DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Makini, Bw. Coaster Kibonde na Mgombea Mwenza Azza Haji Suleiman, wamejitokeza Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC, Njedengwa Jijini Dodoma, kuchukua fomu ya uteuzi kugombea nafasi ya Urais na kubainisha kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo wakiwa na vipaumbele vitatu vikubwa vya Elimu, Kilimo na Afya.
Akifafanua kipaumbele moja wapo cha kilimo amesema Tanzania imejaliwa kuwa na ardhi kubwa hivyo endapo watapata ridhaa ya kuongoza nchini watahakikisha wanagawa mashamba ekari tano kwa kila kijana na kuhakikisha wanatumia zana bora kwenye kilimo ili wapate tija.