Tuki waajiri wengine msilalamike
Shame on Bonge wa Clouds FM na kipindi cha Power Break Fast , asubuhi amesema hospitali zote Dar es salaam zinachapa kazi kama kawadida, jamaa yangu amewahi Mhimbili kuchukua namba kwa ajili ya kumwona Dr. saa 9 alasiri akakuta hakuna bonge la mgomo.
mna ubavu?tuki waajiri wengine msilalamike
mgomo hakuna ila kuna vikao endelevu sasa subiri matokeo ya hivyo vikao endelevu ndio utajua kuna mgomo au la.pigeni propaganda huku watu wakiendelea kufa halafu baadae muanze kuomba kuongea na madaktari.Jamani tupatieni updates za mahospitali mengine hapo DSM na mikoani tafadhali?
mgomo hakuna ila kuna vikao endelevu sasa subiri matokeo ya hivyo vikao endelevu ndio utajua kuna mgomo au la.pigeni propaganda huku watu wakiendelea kufa halafu baadae muanze kuomba kuongea na madaktari.
soma post yako namba 23!!umeandika wewe au umeandikiwa?[/COLOR]
Boss hapo kwenye red, unaniambia mimi au Nyoni? Sometimes uwe unasoma kwa makini post za watu, GTs hawakurupuki mkuu!
Poleni kwa kusumbuliwa ni haki yenu kudai haki yenu ila mtuangalie nasisi maskini,
nina mgonjwa muhimbili lakini bado ninaamini mna haki ya kugoma kudai haki zenu, wanasiasa wana kauli za utata sana, kazi ya ualimu na kazi ya udaktari kila siku wanaimba eti ni kazi ya wito, loh! siasa ni ajira, proffessional ni kazi ya wito, kaazi kweli kweli.
Kuna mtu katoka Muhimbili kaniambia MOI ndio inaonyesha dhahiri kuwa imeathiriwa na mgomo......mapokezi hakuna wagonjwa na pia kuna mgonjwa amemkuta kaletwa na ambulance tangu saa 12 alfajiri hadi saa tano hajapokelewa.
Dr. Chichi huku mikoani tunawategemea huko kukoleza nguvu ya moto huu,hebu basi wahimizeni na manesi,famasia,watu wa maabara,nk wawape nguvu!
Ninafahamu fika kuwa bila daktari huduma hakuna lakini hawa kada zingine za afya ni waoga sana....weka bidii moto usambae tumechoka kulipwa sh.10,000 kama on call allowance ya masaa 24 ambayo pia kuipata mpaka iwe birthday ya mkurugenzi!
Nikiangalia serikali yetu na viongozi wake nakumbuka story za mfalme juha
Najua hata mimi au mwanangu au yoyote provided ni binadamu hasa wa hali ya chini atauguwa na tiba yake ni nyinyi ma-DR mnaoendelea na mgomo,lakini kwa hili mi niko upande wenu tena nawaunga mkono kwa asilimia mia,maana siafiki mtu kumfanyisha kazi halafu usimlipe,siafiki mtu kumwambia unatakiwa kupewa nyumba au kupewa asilimia fulani ikiwa ni gharama ya nyumba tu kwa kuwa ofisi husika haina idadi ya nyumba kukidhi mahitaji,siafiki pia kumwambia mtu utalipwa kiasi kadhaa kama allowance ama ya kjuikimu au OT ama vyovyote halafu usitekeleze na ni mtu mzima na akili yake,na hapo anapofanyia kazi ndipo tegemeo lake,familia yake,ndugu zake nk halafu unamwambia ni wito.kama ingelikuwa hivyo nani yuko tayari kufanya kazi huko aliko tofauti na fani hii na asilipwe?au ukisomea fani hii maana yake ni kujitolea bila malipo?kama ni hivyo nani yuko tayari tena kusomea fani isiyokuwa na malipo?hapa tatizo ni serikali na chama chake.
onyesheni msimamo nanyinyi madaktari sio muanze mambo ya kujipendekeza pendekeza kwa serikali,ingefaa hili likawa fundisho kwa serikali legelege kama hii chini ya CCM.
Aisee! Zumbemkuu, umenikumbusha habari ya mbuni! Mbuni ni ndege mkubwa sana. Mbuni mkubwa hufikia urefu wa FUTI TISA, na uzito wa Kilo 130! Lakini mbuni anachekesha! Akiona adui, anakificha kichwa chake ndani ya mchanga, halafu kiwiliwili chake chote kinakuwa kinaonekana! Ni sawa na Serikali ya JK, inayowatisha waandishi wasitangaze juu ya mgomo wa Madaktari, na kama wakitangaza, wautangaze kwa kupotosha! Serikali ya Mbuni, hiyo!
Japokuwa ushirikiano na wanahabari ni muhimu katika kipindi hiki cha mgomo wa madaktari, lakini inabidi wanahabari waelewe kuwa madaktari hawajagoma ili watangazwe kwenye redio na TV, au wandikwe magazetini! Hivi wanapoambiwa kuwa wapishe mikutano ya ndani kisha watapewa taarifa...halafu wanasusa eti tu kwa sababu wametolewa nje, wanawanyima waTanzania haki yao ya kupata habari.
Lakini habari ni habari tu, ikiwa hot mwandishi atakuja tuu hata hasipoitwa. Hii habari ya mgomo sasa ni hot, na kesho itakuwa hot zaidi, sasa mwandishi hasiyetaka kuuza gazeti au kureport kwenye TV au redio na hasije...kwa kifupi hicho hakitasimamisha mgomo!