GE2025 Mgombea wa urais wa chama Makini aahidi ekari 5 kwa kila kijana endapo atashida

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mgombea Urais wa Chama cha Makini, Coaster Kibonde, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), akiahidi kwamba iwapo ataibuka mshindi, kila kijana wa Kitanzania mwenye umri kuanzia miaka 21 atapewa ekari tano za ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Kibonde anakuwa mgombea wa nne kuchukua fomu, akitanguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt. Emmanuel Nchimbi (CCM), Kunje Ngombare Mwiru na Chumu Abdallah Juma wa Chama cha Wakulima (AAFP), pamoja na Hassan Almas na Ally Hassan wa NRA.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 10, 2025 jijini Dodoma mara baada ya kuchukua fomu, Kibonde ambaye aliambatana na mgombea mwenza wake, Azza Haji Suleiman, alisema serikali yake inalenga kuhamasisha vijana kuingia kwenye kilimo cha kisasa chenye tija, ili kuachana na kilimo cha jadi kisicholeta manufaa ya kudumu.

“Tutafanya kilimo cha umwagiliaji ili kuachana kabisa na kilimo cha kutegemea mvua ambacho ni kilimo cha umasikini. Maana ya Chama Makini ni maarifa; kila kijana tutampatia ekari tano kwa ajili ya kulima kwa kutumia matrekta,” alisema Kibonde.

Alitaja elimu, kilimo na afya kuwa vipaumbele vikuu vya chama chake, akisisitiza dhamira ya kuondoa umaskini kwa Watanzania.

Kwa upande wa elimu, Kibonde alisema itakuwa kipaumbele cha kwanza, akiahidi kuhakikisha kila kijana anapata elimu ya kiwango cha kimataifa.

“Ukimnyima Mtanzania elimu ni sawa na kumfunga gerezani maisha. Tutahakikisha elimu bora inayopatikana duniani kote inamfikia kijana wa Kitanzania,” alisema.

Katika sekta ya afya, Kibonde aliahidi kujenga hospitali katika kila kata na kuzipatia vifaa tiba vya kisasa, sambamba na kuongeza idadi ya wataalamu wa afya kupitia uwekezaji mkubwa kwenye elimu ya sekta hiyo.

Aidha, ametangaza mpango wa kuanzisha bima ya afya kwa wote itakayojulikana kama MakiniCare, yenye lengo la kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora bila ubaguzi.

Screenshot 2025-08-10 175153.png
 
Watu wa Mtwara,DSM hiyo ardhi wataitolea wapi
 
Kama vyama vyao tu vipo dhoofu ili hali, huo uchumi wanaoutaja watauwezea wapi?
 
Hawa nao waache maigizo!!
 
Back
Top Bottom