Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha African Democratic Alliance (ADA - TADEA), Georges Bussungu amenadi sera za chama hicho kwa wakazi mkoa wa Tabora, akiahidi kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo utekaji kwa kununua helikopta maalim kwa Polisi(attack helicopter) kila mkoa zitakazotumika kukabiliana na uhalifu
Bussungu amesema hayo Oktoba 13, 2025 katika, Kata ya Chem Chem, Manispaa ya Tabora akisema kuwa helikopta hizo zitawasaidia Polisi kufika kwa haraka sehemu za matukio kudhibiti uhalifu na hata wale wanaofanya uhalifu na kukimbia wataweza kudhibitiwa kwa kutumia chombo hicho ambacho kitakabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi(RPC) mikoa yote nchini
"Tunataka Polisi kila mkoa wawe na helikopta, jambazi likitoloka helikopta inaruka, nia yetu ni kwamba hii mambo ya kutekwa sijui kuuwawa hatutaki kusikia sisi, hatutaki kusikia mtu kapotea " Bussungu amesema
Aidha, katika kuwaboreshea mazingira rafiki kwa wafugaji, amesema serikali yake itaruhusu mifugo kuchungwa kwenye maeneo ya hifadhi za ili kuwaepushia usumbufu wa kuhama hama kutafuta malisho