GE2025 Mgombea Udiwani kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD) adaiwa kutoweka

GE2025 Mgombea Udiwani kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD) adaiwa kutoweka

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea Udiwani kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD) katika Kata ya Kinyerezi, Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Seleman Shimbi, anadaiwa kutoweka na hajulikani alipo kwa zaidi ya siku sita sasa.

Katibu Mkuu wa chama hicho, ambaye pia ni Mgombea Urais, Doyo Hassan, alisema jana kuwa Shimbi alionekana mara ya mwisho nyumbani kwake Oktoba 14, 2025, kabla ya kutoweka katika mazingira yanayoibua shaka. Alisema juhudi za familia, marafiki na viongozi wa chama kumtafuta hazijazaa matunda.

"Tulifanya jitihada za kumtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio, ndipo tukapeleka taarifa katika Kituo cha Polisi Madale mnamo Oktoba 15, 2025, na tukapewa kumbukumbu namba MDL/RB/3903/2025," alisema Doyo.
1761221348289.png
 
Back
Top Bottom