Mgombea urais anapokiri hajui siasa!

Mgombea urais anapokiri hajui siasa!

p.38

Member
Joined
Sep 3, 2015
Posts
34
Reaction score
7
Urais wa nchi ndiyo wadhifa mkubwa katika Taifa letu. Siasa kwa nijuavyo mimi, ni kitendo cha kuongoza mambo ya watu. Kwa maana hiyo, Rais anapaswa kuwa mwanasiasa mahiri ili kuliongoza taifa na watu wake katika mambo ya ndani ya nchi na yale yahusuyo medani ya kimataifa.

Wiki iliyopita nilikuwa nafuatilia hotuba ya mmoja wa wagombea urais aliyoitoa kwenye mkutano wake wa kampeni mjini Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri unaomilikiwa na chama chake. Mkutano wake kwa hakika ulijaa watu wengi na kwa lugha ya kisasa nadiriki kusema kulikuwa na ‘ nyomi’ akiwamo Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete.

Mgombea urais huyo akayatamka maneno ambayo yameniacha na tafakuri nzito kuhusu nini itakuwa hatima ya nchi yetu iwapo mgombea huyo atachaguliwa kuwa Rais. Kwa mashabiki au kwa manazi wa kisiasa na wakereketwa wa chama, maneno aliyoyatamka mgombea huyo yalipita na kutoweka katikati ya sauti za washangiliaji.

“Mimi sifanyagi (sifanyi) siasa, na kwa bahati mbaya naweza nikawa si mwanasiasa mzuri. Mimi kwangu ni kazi tu” yalikuwa maneno ya Dk John Magufuli. Hapa kazi ipo, kwamba rais ajaye anaweza akawa hajui siasa vizuri! Sikuamini masikio yangu kwa sababu ingekuwa ni katika nchi nyingine, kauli hii ingeweza kumkosesha urais kwa sababu wananchi wanamtegemea rais wao aijue vizuri siasa ili awaongoze vizuri.

Kama si kufanya siasa, chama cha siasa kitatawala vipi nchi? Sera za chama, ilani yao ya uchaguzi na maamuzi mbalimbali atakapokuwa madarakani yanategemea siasa kwa asilimia kubwa. Diplomasia na nchi za nje na mashirika ya kimataifa yanahitaji rais mwenye upeo mkubwa kisiasa hasa katika zama hizi za ulimwengu wa utandawazi.

Utatuzi wa masuala matatizo mengi ya wananchi kijamii, kiuchumi, kielimu na kujenga utawala bora ni mchakato wa kisiasa. Hata utekelezaji wa kauli zake kwamba anataka mabadiliko bora na si bora mabadiliko ni jambo linalotaka mchakato makini wa kisiasa.

Vinginevyo itakuwa ni ubabe wa kisiasa badala ya mabadiliko ya kisiasa. Pengine tuseme mgombea huyo alipotaja ‘siasa’alikuwa na maana ile ya mtaani yaani ujanja ujanja, hila, ghiliba, uongo au porojo?

Lakini ukiiangalia kauli mbiu yake ‘Hapa ni kazi tu’ unaelewa kwamba huyu atakuwa rais mtendaji zaidi kuliko kuwa mwanafikra na mwanadiplomasia (stateman). Ikiwa hivyo, napata shaka kubwa kwamba tutashuhudia rais mwenye kutegemea ‘kuchorewa ramani’ na wanasiasa kwa kuwa yeye hajui siasa.

Katika hali hiyo, anakuwa kama Waziri Mkuu badala ya kuwa Rais. Hofu yangu ni kwamba serikali yake itakuwa ya kiimla inayoongozwa na utendaji wa mtu mmoja jambo ambalo litakuwa ni hasara kwa Taifa.

Kama rais hajui vizuri siasa, ni ipi hatima ya vyama vya siasa, asasi za kijamii, vyombo vya habari na wadau wengine wa maendeleo ya nchi? Ni wazi CCM itahitaji kuwekeza vya kutosha katika kutengenezea timu yenye weledi wa siasa pale Ikulu ya Magogoni ili kuweka uwiano sawa kati ya ‘Hapa ni kazi’ tu na ule upande wa rais unaohitaji weledi wake kisiasa ili kuivusha nchi salama. Vinginevyo kaulimbiu ‘hapa kazi tu’ itakuja kuitokea puani hata CCM yenyewe.

Kila kitu ni siasa

Ulimwengu wa sasa karibu kila kitu ni siasa. Ili kujenga uchumi imara hahitajiki mtu kuwa mchumi mzuri pekee bali pia anahitajika kujua siasa za uchumi. Hivyo hivyo kutafsiri ilani ya uchaguzi ya chama kutoka kwenye maneno kwenda kwenye vitendo. Rais anapaswa kuijua vizuri siasa kwa sababu ilani ni tamko la kisiasa, ndiyo maana hata isipotekelezwa vizuri hakuna mtu anayefikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Sasa mtarajiwa wetu ambaye anakiri hadharani kuwa hajui siasa, hayo atayafanyaje? Ndiyo maana amekaririwa akilinganisha kusambaratika kwa Libya kuwa ni matokeo ya wananchi kutaka mabadiliko. Wanaojua siasa wasingeweza kulinganisha mabadiliko ya Libya na haya ya Tanzania ambayo hata yeye anakiri kutambua kuwa wananchi wana kiu ya mabadiliko.

Mbona hasemi mabadiliko yaliyotokea Tunisia ambayo ndiyo nchi ya kwanza kwa wananchi kuleta mabadiliko? Nadhani mabadiliko ya Tanzania yanafanana zaidi na yale ya Tunisia kwa kuwa yalitokana na wananchi wenyewe kuuchoka utawala wa rais Zainul Abidin. Yale ya Libya yalishinikizwa na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na yalitokea kwa vita kumtia adabu Muammar Gaddafi kwa tuhuma za kuunga mkono ugaidi wa kimataifa wakati haikuwa kweli.

Kwa kutokujua siasa, ndiyo maana anadhani kuondoa tatizo la rushwa ufumbuzi wake ni kuanzisha mahakama ya rushwa ambayo kwa maneno yake mwenyewe “ili mafisadi na wala rushwa wafungwe haraka, Watanzania waishi kwa raha!”. Tujiulize hivi kweli kuiondoa rushwa iliyokita mizizi kutafanikiwa kwa kuyafunga mafisadi na wezi tu? Mbona tulikuwa na sheria za uhujumu uchumi na bado uchumi ukahujumiwa?

Kwa mwanasiasa mweledi atatafuta chanzo na kiini cha rushwa badala ya kuanzisha mahakama ya rushwa, ambayo itaendeshwa na mahakimu na majaji walewale ambao wanahudumu katika mahakama zilizopo sasa. Kutegemea kuunda mahakama ya rushwa kumaliza tatizo la rushwa ni sawa na kutegemea kumaliza ugonjwa wa malaria kwa kugawa vyandarua vyenye dawa tu!

Bahati aliyonayo mgombea huyu wa CCM ni kwamba wananchi wengi wanaowasikiliza wagombea wa nafasi mbalimbali wana uelewa mdogo au wanafanya hivyo huku tayari wakiwa na mapenzi ya kufa kwa wagombea wao. Kibaya zaidi, katika mfumo wa kampeni wagombea hawahojiwi na hivyo hata wakisema chuya wapenzi wanajua ni mchele na watashangilia.

Ifike wakati vyombo vya habari visiishie tu kurusha matangazo ya wagombea au kuandika bali wayachambue yale yanayosemwa kujenga hoja zenye kuwafumbua macho na masikio wapigakura wawaelewe wagombea wanasema nini na kina athari gani kwa sababu kile kinachosemwa majukwaani katika kampeni wananchi wengi hawakielewi.

(Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya maendeleo. 0762 715311)
 
Lowasa ndio chaguo sahihi kwa watanzania
 
Mchambuzi uko vzr sana big up kuna mda alisema pia samia ndo atakuwa makam wa kwanza wa rais mwanamke endapo watapewa ridhaa hapa naona wamebug
 
"Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira".

Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha "wateule" na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao.

Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakatutazama na kuuliza, "kulikoni?". Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya "malofa" wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: "Kama ni hivyo, kwa nini wasile keki na mihogo?

"Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara yao pendwa,vijana wenye vipaji vya mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu",wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wanaambiwa ni majangili huku tembo na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah!

wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona wanawapigia madai yao sahihi yamekuwa kelele wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwatesa waandishi wa habari zao.

Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni "vijisenti", au fedha ya mboga, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa "Wapige mbizi" na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa "Ni heri wale nyasi"…

Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili.

Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM."ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain".

Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!
 
Kutojua siasa wakati upo kwenye Siasa ni sawa na mtu aliye katikati ya Bahari/jangwani halafu amepoteza dira na mwelekeo!Hata awe mpiga mbizi mahiri namna gani atapiga mbizi kuelekea upande gani?
 
magufuli ana upeo mdogo sana......anasema siasa ni uongo.Na anasema hajui siasa.
 
magufuli kwake kazi tu siasa na uongo wafanye mafisadi kama Lowasa na wahuni wenzake.
 
magufuli ana upeo mdogo sana......anasema siasa ni uongo.Na anasema hajui siasa.

mkuu wewe kiazi kweli sisi tunataka watendaji hatutaki wanasiasa kwani siasa zimevuruga nchi nyingi na kuharibu uchumi kwa sababu ya siasa.
 
Kwa hiyo lowasa ndo anajua siasa na pia wewe unauelewa mkubwa wa siasa!!!, usifuate Mkumbo 'siasa ninini ' ukijua definition na etymology wala usinge andika haya. Tuachieni amani yetu ya Tanzania iendelee na sio uroho wa kugawa wananchi kwa udini na ukabila na ukanda. Kachukueni Helkopiter ya Gwajima mtembelee mang'ombe ya lowasa.
 
Yeye atakuwa raisi kivuli tuu. Jk na team yake wanaendelea kututawala kama ccm ikishinda.
 
Asijejishughulisha na siasa ajiandae kutawaliwa na mambumbumbu.
Alisema Plato
 
Kwa hiyo lowasa ndo anajua siasa na pia wewe unauelewa mkubwa wa siasa!!!, usifuate Mkumbo 'siasa ninini ' ukijua definition na etymology wala usinge andika haya. Tuachieni amani yetu ya Tanzania iendelee na sio uroho wa kugawa wananchi kwa udini na ukabila na ukanda. Kachukueni Helkopiter ya Gwajima mtembelee mang'ombe ya lowasa.

hapa magufuli alishindwa kujieleza kama kawaida yake, nilivyo mwelewa yeye sio mwanasiasa akimaanisha hizi siasa za maji taka za bongo, siasa za maji taka hata kwenye mambo ya msingi which I support him
 
Akishapita anayejua siasa lowassa nashauri serikali yake isimuache magufuli kuwa waziri wa ujenzi maana hiyo ndio kazi anayoiweza.
 
Kwa hiyo lowasa ndo anajua siasa na pia wewe unauelewa mkubwa wa siasa!!!, usifuate Mkumbo 'siasa ninini ' ukijua definition na etymology wala usinge andika haya. Tuachieni amani yetu ya Tanzania iendelee na sio uroho wa kugawa wananchi kwa udini na ukabila na ukanda. Kachukueni Helkopiter ya Gwajima mtembelee mang'ombe ya lowasa.

Unaongea hivyo ilikupoteza tageti,safari hii lazima tuwabomoe!manake hakuna namna nyingine.
 
Kwa hiyo lowasa ndo anajua siasa na pia wewe unauelewa mkubwa wa siasa!!!, usifuate Mkumbo 'siasa ninini ' ukijua definition na etymology wala usinge andika haya. Tuachieni amani yetu ya Tanzania iendelee na sio uroho wa kugawa wananchi kwa udini na ukabila na ukanda. Kachukueni Helkopiter ya Gwajima mtembelee mang'ombe ya lowasa.
kwanini mnaache kuchangia hoja na kutoa point za ushawishi tukawaelewa, badala yake mnakimbilia kusema vita,amani vita Amani. Inakuwa kama vya upinzani ni kama rebels hawapo kisheria. Mlio kwenda shule jamani jaribuni kuelimisha wengine badala ya kuendekeza maneno ya wanasiasa njaa, ambao wanasema kuchagua upinzani wataleta vita. Siyo kweli. Chama tawala kina vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Kama ni kuvunja Amani na kuanza vita basi ni yule aliye na vyombo ndiye atasababisha haya. Natuelimishe watu umhimu wa vyama vingi kwa manufaa ya taifa. vitisho vya kuvunjika Amani viachwe na vyombo vya dola vifanye kazi yake
 
"Ili Taifa Letu Liendelee Linahitaji Watu, Ardhi Na Siasa Safi" Sasa Kuna Mgombea Urais Mmoja Anajinasibu Kua Yeye Hua Sio Mzuri Kweye Siasa Ni Mtendaji Tu! Haya Wadau Sasa Tusemeje Sisi? Hivi Kweli Kwa Changamoto Hizi Zinazotukabili Hivi Sasa Hatuhitaji Kiongozi Mwanasiasa? MAAJABU HAYA! Nijuavyo Mimi Kwa Nchi Yeyote Inayoheshimu Misingi Ya Demokrasia Kiongozi Mkuu Wa Nci Lazima Awe Mwanasiasa Mzuri Na Zaidi Ya Hapo Ni Kiongozi Wa Kiimla, Hivi Tunakwenda Wapi Watanzania?
 
"Ili Taifa Letu Liendelee Linahitaji Watu, Ardhi Na Siasa Safi" Sasa Kuna Mgombea Urais Mmoja Anajinasibu Kua Yeye Hua Sio Mzuri Kweye Siasa Ni Mtendaji Tu! Haya Wadau Sasa Tusemeje Sisi? Hivi Kweli Kwa Changamoto Hizi Zinazotukabili Hivi Sasa Hatuhitaji Kiongozi Mwanasiasa? MAAJABU HAYA! Nijuavyo Mimi Kwa Nchi Yeyote Inayoheshimu Misingi Ya Demokrasia Kiongozi Mkuu Wa Nci Lazima Awe Mwanasiasa Mzuri Na Zaidi Ya Hapo Ni Kiongozi Wa Kiimla, Hivi Tunakwenda Wapi Watanzania?

Mtaje basi huo kiongozi tumjue
 
mwanasiasa mzuri sisi tunaamini ndiyo kiongozi mzuri na tunaamini kiongozi anatokana na siasa.kama yeye siyo mwanasiasa basi siyo kiongozi mzuri.
 
"Ili Taifa Letu Liendelee Linahitaji Watu, Ardhi Na Siasa Safi" Sasa Kuna Mgombea Urais Mmoja Anajinasibu Kua Yeye Hua Sio Mzuri Kweye Siasa Ni Mtendaji Tu! Haya Wadau Sasa Tusemeje Sisi? Hivi Kweli Kwa Changamoto Hizi Zinazotukabili Hivi Sasa Hatuhitaji Kiongozi Mwanasiasa? MAAJABU HAYA! Nijuavyo Mimi Kwa Nchi Yeyote Inayoheshimu Misingi Ya Demokrasia Kiongozi Mkuu Wa Nci Lazima Awe Mwanasiasa Mzuri Na Zaidi Ya Hapo Ni Kiongozi Wa Kiimla, Hivi Tunakwenda Wapi Watanzania?
Kama unaogopa taja angalao chama chake tutaelewa
 
Back
Top Bottom