Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,603
Ile standi ya daladala naona mmekuja kumwaga michanga miaka mitano ijayo muache kumwanga miachanga muweke stendi ya kueleweka maana mnapokea kodi za wananchi.
=====================
Mgombea ubunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Geofrey Timoth, ameahidi kuimarisha maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, huku akiahidi kusimamia utekelezaji wa ahadi mpya zilizomo katika Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030. Timoth ameyasema hayo jana Jumapili, Oktoba 5, 2025 wakati akiendelea na kampeni za nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa katika Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, akiwataka wananchi wampe ridhaa ya kuwa mwakilishi wao katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
“Nimekuja kusikiliza kero zenu, kueleza yale tuliyotekeleza na yale tutakayoyafanya tukipata ridhaa yenu tena ili kuhakikisha jimbo letu la Kawe linapiga hatua kimaendeleao,” amesema Timoth. Wakati wa ziara hiyo, mgombea huyo alikutana na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo waendesha bodaboda na bajaji, wazee, wafanyabiashara sokoni pamoja na mama lishe, ambapo amehimiza umoja, amani na ushiriki wa wananchi kupiga kura.