Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Jimbo la Hai kupitia CHAUMMA ajitoa kwenye kinyang'anyiro

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
769
1,959
Mgombea Ubunge Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro kupitia CHAUMMA, Ibrahim Kisimbo ametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho akidai kufanya hivyo ni kujichosha kutokana na kazi alizofanya Mgombea Urais wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli

Kisimbo.jpg

MY TAKE: CCM itaendelea kuwa chama bora kwa kwa miaka mingine 50 Tanzania

==

Simbo alitangaza uamuzi huo juzi mbele ya waandishi wa habari, akidai kuwa ameona atajichosha bure kushindana na kutumia nguvu nyingi ilhali ana nafasi nzuri ya kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa kuwa kazi zake zinaonekana waziwazi.

Wagombea ubunge wanaoendelea na kampeni zao katika Jimbo la Hai ni Saashisha Mafuwe (CCM), Mbarouk Mhina (ACT-Wazalendo) na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

“Kuanzia leo (juzi), nimesitisha zoezi lote na nitaunga mkono chama kinachoongozwa na Rais John Magufuli. Nina sababu za msingi, nimeona ninajichosha kutokana na mambo anayoyafanya Rais Magufuli yanaonekana kwenye jamii.

“Kwa hiyo, kwa ridhaa yangu kutoka moyoni, nitaunga mkono chama kinachoongoza serikali.

Hata mwaka 2010, niligombea ubunge wa Hai, lakini kitu ninachokiona tofauti mpaka nikahama, niliona kwamba jamii yenyewe imekubali na mimi ninaangalia mbali sana. Hata kwa nchi za wenzetu zilizoendelea, huwa wanafanya siasa za aina hii.

"Mimi nilichukua fomu ya kugombea ubunge ili kuleta changamoto, lakini baadaye nikagundua siuwezi muziki wa John Magufuli na chama chake. Ninatoa rai kwa vyama vingine, vingekuwa makini, vingemuunga mkono Rais Magufuli," alisema.

Simbo aliongeza kuwa aliamua kuchukua uamuzi wa kujitoa baada kuangalia ilani za uchaguzi za vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo na kubaini Rais Magufuli kwa kutumia ilani ya chama chake na ahadi ambazo yeye (Simbo) alizozitoa mwaka 2015 na sasa zinatekelezeka.

“(Dk. Magufuli) alinifurahisha juzi, alisema kwamba kuna vitu atavifanya ndani ya miaka mitano na vitaisha ndani ya miaka mitatu. Na kwa sababu kazi yake inaonekana na anafanya kazi vizuri na matunda tumeyaona, nina imani ataendelea hivyo hivyo na ninawaomba wananchi tumuunge mkono," alisema.

NIPASHE
 
Hawa washenzi wanafanya mauzauza kwa sababu wana uhakika Wa ruzuku! Kodi zetu zinatumika vibaya sana!
 
Alivyokuwa anagombea hakulijua hilo?
Ama naye anataka ajulikane kama alijaribu kugombea na kishapo kujipendekeza kwa mkuu??

Anaonekana mmojawapo wa mtu mzima hovyo!!
 
Bado wengi watajitoa huko mbeleni, wakiwemo Wa act na cdm.

Sababu kubwa ni fedha za kuhimili kampeni.
 
Hata ukimwangalia tu usoni utagundua kuwa huyu hana akili. Madevu yake ameshindwa kuyapendezesha. Ni lofa kichwani. Na kama ameoa ni vema akamrudisha mke wake kwa wazazi wake maana naye anahitaji kulelewa na kutunzwa.

Amekipotezea chama chake nafasi adhimu ya kuingia bungeni mapema sana. Lofa kabisa.
 
Je huyu mgombea wakati anachukua fomu alikuwa mentally incapacitated?
TUME inapotupa baadhi ya fomu za wagombea msiseme ni kuminya demokrasia, inajaribu kuangalia utimamu wa akili kutokea hata jinsi fomu ilivyojazwa achilia mbali minor errors.

Acheni twende. Na bado. Before 28 oct ndio mtashangaa hata wanaozunguka na mgimbea urasi wanaunga juhudi za jpm
 
Back
Top Bottom