Mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Bakari Shingo amewaahidi wakazi wa jimbo hilo kuwa atatumia fedha za mfuko wa jimbo kutatua changamoto zao kwa haraka na kushirikiana nao bega kwa bega katika shughuli za maendeleo.