Mgomo wa madaktari: Kasumba ya kulalamika bila kuchukua hatua kwa vitendo, nani aikomeshe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari: Kasumba ya kulalamika bila kuchukua hatua kwa vitendo, nani aikomeshe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gmadenis, Feb 9, 2012.

 1. g

  gmadenis Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mgomo wa madaktari ni wiki ya tatu hii inapita tunaelekea ya nne na serikali haijaonesha nia ya dhati kutatua tatizo hili na kwa bahati mbaya anayeumia na mwananchi wa kawaida. Ni wakati wa kurudi nyuma na kujiuliza mmoja mmoja, kwamba mimi kwa nafasi yangu nimefanya nini au nimefanya harakati gani kusaidia kutatua tatizo hili? Maana kuilaani serikali kwa maneno tu na kulalamika haisaidii kitu, na watanzania wanaendelea kufa.

  Tuna mambo mawili ya kufanya, kutatua tatizo kwa vitendo au kukaa kimya kabisa tuachane na mambo kulaani na kulalamika bila kuchukua hatua yoyote. Yaanzishwe maandamano nchi nzima kuishikiza serikali itatue tatizo kabla hali haijawa ya kutisha. Serikali ni kama nahodha wa Meli, jambo kubwa la serikali ni kulinda raia wake dhidi ya hatari zozote.
   
Loading...