na maEFD yao,mimi mwenyewe leo nimegoma kula,nakunywa tuuuuu!
 
Wakuu nimepita viunga vya mji wa sumbawanga mida hii mgomo unaendele na wafanyabiashara wote wamefunga sehem zao za biashara.

Kuanzia muuza vocha, mwenyewe kibanda cha mpesa/tigo pesa/groceries /mama ntilie hadi maduka makubwa hakuna huduma.

Kuna kundi linapita kila mtaa na kuwaamuru wale waliofungua sehem zao zao za biashara zifungwe ili kuunga mkono mgomo!!

Nadhan ipo haja kwa TRA kutoa elimu zaid kwa wafanyabiashara! !

kama wana ubavu wafunge wiki nzima
 
Kweli mkoroshokigoli, hapo kuna hoja pia. Naona walipakodi wanajua kodi yao haitumiki ipasavyo.
 
ndio maana nawapenda sana wachina,huwezi kudhubutu kufanya hiki kinachofanywa na wafabiashara hapa Tanzania sasa.
hata Idd amini dada kule uganda kunakipindi watu wake walikuwa wakimpenda sana.
Kama kuna mapungufu yafanyiwe kazi,lakini hii haiwezi kuwafanya wafanyabiashara kukataa kuisaidia serikali kukusanya kodi
Serikali isipo jenga barabara nzuri tunalalamika,inapotaka kukusanya kodi ili iweze kuboresha miundo msingi ya nchii hii tunagoma,nini tunataka? nchi za wenzetu zinaendelea tunawaonea wivu,sisi hatutaki kuliwa ili nchi isonge mbele,
tusione vinaelea huko majuu,watu wametaabika jamani kufikia malengo.
Lakini pia serikali iwe makini krk hili,maana isije ikawa kama zile speed governor sijui ziliishia wapi.mambo kama haya pia yanawakatisha watu tamaa na kuogopa kutekeleza maagizo ya serikali.

Hawa wafanyabiashara naweza kuwaita wapuuzi!! Haiwezekani wewe ufanye biashara bila kulipa kodi! Mfanyakazi analipa kodi bila kukosa, tena naambiwa sisi Watanzania ndio tunalipa kodi kubwa zaidi East Africa

(Soma Hapa TANZANIAN EMPLOYEES 'THE MOST HIGHLY TAXED IN EAC' )

hii ni kwasababu mzigo wa kulipa kodi wameachiwa wafanyakazi tena kwa kiwango kikubwa wa sekta binafsi.

Wafanyabiashara wanatoza kodi ya VAT 18%, baada ya hapo wanapeleka wapi? Matumboni mwao, halafu wanapita wakitukana wafanyakazi kuwa wajinga kwanini wasijiajiri!!

Hapa hata kama serikali ni dhaifu vipi, kwa hili nawaunga mkono, lazima kodi ilipwe na kila mwananchi mjenga nchi!
 
Lakini wadau,tusizungumze tu juu ya kodi na maendeleo ya Taifa letu,ila tufikirie pia ni kwa jinsi gani wanasiasa na watawala wanavyotafuna pesa zetu kienyejienyeji,huenda nayo ni sababu na hawasemi,si mmeona na mmesikia inasemekana wajumbe wa bunge la katiba watalamba 49 mil,serikali haijakanusha,
vilevile si mmesikia ile 160 mil ya kiinua UTI WA MGONGO??? Ingawa serikali imekanusha,ila lisemwalo.......
Matumizi mabaya ya serikali yanasikika,ubadhilifu unasikika,mchwa wanaokula pesa za Halmashauri mnawasikia,hii ina maana gani???hii inatia hasira walipa kodi,si wafanyabiashara tu,hata mim mfanyakazi ambaye nalipwa kiasi kidogo kabisa

Unajua ni kwanini kumekuwa na mwitikio mdogo kwenye mambo ya muhimu kama kupinga ongezeko la bei ya umeme, ufisadi kama huo unaoutaja hapo, ni kwa sababu kuna watu wengi wamekuwa na kipato cha ujanja ujanja kama hao wafanya biashara ndio maana hakuna kulalamika wanaona sawa tu.

Sasa wakianza kulipa kodi utaona mwamko, kila mtu atafikiria hela yake inavyopotea atakuwa mkali.... LAZIMA KODI ILIPWE!!
 
Back
Top Bottom