GE2025 Mgombea Udiwani CCM Kata ya Vibaoni, Marry Chambuya awaahidi wananchi kupata Stendi na Barabara za Mitaa

GE2025 Mgombea Udiwani CCM Kata ya Vibaoni, Marry Chambuya awaahidi wananchi kupata Stendi na Barabara za Mitaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea udiwani kata ya Vibaoni halmashauri ya Mji Handeni mkoani Tanga Marry Chambuya amewaahidi wananchi wa eneo hilo endapo watampa ridhaa ya kuwa diwani wao kwa kumchagua,atasimamia kupatikana kwa kituo cha mabasi jambo ambalo ni moja ya changamoto yao

Akizungumza kwenye mkutano wake kufungua kampeni zilizofanyika katika viwanja vya Soko la Vibaoni Chambuya amesema tayari fidia imeanza kulipwa,hivyo mradi huo unakwenda kutekelezwa ikiwemo kukarabatiwa barabara za mitaa ambazo bado hazijafanyiwa ukarabati

Akifungua kampeni hizo Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Handeni Sophia Masimba akimnadi mgombea huyo amesema serikali ya CCM imetekeleza miradi mingi ya maendeleo,na wananchi wakiwapa ridhaa watakwenda kuendelea kuikalimisha ili iwe na manufaa kwao

Kwa upande wake aliyekuwa mgombea ubunge Handeni Mjini kwenye kura za maoni Sonia Magogo amesema chama kimeweka wagombea ambao watakwenda kusimamia maendeleo yao,hivyo ni vizuri kwenda kuwapigia kura

Vyama mbalimbali vya siasa vipo kwenye kampeni za kujinadi kwa wananchi kwaajili kutoa sera zao ni kitu gani wanakwenda kufanya ili kupewa ridhaa,kwa kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu


 
Back
Top Bottom