Haaaah! Eti Umasikini???????? Tanzania tuwe na subira! Mnataka kunikataa kichwa changu? Hizi ni baadhi ya statements za VC wa Taasisi ya Nelson Mandela akijaribu kuzima mgomo unaoendelea ndani ya kampasi hapa A. town.
Wadau leo nikuwepo hapa hasa baada ya kupata taarifa za tukio hili. Mwanafunzi wa hapa anatakiwa kupewa hela ya utafiti sh. 12.5 milioni kwa Masters na 37.5 milioni kwa PhD.
Umekuwa hivi:
Mwezi wa 11 mwaka jana wanafunzi walipitishiwa proposal zao na bajeti inayokidhi kumaliza mahitaji yake. Baada ya kupitishwa kwa bajeti hizi kukawa na mchakato wa kamati ya Utafiti ambayo ilipitisha hela hizi.
Baada ya kupitishwa ikatokea tatizo hasa nani wa kusimamia hela za utafiti. Supervisor au DVC-Resaerch. Ikawa ni DVC. Sasa nani atanunua mahitaji kama vifaa vya maabara ya kemikali, uongozi ukajipa majukumu yote. Hii ilipingwa na wanafunzi wakiangalia mfumo wa manunuzi ya serikali.
Baada ya hapo, wanafunzi wakaanza kuomba hela. Mfano, ukiomba imprest ya sh. 2.0 milioni unakuta unapewa sh. 1.0milioni. Wanafunzi wakawawanaumia tu.
Kibaya zaidi imekuwa hivi. Wanafunzi wameingia mikataba ya hela ya kujikimu (kila mwezi na utafiti). Baada ya kuanza kutoa cheki za hela wakasema hela ya utafiti inakatwa kwenye hela ya kujikimu. Hivyo, mwanafuzi atakaye fanya utafiti kwa siku zaidi ya 90 hata pata hela tena mapaka anaondoka chuo. Hili ni tatizo.
Wanafunzi wanauliza. Kuna hela ya utafiti na kujikmu na kuna mikataba tofauti, je imekuweje?????
Tatizo ndo hilo wakuu. Na wamesema hawatafanya kazi yoyote mpaka watakapopata ufumbuzi wa tatizo hili.
Mimi ninavyo amini hapa kuna dili za MACCM. Wamepata fedha kwa migongo ya wanafunzi lakini hawataki kuitoa.
THANX GUYZ