Mgomo wa Manesi Wote haukwepeki!

Mgomo wa Manesi Wote haukwepeki!

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
8,246
Reaction score
12,795
Wakati ndio huu,jumatano hakuna kutoa huduma,hakuna sababu tena ya kuwategemea madaktari watetee maslahi yenu.

Mbona matatizo yenu ni makubwa mno? Nyie ndio kada pekee katika sekta ya afya ambao mnakaa karibu na mgojwa zaidi ya saa 8 kwa siku, nyie ndio mnaongoza kwa wingi katika watumishi wa afya, watumishi wanaoambukizwa kwa wingi magonjwa kama TB, ukimwi nk ni wauguzi kwasababu ya ukosefu wa vifaa vya kujikinga, lishe duni itokanayo na mishahara duni.

Kwanini ni nyie tu mnaolipia leseni ya kutoa huduma elfu hamsini, kisa eti ni sheria iliyopitishwa na bunge, sheria kandamizi na ya kinyonyaji?

Nesi wa Tanzani ana kipato gani cha kulipia leseni?

Manesi kuwa na sauti moja, hivyo vyama vyenu vya TANA, PRINMAT, nk ni wezi tu, malengo yao na perdm za vikao vinavyofanyika kwenye mahoteli makubwa, mtetezi wa muuguzi ni muuguzi mwenyewe na sio TANA.

WAKATI WA KUONYESHA MSHIKAMANO NI HUU!
 
malezenu migomo yenu nasi mapolisi tuanze wa kwetu, sio kila siku watutume kunanii tu.
 
aisee.... Imagien the world without nurses
 
Last edited by a moderator:
Polisi nao wagome kwa jinsi walivyoridhika na silaha tu mkononi hata kama mifukoni wanapunjika?? Aaaahh wapi, ni heka za abunuasi tu hizo kwake huyu mwenzetu aliyejichombezea japo kaneno hapo kwenye posti namba tatu hapo juu!!!!!!!!!!!!!

nyie mgome? Itakuwa ni ajabu la 9 la dunia.
 
Katibu wa TANA taifa ni mmojawapo wa mamluki wanaotumiwa na serikali kuwagombanisha manesi na madaktari.

Ni mfanyakazi wa wizara ya afya (watuhumiwa) halafu hapo hapo analazimisha kuwa muwakilishi wa wauguzi kwenye vikao vya kudai maslahi zaidi.

Kipindi chote alichokuwepo hapo wizarani amefanya nini kuwatetea manesi?

Mtetezi wa kweli ni lazima ateuliwe kwenye mkutano wenye ajenda ya kudai maslahi yenu la sivyo mtawekewa mamluki.

Hiyo jumatano lazima mkutane ili mjipange.
 
Duh, sasa wewe umeanza kuwataja, mimi kwenye post yangu sikuanika hivi

Good one... na wanatumiwa kweli!!
 
duh, sasa wewe umeanza kuwataja, mimi kwenye post yangu sikuanika hivi

good one... na wanatumiwa kweli!!

mkuu lazima manesi wajue adui yao mkuu ni viongozi wao ambao wameshidwa kuwatetea kwa miaka mingi na badala yake wanaishia kulipisha leseni na michango mengine ya ajabu ajabu!
 
manesi bora mshituke mapema serikali hii bila migomo hamuwezi kukumbukwa...

Aliyesema na mapolisi wagome anawajua anawasikia? Hao ni watu wa kudanganywa! Si unakumbuka kipindi cha bajeti waziri nahodha aliliambia bunge posho za askari polisi zimepanda kutoka 100,000/- hadi 200,000/-, lakini hadi leo wanavyotumwa kushusha bendera za CHADEMA usiku huko Tunduma hawajaongezewa hicho kiwango...

Wenyewe wanaamani na sasa hivi wanajiandaa kwenda kutumika ARUMERU!

Jamani, kwa umoja wetu tumwombe Mungu awafanye hawa mapolisi wetu wajue thamani yao waweze kudai haki zao!
 
Watumishi kada zote wangekuwa na umoja wa hivyo nchi ingekuwa tambarare sana,viongozi full nidhamu lkn mmmmmmmh lets wait and see
 
Ni kweli nawashangaa hawa watumishi wengine wa afya wanavyosubiri kudandia mgongoni mwa madaktari....
 
Tutafute raisi wa kukodi labda nchi itapata maendeleo
...naunga mkono hoja,tutangaze tenda ya nafasi ya uraisi,tuseme hii "nafasi ya urais tz iko wazi",tunataka mtu mwenye sifa ya uraisi,atakaye-shikilia nafasi ya urais wa tz kuanzia tarehe1/07/2012 hadi -/10/2015 tutakapo fanya uchaguzi...ili wazo mbona ni zuri tu,kuna viongozi wastahafu wenye CV nzuri sana wanaweza kuomba hii nafasi tukawapatia hii kazi...niwataje kwa uchache ambao naamini wakituma maombi ya kazi hatuwezi kunyima...
1.B.CLINTON
2.CHISANO
3.rais anaye shikilia tuzo ya MO Hibrahim kwa sasa(simkumbuki jina lake)
4.unaweza kuendele...
 
Wakati ndio huu,jumatano hakuna kutoa huduma,hakuna sababu tena ya kuwategemea madaktari watetee maslahi yenu.

Mbona matatizo yenu ni makubwa mno? Nyie ndio kada pekee katika sekta ya afya ambao mnakaa karibu na mgojwa zaidi ya saa 8 kwa siku, nyie ndio mnaongoza kwa wingi katika watumishi wa afya, watumishi wanaoambukizwa kwa wingi magonjwa kama TB, ukimwi nk ni wauguzi kwasababu ya ukosefu wa vifaa vya kujikinga, lishe duni itokanayo na mishahara duni.

Kwanini ni nyie tu mnaolipia leseni ya kutoa huduma elfu hamsini, kisa eti ni sheria iliyopitishwa na bunge, sheria kandamizi na ya kinyonyaji?

Nesi wa Tanzani ana kipato gani cha kulipia leseni?

Manesi kuwa na sauti moja, hivyo vyama vyenu vya TANA, PRINMAT, nk ni wezi tu, malengo yao na perdm za vikao vinavyofanyika kwenye mahoteli makubwa, mtetezi wa muuguzi ni muuguzi mwenyewe na sio TANA.

WAKATI WA KUONYESHA MSHIKAMANO NI HUU!

Duh hii bongo tu!
TANZANIA zaidi ya uijuavyo!
 
Back
Top Bottom