Elections 2010 Mgombea Ubunge Tabora abambikizia kesi Dereva wa Daladala

MmasaiHalisi

Senior Member
Jan 15, 2009
192
23
Mgombea ubunge mtarajiwa kupitia chama tawala (CCM) mkoani Tabora Bwana CLEMENT NSANYAMA, ambaye in PLANNING OFFICER WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO, amembambikiziaa kesi kijana aitwaye October,Bwana Clement anamtuhumu Dereva huyo kumchukulia nyumba ndogo yake aliyouipangishia maeneo ya kinondoni,nyuma ya Bonga Bar uchunguzi unilofanya ni kuwa Bwana clement amewahonga police wa kituo cha Oysterbay na kumbambikizia kesi kijana huyo kuwa kamwibia Milioni Tatu,Mbunge huyo mtarajiwa ambaye anaishi Mbagala Mission Pamoja na Familia yake(mke wake ambaye ni Nurse katika Kituo cha afya Mmbagala ZAKIHEMU),pia mefikia hatua ya kumtishia maisha kijana huyo,
Jamani mnaona jinsi CCM inavyo wakumbatia watu washenzi kama huyo bwana,
 
Mkuu MmasaiHalisi,

Hii habari yako naona imekaa kiudaku udaku kwa kuwa haieleweki vizuri. Unahitaji kutoa ufafanuzi wa mambo machache kabla watu hawajaanza kuchangia.

1. Je, ni kweli Bwana October anamega nyumba ndogo ya huyo mgombea mtarajiwa?

2. Unasema amewahonga polisi, una uhakika na hili? Huo uchunguzi uliufanya lini kiasi kwamba ukawa na uhakika kwamba Clement amewahonga polisi au ni kwa hisia tu?

3. Kama ni kesi ya kubambikiziwa na haina ushahidi wa kutosha kijana hawezi kufungwa. Unless kama kijana ameajiriwa na Clement na hivyo Clement akajenga hoja ya kupotea hela wakati kijana huyo akiwa maeneo hayo. Kwa hiyo weka wazi kama October ni dereva wa Clement ama wana uhusiano gani zaidi ya huo wa kumega tundi moja.

4. Umesema Clement amemtishia maisha huyo kijana, ilikuwa lini? Kabla au baada ya kubambikiwa kesi? Je, aliripoti polisi kwamba ametishiwa maisha? Kama hakuripoti, ni kwanini alikaa kimya?

5. Hakuna chama chochote ambacho kinaweza kuwa na info za maisha binafsi ya mtu katika ngazi za huko mtaani. Kwa hiyo kutumia mkasa huu na kusema CCM inakumbatia watu washenzi, sidhani kama ni sahihi.

6. Kama October anamega nyumba ndogo ya Clement, basi wote wawili, yaani Clement na October ni wahuni, na walichofanyiana ni kuonyeshana nani zaidi. Wote wawili wanaweza kuwa na makosa, ni kosa kumega nyumba ndogo ya mwenzako, na pia ni kosa Clement kuwa na nyumba ndogo, japo inawezekana mke wa Clement ameruhusu. So you can not conclude kwamba Clement ni mshenzi, but October nae ni mshenzi kwa kumega nyumba ndogo ya watu, si angetafuta ambaye yuko huru, mbona totoz ziko kibao.

Mwisho, mtu kuwa na nyumba ndogo ni swala binafsi na linagusa maisha ya mhusika kivyake. Kosa nililoliona hapo juu ni hilo la kutishia maisha tu. Hiyo kesi ya kubambikizwa, sidhani kama ina nguvu kama hakuna ushahidi wa kutosha.
 
Back
Top Bottom