Mgomo wa madaktari-serikali imejilipua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari-serikali imejilipua!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shansila, Mar 8, 2012.

 1. S

  Shansila Senior Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgomo wa madaktari umeanza tena katika mikoa/miji yenye ushawishi mkubwa ya Dar,Mwanza na Mbeya!Athari za mgomo zitaanza kuonekana punde.Lkn mgomo huu ulikuwa unazuilika,hasa:
  1- kwa serikali kuwaondoa ktk nafasi zao Waziri wa afya na naibu wake kwa vile si wao tu wanaoweza kuongoza wizara hiyo.

  2-kwa serikali kuendelea kutafuta mwafaka na madaktari kwa njia ya mazungumzo kwa kuunda tume huru inayoshirikisha pande zinazokinzana.

  Lakini serikali kupitia mtoto wa mkulima imeamua kumeza bomu na kujilipua kwa :-

  1.Kuwapuuza madaktari kwa kudai kuwa imejipanga kuwahudumia wagonjwa ktk kipindi hiki cha mgomo wakati haina alternative,

  2.Kuwagawa madaktari ili kuwadhoofisha wasiwe na umoja(divide & rule),kwa kueneza propaganda kupitia vyombo vyake vya habari kuwa huduma ktka mahospitali zinaendelea kama kawaida huku watu wakiendelea kufa na wao kuendelea kukaa maofisini.

  My take:
  Serikali isichukulie mgomo wa madaktari kama suala la kisiasa,hata kama ni la kisiasa!Wnaoumia ni walipakodi wake.
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  serikali legelege ni ile isiyowajali wananchi wake hivyo kuwatoa kafara ili kushinda uchaguzi arumeru.


  mizambwa
  inaniuma sana!!!
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mpaka sasa bado napata shida sana kuelewa ni kwanini Serikali inashindwa kuwaondoa hawa mawaziri,hivi uwajibikaji upo wapi siku hizi?Kuna jambo gani ambalo ni muhimu sana toka kwa hawa mawaziri mpaka iwe nongwa kwao kujiuzuru?Nijuavyo uwaziri si nafasi ambayo mtu anaweza kusema alisomea na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuishika,inamshinda nini Rais kuwaondoa hawa watu mapaka mgomo mwingine unatokea?Rais na serikali yake wanafaidika na mgomo huu au wanafurahi kuona wagonjwa wakifa bila msaada?
  Inaumiza sana kuona viongozi hawa ambao walikuwa wakipita huku na kule kuomba kura kwa wananchi kwa ajili ya kuwatumikia hii leo wamegeuka kuwa watumikiwa na hawajali hali za wanaowatumikia.
  Shime wananchi nadhani sasa mmekwishajua kuwa serikali ya CCM imeshindwa kutatua matatizo yenu na kwa kuanzia au kuendelea basi Arumeru msifanye makosa kwa kuinyima kura CCM.
   
 4. S

  Shansila Senior Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Brother Jose,wananchi wa Arumeru hata wakikipa chama kingine kura zao,mwisho ccm itashinda tu.CCM itashindwaje huku kina John Tendwa,Raja Kiravu & Lewis Makame wakiwapo kwenye tume ya uchaguzi na msajili wa vyama vya siasa?Tusijiingize sana kwenye siasa,tujiulize ni kweli serikali yetu imejipanga kuwahudumia wagonjwa ktk kipindi cha mgomo wa madaktari?
   
Loading...