Mgomo wa wafanyabiashara nchi nzima kesho

MLIPAKODI

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
234
Reaction score
90
Kuna ujumbe unasambazwa na wafanyabiashara kufunga biashara nchi nzima kesho. Ujumbe huo ni huu hapa

"Breaking News,tarehe 11/02/2015, M/kiti wa wafanyabiashara anapandishwa kizimbani, kwa hiyo wafanyabiashara wote wanatakiwa kufunga biashara zao zote, pamoja na magari kutofanya safari zake yale ya safari ndefu na fupi.TANGAZO HILI NI MHIMU, mrushie mwenzio..."

My take: Serikali kwanini haiwasikilizi wafanyabiashara na kutatua matatizo yao? Wafanyabiashara wakifunga maduka nchi nzima serikali itaingia hasara ya shilingi ngapi?

Kazi kwenu wadau, nawasilisha
.
 
kufanya biashara kwa mazoea kunatakiwa kusitishwa kwa nguvu zote na serikali lazma ihakikishe wanalipa kodi

Wafanyabiashara wanalipa kodi vizuri tu ila ninacho kiona ni kwamba wanapinga kodi kandamizi. Ambazo hazita muadhiri sana mfanyabiashara kwani yeye atapandisha bei na ataye adhirika zaidi na hili ni mlaji wa mwisho ambaye ni ww na mm na ndugu zetu ambao wapo kijijini huko
 
shenz type zao kufanya biashara kwa mazoea kunatakiwa kusitishwa kwa nguvu zote na serikali lazma ihakikishe wanalipa kodi

Hawa ni wajinga sana, suala lao liko very clear, serikali imewafafanulia sana misingi ya uwekaji kumbukumbu za kodi na jinsi ya kukokotoa, lakini wanaonekana wana lao jambo. Wengi hawajasoma shule kabisa wanafuata mkumbo tu mimi naona sasa WAPIGWE TU
 
hakuna kitu hamlipi kodi ukiacha Wafanyabiashara wa mkoa wa Kilimanjaro nchi nzima wanaojiita wafanyabishara wamekataa EFD sasa unajiuliza nchi itaendeshwa vipi? na mnalipa vipi kodi bila ya rekodi kutoka EFD machines? Inabidi tuwaite wezi sasa maana hawaendani na jina biashara!
 
Mnaochangia hii hoja nakuwaponda wafanyabiashara mmewahifanya biashara? Vimekaliwa vikao vingi kutatua jambo hili utekelezaji wake nishida.
 

Wafanyabiashara hawakatai efd bali wanakataa mfumo wa efd. Efd inakata kodi kutoka kwenye mauzo haiangalii umepata faida kiasi gan. Efd haiingizai matumizi, kodi inatakiwa ikatwe kwenye faida na sio mauzo. Sasa hivi wafanyabiashara wanaambiwa walipe mapato mara mbili ya yale waliolipa mwaka jana. Wanatumia vigezo gani kupandisha mapato kiasi hicho? Huu ni unyonyaji kwa watz na sio kwa mfanyabiashara tu. Mlaji wa mwisho ndiye anaeumia zaidi kwa hiyo hili swala linamgusa kila mtz
 

sasa faida inatotolewa vp?na mbona kenya na Kilimanjaro wafanyabiashara hawajapinga? kama biashara yako haitengenezi faida si unaiacha na kufanya kitu kingine? kila mnachouza lazma kikatwe kodi hata kama ni pipi kila inayouzwa lazma sumni itoke! Wapuuzi sana wafanyabisahara wa nchi hii, tumewachoka!
 
Hawa ni wajinga sana, suala lao liko very clear, serikali imewafafanulia sana misingi ya uwekaji kumbukumbu za kodi na jinsi ya kukokotoa, lakini wanaonekana wana lao jambo. Wengi hawajasoma shule kabisa wanafuata mkumbo tu mimi naona sasa WAPIGWE TU

Punguza hasira, au mzigo mzito nini?!
 

Attachments

  • 1423551622221.jpg
    29.8 KB · Views: 120

Utam wa ngoma ingia ucheze hata walim wanapofanya migomo tunawapuuza hivyohivyo. Na ndio tunaona elimu yetu sasa ilipo. Mm binafsi sio mfanya biashara ila nimekuwa nifuatilia hili swala hili kwa karibu kwani kuna jamaa zangu wanafanya biashara na nikaona madai yao yanaukweli ndani yake. Katika nchi hii hakujawahi tokea mgomao wa wafanya biashara kabla ya mfumo wa efd, na kodi zilikuwa zinalipwa bila shaka na serikali ilipata mapato vizuri kabisa. Kwa nn serikali isirekebishe mfumo wa efd uendane na matakwa wanayotaka wafanyabiashara
 
Kodi za gesi na madini kama dhahabu,tanzanite,almas na mengine mengi hatujawai ambiwA zimeingizia nchi faida ,hakuna uwazi ktka mambo hayo yenye utajiri wa nchi yetu.leo serkari wanaacha kuangalia vianzo hvo,wanabaki kulazmisha wafanyabiashara knunua efd, viongozi wa nchi nyngi africa ni majuha ,sio wabunifu hata kidogo, mbona china hakuna efd lakini nch inatajirika sana,...serkari weka mapato ya resource alizotupa Mungu tukiridhika ndy mutushawishi efd ni nini na ina manufaa gani!
 
Sms zinazidi kuongezeka ngingine hii hapa


Serikali ichukue hatua wafanyabiashara ndio wanaoleta mapato ya kuendesha nnchi hii
 

achaneni na majungu biashara ni yako suala la kuanza kukusanyana na kutaka kugoma is a rubbissh kama unaona biashara hailipi close your shop na kafanye mambo mengine yatakayokufaisha kuliko kutuletea vurugu. mkitaka kuona mnafanya ujinga acheni vibanda vyenu uone watanzania wengine watiifu watalipa kodi na kufanya biashara kwa uaminifu na uadilifu. tumechoka tunataka tusikie creative idea za kimaendeleo. my brother if u cant do others will, give us the facillities including premises we will, we are tired of you!!!! shame on you!!!
 

Nafikiri hapa kuna utata. Kwa mujibu wa sheria ya sasa ya kodi ya mapato, kodi inakatwa kutokana na mauzo ghafi(gross sales).Hii ina kikomo kwenye shilingi milioni 20. Zaidi ya hayo mauzo ya shilingi milioni 20 kwa mwaka kodi inakatwa kutokana na faida na lazima mahesabu
yaliyokaguliwa yafanywe. EFD inarekodi mauzo ghafi na kodi ya ongezeko la thamani(VAT). Hapo mwanzo wafanya biashara waliifanya
asilimia 18% ya VAT kama faida yao, sasa wanashindwa kuiacha..
 
Huyu si ni mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo,sasa kwanini nchi nzima tugome?wagome hao hao wa Kariakoo
 
Mkuu nchi haiwezi ikaendeshwa kwa kumkamua mfanya biashara mdogo tu huku wakubwa wakiachwa tu kulipa kodi wanavyopenda, ni kweli hawa wafanya biashara wadogo wengi wao wanatumika tu, ila kitu kingine kinachofanya ulipaji kodi uwe mgumu hususani kwa nchi zetu hizi ni matumizi ya hizo kodi mtu haoni jinsi inavyomnufaisha kila siku ni habari za pesa fulani zimeliwa!! Na hiyo misamahama ya ovyo ya kodi. Ndio maana hata wao wanaona kama wanaonewa. Na hili suala la EFD hata serikali iseme izitoe bure bado itakuwepo shida tu watazusha lingine.
 
Kumpandisha mwenyekiti kizimbani ni sawa na Kutupandisha wafanya biashara wote kizimbani Tutafunga Biashara kusikiliza Kesi yetu.
 
Wakati mnaishinikiza serikali kuzikubali hoja zenu tumieni muda huu kuhamasishana kutoipigia kura ccm, hii ni golden chance kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…