Mgomo wa mabasi wanukia tena

Mgomo wa mabasi wanukia tena

Sheria za nchi lazima zifuatwe. Safari hii serikali isikubali kuyumbishwa na wahuni wachache. Mmiliki akigoma fungia yeye leseni halafu leta bus la jeshi wakati mabasi mengine yanaagizwa china au kenya au brazil au afrika ya kusini na matajiri wenye uchungu na Tanzania. Wamiliki hawa uchwara wajue kwamba kuna watu wana mihela imekaa tu wanatafuta investment opportunities kama hizo. Kova hakuna tena kusema wamiliki oyeee. Mtu anagoma toa basi lake UBT funga leseni.
 
Nafurahi sanaaaaa kunapokuwa na migomo hii maana hatuendi kazini tunajipigia midudu tu hapa kona bar kama hatuna akili nzuri
 
kama serikali inajali wananchi wrote ,basi hakuna haja ya kufanya haraka,

Imarisha treni(hii ni amri)
Rudisha mabasi ya kamata

Rudisha mabasi ya Ushirika ya kanda

Tunataka tuachane na kina Abood,Hood ,shabiby ,ngorika majinja nk
 
naweza kusema umefika muda wa serikali kununua mabasi yao ya kusafirisha abiri hili kuondoa hii kadhia kwa wasafiri, kupitia hivi vyombo vya usafiri vya serikali itawekwa nauli maalum,pia itatoa changamoto ya kibiashara kwa mabasi ya watu binafsi hii pia itasaidia kupunguza migomo kabisa,kwani ukigoma na basi lako bado abiria watasafiri kwa mabasi ya serikali, hivi mnajua kwamba haya mabasi yanagoma siku kwa sababu hawapati changamoto. huu ndio mwarobaini wa hii migomo

we naye unaongea nini!?? hiyo train anaiendesha nani? kivuko cha kigamboni, mbona kote huko ni shida tupu, sembuse biashara ya mabasi!!!viwanda vyote vilivyokuwa chini ya serikali viko wapi? mkuu uchumi wa namna hiyo serikali ilishatoka na dunia ya sasa huwezi kurudi huko. Tatizo la tz hicho kiburi cha TABOA, kinakuwepo kutokana na wenye mabasi hayo ndio viongozi wa serikali, hao unao waona eti mwenyekiti wao ni boya tu wenywewe, wako nyuma, tena ndio wasimamizi wa hizo sheria, unategemea nini hapo? mwaka juzi EWURA, si walikuwa wanapanga bei elekezi za mafuta kila mwezi, uliza kilichowapata, leo unawasakia tena??? hii nchi hadi midanganyika itakapopata akili ya kusema usitegemee hao mabepari kuwa ndio viongozi, nawakujali we masikini. Na ndio maana nchi imekuwa kama haina mwenyewe, hata hao mawaziri wanashindwa, kupambana na system.
 
Serikali iimarirshe treni zote Tazara,Reli ya kati na ya Kaskazini na ifufue mashirika Kama KAMATA na Mabasi ya Railway ndio dawa. kwa sasa ombeni mabasi jeshi na ya mashirika.Halafu fungia leseni za hao wababaishaji.

Inaelekea Hii serikali ya JK ianaendeshwa na wafanyabiashara kama vile nchi haina sheria na masharti ya kuendesha biashara.
Hii ndio madhara ya kuwachagua watunga sera ambao ni wafanyabiashara chagueni walalahoi wenzenu 2015
hao wafanyabiashara, kwenye kampeni za urais ndio mnawafuata kuchangia chama, kwanini nao wasilipwe fadhira?? na ndio hao hao wanaohakikisha fulani amekuwa rais, badaye unategemea nini?! Wapumbavu ni wananchi, na hali itaweza kuwa mbaya zaidi endapo yule jamaa atakuwa raisi kwani wapambe wake ni ma MAFIA TUPU, na ndio wengi wanasumbua nchi hii, sasa wanataka kaa jikoni kabisa, wale mavidali na maini tupu.
 
ngoja nikaweke boda boda yangu full tank naona siku za kupiga hela zinakaribia...
 
wawekeze kwenye usafiri wa anga sasa, maana hawa jamaa tumeshawachoka, wao hawajui taratibu??
 
Nafurahi sanaaaaa kunapokuwa na migomo hii maana hatuendi kazini tunajipigia midudu tu hapa kona bar kama hatuna akili nzuri
Kigogo watu wanawaza habari za uchumi kudhorota siku za migomowe unawaza kupiga wadudu. Haahahaaaaah heshima kwako mkuu
 
Last edited by a moderator:
Kwenye paragraph No.2 ni kuwa tayari makampuni mengine hayakati tiketi na wengine wanawapa abilia two options kuhusu kesho kwamba kutakuwa na safari au lah!.
 
Asee mdau hawa wamiliki puuzi sana hao, yaani wanachong'ang'ania hata hakina mantiki kwa upungufu waliokubaliana na ambao leo wanaupinga tena.
Kama sikosei ni hv mfano, Dar -Moro nauli shs 7500, hivo kwa nauli mpya bi shs 6900 tofauti ni 600.

Wakati huohuo kwa sasa kuna wapiga debe ambaye akikuona na kukufuata kwa nyuma unaingia ofc ya kukata tiketi unakata na kuondoka yeye anaingia na kusema kakuleta anapewa 1000.

Sasa basi hiyo ya 600 na hiyo ya 1000 wapi kuna hasara?

kwani nauli mpya zipoje

Nashukuru serikali yangu kwa taarifa nilizopata kuwa train ya Dar -Arusha ipo tayari endapo watagoma kesho.
Kwa kuongezea, fungia wote hao watakaofanya upumbafu huo.
Na mabasi ya jeshi zaidi ya 200 yapo tayari kutoa huduma nchi nzima.
 
Back
Top Bottom