Mgomo wa mabasi wanukia tena

Mgomo wa mabasi wanukia tena

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,028
Reaction score
59,657
Huu utakuwa wa nchi nzima, TABOA wamekataa na hawakubaliani na nauli mpya iliyowekwa na SUMATRA

Leo mpaka sa sita wasipopata jibu hawatakata ticket. Na mgomo kesho utakuwepo kama kawa.

Mkurugenzi wa sumatra yeye kasema kuwa Taboa hawajui taratibu kwani taratibu zipo badala ya kugoma.

=============================

Hali-ilivyokuwa-jijini-Dar-es-Salaam-kufuatia-mgomo-wa-magari-na-daladala-uliofanyika-Aprili-10-2015-750x350.jpg

KUNA kila dalili ya kutokea mgomo mwingine wa madereva wa mabasi yanayoofanya safari zake kati ya mikoa na mikoa pamoja na daladala nchi nzima, kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kile kinachoelezwa kuwa ni kiburi cha Serikali.


Aprili 10, 2015, madereva wa mabasi ya abiria yanafanya safari zake mikoani pamoja na madereva wa daladala walifanya mgomo nchi nzima, ambao ulitikisa kwa kiasi kikubwa sekta hiyo ya usafiri na usafirishaji kabla ya viongozi wa Serikali kuingilia kati ili kunusulu hali mbaya kwa abiria iliyokuwepo.


Katika mgomo huo uliochukua takriban saa tisa, ulioanza asubuhi saa 12:00 hadi saa 9:00 alasiri ambapo mabasi ya mikoani na daladala yaliporejesha huduma, mawaziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka walilazimika kutoka maofisini mwao na kwenda kusikiliza madai ya madereva hao, ingawa awali kabla ya mgomo huo, walikuwa wamewapuuza.


Habari za uhakika zilizoifikia FikraPevu na baadaye kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama Vya Madereva nchini, Clement Masanja, zinasema mgomo huo mwingine wa madereva wa mabasi unaweza kuanza muda na siku yoyote kuanzia sasa.


Sababu zinazotajwa na madereva hao kutaka kurejea kwenye mgomo wao mwingine huo, zimetajwa kwamba ni...

Habari zaidi, soma=>
: FikraPevu: Mgomo mwingine wa Madereva wa Mabasi ya Abiria na Daladala wanukia kuanzia Sasa
 
Hawa wafanyabiashara ni tatizo kubwa katika hii nchi...............
yaani kwanza haya mabasi hatujaona wanatoa tamko lolote lile juu ya ajali zinazotokea na kugharimu maisha yetu, lkn eti apa wanatakataa kisa nauli. Nauli yenyewe ukipiga hesabu ni sh 700-1500 kwa safar ndefu.

sasa apa wanachokitaka eti kugoma na sisi abiria tugome kupanda kwasabb ya ajali wanazotusababishia, imagine vilema wangapi wanazalishwa kupitia hizi ajali, achili mbali wanaoachwa wajana ama wagane, na watoto yatima
 
duh mazoezi ya kutembea tutayafanya kwa lazima...
 
Wasubiri subiri hadi December ndio wagome sisi wa kas tusiende kuhesabiwa.
 
Serikali inazidi kupelekeshwa! Ina maana hawa wamiliki walikuwa wapi kupunguza bei ya nauli pindi mafuta yaliposhuka? halafu saivi wanashinikiza nauli zipande mafuta yakishuka jamaa hawapunguzi hata hamsini!
 
Taboa huwa siwaelewi ktk swala la kupanda nauli huwa wanakua na ushirikiano mkubwa sana pale mafuta yakipanda bei na kuongeza nauli,tetesi tuu ya kupanda bei huwa nauli kamili lakini mafuta yameshuka bei wao wanakuja na sera ya vipuli,mafuta yakipanda bei nauli hupanda haraka vipuli sio sababu tena. Mkae mjadiliane ni swala la muda tuu kuanzia mwezi wa saba mafuta yatapanda tena bei hapa Tanzania tuu as dola inavyokua imara ughali wa kununua mafuta utaongezeka kwa kuagiza. Viongozi wetu siasa ktk mambo ya msingi kabisa.
 
Wao wanajua mamboyaotu, sasa walisema wana mabasi zaid ya 300 wayalete tuone
 
Serikali inazidi kupelekeshwa! Ina maana hawa wamiliki walikuwa wapi kupunguza bei ya nauli pindi mafuta yaliposhuka? halafu saivi wanashinikiza nauli zipande mafuta yakishuka jamaa hawapunguzi hata hamsini!

Mbona umeandika kama mtu mwenye haraka, hebu pangilia taarifa yako ili namimi nielewe niweze kuchangia ikibidi
 
Huu utakuwa wa nchi nzima, TABOA wamekataa na hawakubaliani na nauli mpya iliyowekwa na SUMATRA

Leo mpaka sa sita wasipopata jibu hawatakata ticket. Na mgomo kesho utakuwepo kama kawa.

Mkurugenzi wa sumatra yeye kasema kuwa Taboa hawajui taratibu kwani taratibu zipo badala ya kugoma.


===
Mgomo mzito wanukia.

 Mabasi yote ya abiria yapanga kugoma nchi nzima.

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra)
Siku 17 baada ya madereva wa mabasi mchini kugoma na kutikisa nchi, Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (Taboa) kimetangaza mgomo mwingine nchi nzima.

Mgomo wa Aprili 9, mwaka huu uliodumu kuanzia alfajiri hadi saa 7:00 mchana ulitikisa nchi na kuwaathiri abiria wengi waliokuwa wanasafiri kwenda maeneo mbalimbali ya nchi.

Jana Taboa walitangaza kusitisha utoaji huduma kuanzia kesho ikiwa ni hatua ya kupinga nauli mpya za mabasi zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Kufuatia hali hiyo, Taboa kimewataka mawakala kutokatisha tiketi kuanzia leo kwa abiria hadi hapo Sumatra itakapotoa taarifa za kuruhusu nauli ya zamani ziendelee kutumika.

Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu, alitoa taarifa hiyo jana wakati akitoa majumuisho ya mkutano mkuu wa dharura uliojumuisha wadau wa usafirishaji.

Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu tatu ambazo ni ajali za barabarani, nauli mpya zilizotangazwa na Sumatra, madaraja ya mabasi, mgomo wa madereva na vituo vya kubadilishia madereva wanaokwenda umbali mrefu.

Mrutu akisoma maazimio hayo baada ya kumalizika kwa majadiliano hayo, alisema sababu iliyotolewa na Sumatra kushusha nauli kutokana na bei ya mafuta kushuka siyo kigezo muhimu bali ni shinikizo kutoka kwa wanasiasa.

“Kesho kutwa (kesho) hakuna gari ambalo litatoka kituo cha mabasi Ubungo kwenda mkoani na kama tutapigwa mabomu tupigwe, ila msimamo wetu uko pale pale wa kutotoa magari hadi Sumatra watakapotoa tamko la kutaka nauli za awali ziendelee kutumika,” alisema.

Kuhusu ajali, alisema kutokana na kukithiri kwa ajali za mabasi, wanakubaliana na utaratibu uliowekwa na serikali wa madereva kubadilishana wanaokwenda masafa marefu katika vituo ambavyo vitatengwa ili kupunguza ajali hizo.

KILOMITA 80 KWA SAA
Mrutu aliagiza madereva wote watumie mwendo wa kilomita 80 kwa saa na wazingatie sheria za usalama barabarani na watakaokiuka sheria hizo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Alisema kuanzia Mei mosi, mwaka huu wataanza kutumia vituo maalum vya kubadilishia madereva kwenye mabasi ya masafa marefu kwa muda wa miezi mitatu kwa majaribio.

Vituo hivyo ni Singida mjini, kwa mabasi ya Dar es Salaam kwenda Mwanza, Bukoba, Kahama; na kituo cha Morogoro kwa mabasi yanayokwenda mikoa ya nyanda za juu kusini.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na mapendekezo ya Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani, kubainisha kuwa chanzo cha ajali kwa mabasi yaendeyo masafa marefu ni uchovu wa madereva.

Mrutu aliwataka wamiliki wa mabasi kuhakikisha madereva wao wanazingatia taratibu na sheria zilizowekwa na Jeshi la Polisi pamoja na Sumatra ili utoaji wa huduma uweze kwenda vizuri.

Alisema madereva ambao wameanza tabia ya kuwachafua wamiliki wa mabasi kwamba wamekuwa wakielekezwa kwenda mwendo wa kasi ili kuwahi abiria watawachukulia hatua kwasababu suala hilo siyo la kweli.

“Mimi ninunue gari la mamilioni halafu nimlazimishe dereva aende mwendo kasi ni kitu ambacho hakiniingii akilini inamaana sina uchungu na gari yangu,” alisema Mrutu

Alisema mwendokasi wa kilomita 80 kwa saa, uwepo wa vituo vya kubadilisha madereva wa mwendo mrefu na kukoma kwa urasimu miongoni mwa askari polisi kuwa suluhisho la ajali za barabarani nchini.

Mrutu alisema katika utafiti wao wamebaini kuwa chanzo kimojawapo kinachosababisha kutokea kwa ajali nchini ni ubovu wa miundombinu ya barabara.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa maadili iliyopewa jukumu la kuchunguza tatizo la ajali nchini, Abdulrazack Kimaro, alisema ajali za barabarani zinasababishwa na mwendokasi.

Alisema katika uchunguzi wao wamebaini hakuna hata dereva mmoja anayezingatia sheria za usalama za barabrani ingawa Sumatra na askari wa kikosi cha usalama barabarani wanakuwapo bali kinachofanyika ni kumalizana kwa kupeana ‘kitu kidogo’.

Abdulrazack alisema wao kama wamiliki wa mabasi hawako tayari kuendekeza madereva wanaokwenda kinyume cha sheria, hivyo kila mmiliki kwa muda wake atoe somo kwa dereva wake juu ya makubaliano hayo ili kudhibiti ajali. Alisema madereva wanatakiwa kusimamiwa kikamilifu kwenye utendaji wao na kwamba kila mmiliki anapaswa kuwasilisha majina ya dereva wake na vyeti, leseni kwa Taboa ili kuthibitisha ufanisi wake kwa kazi anayoifanya.

Naye Katibu wa Wamiliki wa Mabasi Mkoani Kigoma (Kiboa), Hussein Kalyango, alisema serikali inatakiwa kuyafanyia marekebisho baadhi ya mambo yakiwamo kanuni za usafirishaji zinazomkandamiza mmiliki zaidi huku zikimwacha dereva nje ya lawama mfano chanzo cha ajali.

Kalyango alisema utaratibu wa sheria za Sumatra zinamlenga mmiliki wa basi kwa utovu wowote wa basi ambao anaufanya dereva.
“Tunaiomba Sumatra ibadilishe sheria makosa anayofanya dereva adhibitiwe dereva na hata kuchukuliwa sheria za zaidi na tunatakiwa kushirikiana Sumatra, polisi na sisi kumaliza ajali hizi za barabarani,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
Wenye mabasi watakaokuwa tayari kutoa huduma kwa raia wasaini na kutekeleza mara moja madhumuni ya leseni zao.

Kiukweli wanachotaka kufanya taboa ni kuhujumu uchumi wa taifa.

Watakaokataa kwa kisingizio chochote Futia leseni hao!!! na muwaalike rasmi watengeneza mabasi ya yutong waingie kwenye biashara na muwapunguzie baadhi ya ushuru.

Watakaofutiwa leseni hawataruhusiwa kupata leseni kufanya biashara yoyote hapa tanzania.

Manake tumechoka sasa!!!
 
bar na grocery/pombe zipigwe marufuku au
ziendelee kuuzwa karibu na mabasi?/stendi/taboa?
Kama ziendelee:
Huduma za pombe ziwekwe katika kila basi?
Bangi?
N.k.??
?
?
 
sijawah sikia serikali ya hovyo kama hii kwa umri wangu huu Wa fanya biashara sasa wana nguvu kuliko serikal Yang. Wabunge wengi Wa.CCM ni Wa fanya biashara kama Abood shabiby na wengine weng so.tegea serikali kushindwa
 
naweza kusema umefika muda wa serikali kununua mabasi yao ya kusafirisha abiri hili kuondoa hii kadhia kwa wasafiri, kupitia hivi vyombo vya usafiri vya serikali itawekwa nauli maalum,pia itatoa changamoto ya kibiashara kwa mabasi ya watu binafsi hii pia itasaidia kupunguza migomo kabisa,kwani ukigoma na basi lako bado abiria watasafiri kwa mabasi ya serikali, hivi mnajua kwamba haya mabasi yanagoma siku kwa sababu hawapati changamoto. huu ndio mwarobaini wa hii migomo
 
Kuna haja ya sisi abiria kuchukua hatua dhidi ya ubepari huu,hili nimekishuhudia Sikh kadhaa la mabasi kupnekana kukosa abiria tayari unakuta seat zaidi ya 15 hazina abiria na wakati mwingine inakuwa sawa na nusu kwa nusu ...kwangu hii in nzuri hasahasa wale was njia ya kati mnaweza mkaanza kuchangamka na treni ya mpya ambayo ina nauli wastani kabisa na utulivu was kutosha,waacheni wapandishe manauli yao na waendelee na ajari zao sie tutajua LA kufanya
 
Serikali iimarirshe treni zote Tazara,Reli ya kati na ya Kaskazini na ifufue mashirika Kama KAMATA na Mabasi ya Railway ndio dawa. kwa sasa ombeni mabasi jeshi na ya mashirika.Halafu fungia leseni za hao wababaishaji.

Inaelekea Hii serikali ya JK ianaendeshwa na wafanyabiashara kama vile nchi haina sheria na masharti ya kuendesha biashara.
Hii ndio madhara ya kuwachagua watunga sera ambao ni wafanyabiashara chagueni walalahoi wenzenu 2015
 
Hawa wafanyabiashara ni tatizo kubwa katika hii nchi...............
yaani kwanza haya mabasi hatujaona wanatoa tamko lolote lile juu ya ajali zinazotokea na kugharimu maisha yetu, lkn eti apa wanatakataa kisa nauli. Nauli yenyewe ukipiga hesabu ni sh 700-1500 kwa safar ndefu.

sasa apa wanachokitaka eti kugoma na sisi abiria tugome kupanda kwasabb ya ajali wanazotusababishia, imagine vilema wangapi wanazalishwa kupitia hizi ajali, achili mbali wanaoachwa wajana ama wagane, na watoto yatima

Kwenye ajali naomba usilalamike abiria mwenzangu, hakuna anayependa ajali na ajali hutokana na mambo mengi tu. Ukifatilia ajili nyingi hizo ulizosikia wewe hivi karibuni na madereva na hupoteza maisha(Huyu dereva ndo mtu ambaye huwa anaiona ajali yote na jinsi gari inavyomshinda)

Acha madereva na wenye mabasi waexpress matatizo yao kupitia mgomo kwa sababu wakifuata taratibu majibu yanayotoka serikalini huwa hayaridhishi.

Mgomo at the end of the day huwa unasaidia, Imagine mie mpanda basi miaka ya 2008 nilikua na uwezo wa kufika MWZ toka DAR saa 2 usiku na barabara ilikua haijakamilika kipande kirefu cha Singida hadi Dodoma. Sasa angalia sahizi mabasi kufika siku hiyo hiyo toka MZA/DAR DAR/MZA ni majaaliwa yani uhakika zaidi ni siku inayofuata na ajali ndo zimepamba moto sasa tueleweje.?

Pliz acha watu wafikishe ujumbe
 
Huu utakuwa wa nchi nzima, TABOA wamekataa na hawakubaliani na nauli mpya iliyowekwa na SUMATRA

Leo mpaka sa sita wasipopata jibu hawatakata ticket. Na mgomo kesho utakuwepo kama kawa.

Mkurugenzi wa sumatra yeye kasema kuwa Taboa hawajui taratibu kwani taratibu zipo badala ya kugoma.

=============================



Chanzo: Nipashe



Tumechoka nao serikali itupe mkopo tununue yetu
 
Back
Top Bottom