Mgombea Chadema anusurika kuuawa mahabusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea Chadema anusurika kuuawa mahabusu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mgombea udiwani wa Kata ya Mjini Kati, Simba Seif (Chadema), amelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akiwa mahututi baada ya kunyongwa na mahabusu wenzake akiwa kuwekwa ndani.
  Kabla ya kunyongwa, Seif alifikishwa katika Mahakama ya Mkoa jana mchana kwa kile kilichodaiwa na wakala wa kampuni inashughulikia kukusanya ushuru wa kuegesha magari stendi ya mabasi yaendayo mikoani mjini hapa, kwa kuhoji kwanini kampuni hiyo ilikuwa ikikusanya ushuru hadi sikukuu ya Idd el Fitri.

  Baada ya kukamatwa na polisi siku ya Idd, Seif alipewa dhamana na Mwenyekiti wa Wilaya wa Chadema, Derick Magomba, hadi jana alipopigiwa simu na polisi wakimtaka kwenda mahakamani kujibu shitaka lake.
  Kabla ya kesi yake kuanza, Seif alipelekwa mahabusu ya mahakamani hapo na ilidaiwa kuwa askari aliyekuwepo mlangani alimtaka ampe Sh. 20,000 ili asiingizwe ndani.
  Aliposema kwamba hana hela, askari huyo alimwingiza ndani na hapo mahabusi waliokuwa ndani walimlaki kwa kumshambulia na kumnyonga.

  Akizungumza kwa shida katika wodi ya wagonjwa mahututi, Seif alisema wakati akishambuliwa na wenzake, huku akipiga kelele za kuomba msaada, alisikia sauti ya askari aliyepo nje ikimweleza kuwa apigane kama anavyosimama kwenye majukwaa kuhutubia.
  "Pigana kiume kama unavyosimama kwenye majukwaa kuhutubia," Seif alijaribu kumnukuu askari huyo.
  Hata hivyo, kadiri kelele zilivyozidi, watu waliokuwa nje ya mahabusu walimshinikiza askari huyo amfungue mlango ili kumwokoa.

  Lakini ilidaiwa kuwa askari huyo aliwaeleza watu hao kuwa hawawezi kumfanya lolote na anaweza kuwapiga bastola na angewasingizia kwamba mahabusu walitaka kukimbia.
  Hata hivyo, ilielezwa kuwa watu hao waliendelea kupiga kelele na wakaenda kumweleza hakimu ambaye kesi hiyo ilikuwa mbele yake.
  Alieleza kuwa hakimu alimwamuru askari huyo kufungua mlango na ndipo walipomkuta Seifi akiwa mahututi.

  Baada ya hapo alikimbizwa hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.
  Akiwa hospitalini hapo wauguzi walimwekea oksijeni na kumlaza.
  Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Zuberi Mumbesa alifika hospitalini hapo na kumfanyia mahojiano na baada ya kuchukua maelezo yake aliondoka.
  Naye Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema uchungizi zaidi unafanyika.
  Muda wote huo, Seif alikuwa akishughulikwa na wauguzi.

  Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Magomba, alisema chama chake kitafuatilia tukio hilo na kitawachukuliwa hatua watu wote waliohusika.
  Aliwataka wagombea kuacha kufanya mchezo mchafu katika kampeni kwani zinaweza kuleta madhara makubwa hata kumwaga damu.  CHANZO: NIPASHE

  Hivyo hata hao Maaskari pia wanaunga mkono Chama cha CCM? Kasheshe kweli Nchi yetu hii Tanzania.
   
Loading...