tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya ubunge Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Patrick Mwalunenge katika kuhamasisha makundi mbalimbali wajitokeze kwenye mkutano wa mgombea nafasi ya U-Rais kwa tiketi ya chama chao, ameonekana akiuza samaki katika soko la Soweto huku akiwasihi wafike kwenye mkutano waweze kusikiliza sera anazokwenda kunadi mgombea wao wa urais Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo kesho Septemba 4, 2025.
Soma pia: Mwalunenge achukua fomu kugombea ubunge Mbeya Mjini
Mhe. Mwalunenge amefika sokoni hapo na kusalimiana na wafanyabiashara wanaofanya biashara katika soko hilo wakiwemo kinamama wanaouza samaki, nyanya na matunda kisha kuwaeleza faida za kuhudhuria mkutano huo.