Mgomo wa wafanyabiashara kesho

Mgomo wa wafanyabiashara kesho

Serikali imekurupuka na EFD bila kutoa elimu na kuagiza kama unapelekea pumba nguruwe. Hata wafanyakazi nahisi wapashwa kuanzisha mgomo maana inchi haitendi haki. Wabunge wanapewa mamilioni ya shilingi kwa jina la sitting allowance bila kukatwa kodi. wafungaji wanauza ng'ombe hata 40 kila mwezi hawatozwi kodi kama waajiriwa. we acha tu io siku
 
Nimepata taarifa kutoka kwa wadau fulani kwamba kesho mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Bwana Minja anapandishwa kizimbani Dodoma.

Kwa hiyo wafanyabiashara wanaendeleza mgomo wao wa kutofungua biashara siku mwenyekiti wao anapopandishwa kizimbani.

My take: Nimemsikiliza Minja kwenye power breakfast asubuhi anasema suala hili lilikuwa kwenye mazungumzo Kati jumuiya ya Wafanyabiashara na TRA, so kwanini serikali imfungulie kesi huyu Minja wakati suala liko katika mazungumzo.

Sasa ukifunga duka unamkomoa nani? Nyinyi ndio mnaogomaga kula halafu mnakonda na kufa au kupata vidonda vya tumbo. Ukisikia akili ndogo ndio kama hizo zenu
 
Walipe kodi, wafanyakazi wanalipa kodi kubwa, wenyewe wanapeta tuu, walipe kodi bila shuruti,

Hujui unachoongea hakuna mtu ambaye hataki kulipa kodi, go deep,, kuna double counting za kutosha kwenye kodi ya TANZANIA, everybody yupo tiyari kulipa kodi halali na kwa vigezo halali but not this way
 
Hii serikali legelege haiwezi hata kutekeleza sheria ya kodi ambayo imejadiliwa na kupitishwa na bunge! Ningekuwa waziri Mkuu ningefuta leseni za wafanyabiashara wote wanaofunga maduka kwa shinikizo la kukwepa mashine za efd. Mashine hizi ndizo zinatumika dunia nzima kuhakiki mapato na kukadiria kodi. Huko ulaya ambako tunatembeza bakuli hata wauza mboga sokoni wanazitumia na mboga zinatozwa vat! Futa leseni tuone jeuri yao ccm isibembeleze kura za wafanyabiashara za wafanyakazi na wakulima zinatosha.

Huko ulaya kodi inatumika kwa mambo ya msingi miundombinu ya kueleweka na chenchi tunapewa msaada halafu tunanunulia rada mbovu, huku kwetu kodi inatumika kununua magar ambayo hayana barabara za kupita, ambazo mvua ikinyesha dk 5 barabara zote zinapotea tunaona mito tu dar es salaam barabara ya uhuru kutoka round about mpka karume inajengwa almost miezi nane na zaid sa hiv et mkandarasi anatumia sururu kuchimba mtaro wa maji, wilaya ya ilala ambayo ndipo ikulu na wizara na idara na ofice kubwa zote zilipo, Ahsante
 
Tatizo ni Elimu Ndogo waliyonayo. Kwanza wengi biashara zao za Mazindiko na kutoa kafara. Mtu wa vile unafikiri ni rahisi kumwambia aendeshe biashara kisasa akakuelewa?

Heri yao wapatanishi maana milango ya Rehema I juu yao! Msiba wa mwenzio usiudharau kama unabusara mfariji maana hujui kesho!
 
Lipeni kodi..sisi wafanyakazi tunakatwa kodi hata senti moja hatusamehewi.
 
Hii serikali legelege haiwezi hata kutekeleza sheria ya kodi ambayo imejadiliwa na kupitishwa na bunge! Ningekuwa waziri Mkuu ningefuta leseni za wafanyabiashara wote wanaofunga maduka kwa shinikizo la kukwepa mashine za efd. Mashine hizi ndizo zinatumika dunia nzima kuhakiki mapato na kukadiria kodi. Huko ulaya ambako tunatembeza bakuli hata wauza mboga sokoni wanazitumia na mboga zinatozwa vat! Futa leseni tuone jeuri yao ccm isibembeleze kura za wafanyabiashara za wafanyakazi na wakulima zinatosha.

Acha uongo dunia nzima wapi unaongelea. ucwe kama bwabwa wewe. kama hujui kaa kimya. au uliza. waambie serikali yako kwanini hawataki cc tulipe kodi. unalipia container la futi 20 nguo tshs milion 40 halafu unaletewa risiti yenye kuonyesha umelipa tshs milion 12 kwanini wasituonyeshe hiyo account tutumbukize zote 40 au ni wewe unaetetea huu ujinga.
 
Uthibitisho

attachment.php
 
Ifike wakati sasa hii migomomigomo ipatiwe ufumbuzi,ni aibu kwa Taifa zima,kila kitu mgomo!viongozi kukaa kimya inamaana mmekubaliana na hali ilivyo siyo?usitumie nguvu kubwa kunyamazisha nguvu ndogo,chukua💃💃💃💃
 
Hili jambo wafanyabiashara pekee ndio wanafahamu, wengine wanapoga kelele tu. Maana wanasubiria mwisho wa mwezi walipwe hela ndogo
 
Hii serikali legelege haiwezi hata kutekeleza sheria ya kodi ambayo imejadiliwa na kupitishwa na bunge! Ningekuwa waziri Mkuu ningefuta leseni za wafanyabiashara wote wanaofunga maduka kwa shinikizo la kukwepa mashine za efd. Mashine hizi ndizo zinatumika dunia nzima kuhakiki mapato na kukadiria kodi. Huko ulaya ambako tunatembeza bakuli hata wauza mboga sokoni wanazitumia na mboga zinatozwa vat! Futa leseni tuone jeuri yao ccm isibembeleze kura za wafanyabiashara za wafanyakazi na wakulima zinatosha.

Na uchaguzi watapata wapi hela za kununulia vitenge, pilau, mafuta ya taa? Hao hao wafanyabiashara wanawezesha ushindi wa kishindo kuanzia balozi nyumba kumi, mtaa hadi .....
 
Minja anatumikia wanasiasa kuhujumu serikali. Fungeni maduka yenu kesho sisi leo tunanunua mahitaji muhimu na maduka mengine ndio faida kwao watafanya biashara nzuri kesho. Huyu Minja na wachaga wnzake wamekodi mamluki wa kuhujumu wafanyabiashara watakaofungua maduka. Vitisho vilivyoko ni pamoja na kuwachomea moto,faini na hujuma zingine. TRA imeshakanusha maelezo anayotoa Minja na kazi kubwa ya hizo mashine ni kuweka wazi mapato ya wafanyabiashara ili waweze kulipa kodi halisi kulingana na mapato yao wakati wa kulipa kodi. Na nyie makanjanja humu Jf wabunge wenu wanapoishambulia serikali haikusanyi kodi ipasavyo mnashangilia sana na inapoanza kukusanya kodi mnalia. Ni viroba vinawasumbua hivyo. Waambieni hao wafanyabiashara wasifungue kabisa

USHAURI KWA WAFANYABIASHA
Ni muda muafaka sasa kuanzisha jumuia huru ya wafanyabiashara itakayokuwa na uhuru wa mawazo na maamuzi,ambayo itakuwa huru na haitumikii wanasiasa,muachieni Minja hiyo jumuia na wachaga wenzake.
 
Hujui unachoongea hakuna mtu ambaye hataki kulipa kodi, go deep,, kuna double counting za kutosha kwenye kodi ya TANZANIA, everybody yupo tiyari kulipa kodi halali na kwa vigezo halali but not this way

Wewe ndio hujui unachoongea hakuna mfanyabiashara anayependa kulipa kodi halisi kulingana na mapato yake. Wafunge tu sisi leo tunanunua mahitaji yetu mapema,tena waambieni warefushe mgomo maana wafanyabiashara wengine wananufaika na mgomo huu. Kwanza huu mgomo hauko huru kuna vitisho na kulazimishana. Ni vizuri wafanyabiasha wakaanzisha jumuiya nyingine itakayokuwa huru wamuachie Minja na wachaga wenzie jumuiya hiyo kuwatumikia wanasiasa
 
Acha uongo dunia nzima wapi unaongelea. ucwe kama bwabwa wewe. kama hujui kaa kimya. au uliza. waambie serikali yako kwanini hawataki cc tulipe kodi. unalipia container la futi 20 nguo tshs milion 40 halafu unaletewa risiti yenye kuonyesha umelipa tshs milion 12 kwanini wasituonyeshe hiyo account tutumbukize zote 40 au ni wewe unaetetea huu ujinga.

Acha kudanganya wewe. Wafanyabiashara ndio chanzo cha hayo yote unayosema wala wewe si mfanyabiashara kwa namna ulivyocomment,wala hujui mfumo wa kodi hapo bandarini na jinsi gani deal zinavyopigwa kukwepa kodi.
 
MTUNZI KATUMIA FALSAFA NZURI SANA.

Mtoto mdogo alimfuata baba yake na
kumuliza, "
Nini maana ya SIASA?"
Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu
kujibu kwa mfano huu,
Mimi natafuta fedha
ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI,
Mama yako yeye anasimamia matumizi ya
fedha, hivyo mwite SERIKALI,
Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie
mahitaji yenu hivyo nyinyi
twawaita WANANCHI.
Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa
ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI. Na mdogo
wako ambaye ni mdogo tumwite FURSA ZA
BAADAYE" Haya sasa mwanangu hebu fikiri na
uone kama ina kupa jibu la kuridhisha....!
Kijana akaondoka na kwenda kulala huku
akifikiri na kuyatafakari maneno aliyoyasema baba.
Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni
mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua
kuamka na kwenda kumcheki. Akaona mtoto
kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia
kuashiria anahitaji msaada. Akaamua aende
chumbani kwa baba na
mama, akamshuhudia mama akiwa peke
yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote.
Hakutaka kumwamsha akaona angemsumbua
mama, akarudi na kwenda chumba cha dada wa
kazi na kuona mlango umefungwa.
Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na
kuona dada wa kazi akiwa na baba. Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya kuwa
na msaada wowote kwa mdogo wake.
Siku ya pili mtoto akamwambia baba,
"sasa nafikiri naelewa maana halisi ya SIASA."
Baba akasema,
" safi sana mtoto mzuri,
haya sasa niambie kwa maneno yako maana halisi
ya siasa kwa jinsi
ulivyoitafakari"
Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI
anamyanyasa na kumtumia vibaya
MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi mzito, Na
WANANCHI hawasikilizwi shida zao huku FURSA
ZA BAADAYE zikiwa zimesusiwa kwenye uchafu bila
msaada.
Baba kidogo azimie.
TAFAKARI, CHUKUA 🏃👣HATUA
 
Mlipe kodi achen janjajanja cox mnairudisha nchi nyuma kimaendeleo wazir mwenye dhamana futa leseni za hao wanaofunga mduka(wezi Wa kodi) lipa kodi kwa manufaa ya nchi but tatizo ni hii serikali ya maccm hawawezi chukuwa uamuzi mgumuuu
 
Hili jambo wafanyabiashara pekee ndio wanafahamu, wengine wanapoga kelele tu. Maana wanasubiria mwisho wa mwezi walipwe hela ndogo

Exactly, mtu umekaa unapiga kelele mbona wafanyakazi tunakatwa kodi muulize sh ngap?! Utasikia PAYE 80,000 wakati mtu anaingiza container la alluminium bandari unatoa 50m, dukani unaeka TRA nao wanataka 18% after sales, anakuja mteja ananunua anapeleka dukani kwake mbagala akauze naye ana 18% nyingine kutoka TRA, kuna leseni huduma za jiji, na kodi kibao nyingine halaf mtu anakaa nyuma ya keyboard anaongea tu
 
Mlipe kodi achen janjajanja cox mnairudisha nchi nyuma kimaendeleo wazir mwenye dhamana futa leseni za hao wanaofunga mduka(wezi Wa kodi) lipa kodi kwa manufaa ya nchi but tatizo ni hii serikali ya maccm hawawezi chukuwa uamuzi mgumuuu

Its not that easy, do u think akili hawana au unadhani nchi hii itaendeshwa na PAYE ya 120,000
 
Kweli hii nchi tulipo fika pabaya serikali inatakiwa isikilize matatizo ya wananchi wako la sivyo kunasiku kutanuka vibaya

Wewe ndio umefikia pabaya kutokana na akili yako kutokuwa na uwezo wa kupambanua
 
Back
Top Bottom