Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,559
- 3,953
Majalio Paul Kyara, mgombea urais wa Tanzania na Katibu Mkuu wa chama cha Sauti ya Umma (SAU), amepiga kura leo katika kituo cha kupigia kura cha Mbuyuni Changanyikeni, Dar es Salaam.
Kyara aliwasili katika kituo hicho akiwa na mkewe, na wote walishiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Kyara aliwasili katika kituo hicho akiwa na mkewe, na wote walishiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.
AHADI ZA MAJALIO IWAPO ATAKUWA RAIS WA TANZANIA
Mwaka 2005, Majalio alipokuwa na umri wa miaka 25, alijitokeza kuwania jimbo la Kibiti, Pwani. Mwaka 2010, aliingia ulingoni jimbo la Kibaha Mjini. Alirejea tena Kibaha Mjini mwaka 2020. Mara zote hizo aliwania ubunge kwa tiketi ya SAU, lakini hakufanikiwa.
Kumbukumbu hizo ni kuonesha kwamba Majalio amekuwa kwenye siasa za ushindani kwa miongo miwili. Ndani ya kipindi hicho, Tanzania imefanya Uchaguzi Mkuu mara nne na Oktoba 29, 2025, utafan-yika wa tano. Mara hizo tano, Majalio ameshiriki moja kwa moja majaribio manne; ubunge mara tatu na urais mara moja. Ni Uchaguzi Mkuu wa 2015 pekee ndiyo Majalio hakushiriki.
Majalio anasema akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atawajenga wananchi, hasa watumishi wa umma, wawe na hofu ya Mungu. Anaamini kuwa taifa likiwa na watu wenye hofu ya Mungu, amani, upendo na uadilifu vitashamiri.
Anasema ukosefu wa maadili kwenye siasa na utumishi wa umma, chanzo chake ni watu kukosa hofu ya Mungu. Anataka kulishughulikia hilo kwa nafasi ya kwanza akiwa Rais.
Majalio anasema kuwa Serikali ya SAU, ambayo yeye ataiongoza, itajikita kwenye mambo matatu am-bayo ni kilimo, viwanda na teknolojia. Anafafanua kuwa utafiti waluoufanya umewapa majibu kwamba tatizo kubwa la ajira Tanzania litapata utatuzi endapo mambo hayo matatu yatashughulikiwa kwa pamoja.
Ahadi ya Majalio, kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya SAU, ni kwamba ndani ya miaka mi-tano, kupitia nguvu kubwa watakayoiweka kwenye kilimo, viwanda na teknolojia, wanatarajia kuten-geneza ajira milioni 10.
Kilimo Uhai ni programu ambayo Sau wanaahidi kuja nayo, kwa kuhakikisha kunakuwa na matumizi ya mbegu za asili, vilevile kilimo cha kisasa bila kemikali.
Mkazo wake kwenye mifugo ni kuwa machinjio yatakuwepo vijijini. Mijini na nje ya nchi zitasafirishwa nyama. Anatoa mfano kuwa kutoa ng’ombe Shinyanga kumsafirisha hadi Dar es Salaam kuchinjwa ni makosa kwa sababu Dar hakuna malisho bora. Ubora wa nyama unapungua njiani kwa kutandikwa, pia ukosefu wa chakula husababisha ng’ombe wale mchanga Dar.
Majalio anasema ngozi pia ubora wake hupungua kwa sababu njiani wanyama wanachapwa bakora. Kingine, ng’ombe huweza kupata magonjwa, matokeo yake ngozi hupungua ubora. Anaeleza kuwa kitendo cha wanyama kuchinjwa vijijini kitasaidia kupatikana nyama bora, pia ngozi safi.
Akichambua zaidi, Majalio anasema mabaki ya ng’ombe Dar es Salaam yanatupwa na kusababisha uchafu pamoja na uharibifu wa mazingira. Wakati vijijini, yangetumika kama mbolea. Anatoa mfano wa hali ya hewa ilivyo mbaya Soko la Shekilango, Ubungo, kwa sababu kuku huchinjwa sokoni hapo. Anaamini kwamba kuku wangechinjwa vijijini kungeepusha uchafuzi huo wa hali ya hewa, lakini pia mabaki hayo ya kuku yangekuwa mbolea vijijini.