Mgomo wa mabasi moshi na arusha watikisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa mabasi moshi na arusha watikisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dm2000inter, Jul 9, 2012.

 1. d

  dm2000inter Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ndugu zangu wana JF,
  Tangu asubuhi ya leo hakuna usafiri wa kutoka Moshi kwenda Arusha wala kutoka Arusha kwenda Moshi. Hii inatokana na mgomo mkali kuwahi kuonekana ambao ulianza leo saa 11:00 Alfajiri. Mgomo huu umesambaa na kuhusisha mabasi yote ya daladala maarufu kama Hiace. Pia unahusisha mabasi yote ya wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro. Wamiliki wa mabasi wanapinga ongezeko la parking fee katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi ambao umepanda kutoka sh1,000 kwa siku kwa mabasi madogo hadi sh1,500 na sh1,000 hadi sh2,000 kwa mabasi makubwa ya abiria. Hoja yao ni kwamba kila Halmashauri wanalipa Parking fees ambazo ukitoka Arusha hadi Dar Es Salaam wanatakiwa kulipa ushuru wa aina hiyo katika stendi zipatazo 10 na kwa hesabu rahisi wanalipa karibu sh400,000 kwa mwezi. Wakati Halmashauri zina ruksa ya kupandisha ushuru bila hata kuwashirikisha wadau, wamiliki wa mabasi wanakataliwa kupandisha nauli licha ya gharama za uendesha kuongezeka hasa kutokana na ongezeko la bei ya mafuta. Athari za mgomo ni kubwa. Abiria wanatembea kwa miguu. Huduma kwenye ofisi mbalimbali zimeathirika.
  Naomba kuwasilisha
   
 2. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,509
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Hoja za Madereva ni za msingi kabisa
   
Loading...